Mimi mwenzenu nilikuwa mmojawapo wa wakimbiaji wa mabomu ya gongo la mboto.
Ni Kati ya wale waliokimbia kuelekea chanika. Nikiwa huko mstuni kwenye maficho, nilijifunza mambo mengi sana. Kwanza ndiko nilikojua kwamba makambi yote ya jeshi yalimpa kura Slaa, yakamnyima Kikwete, Pili, ndipo nilipojua kwamba watanzania wamemchoka kikwete kwa kumaanisha na si kwa utani.
Watanzania wengi wanasubiri tu muongozaji wa kuwaelekeza cha kufanya ili kwamba waweze kuingia katika maandamano ya kumuondoa Nduli Kikwete.
Watanzania wanatamani uchaguzi urudiwe ili waweze kufanya maamuzi sahihi. wengi wanajuta sana juu ya uamuzi wao wa kumchagua huyu kiongozi dikteta asiyeyahurumia maisha ya watanzania. Wapo waliofika mahali wakaonyesha wazi kuchoka na utawala huu wa kidemokrasia ambao unawaumiza na kuwakandamiza na kuona ni bora utawala wa kijeshi ambao unafahamika kuwa ni wa kikatili kuliko huu wa kidemokrasia ndani ya udikteta na ukatili mkubwa. Watu walikumbushana juu ya hali ngumu ya maisha iliyotokana na kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbli na kuongezeka kwa jumla kwa gharama ya maisha.
Watanzania wapo tayari kuandamana kuanzia sasa, anakosekana tu mhamasishaji. Kama atajitokeza yeyote ambaye yupo tayari kuanzisha hili vagi basi aamini kwamba watanzania wengi watamuunga mkono kwa dhati kabisa. Watanzania wamechoka, na kwa hisia za harakaharaka ni kwamba wanajeshi wanalipua yale mabomu makusudi ili kuongeza hasira za watanzania dhidi ya serikali yao. Na hili linaonekana kupata mafanikio makubwa sana. Maana watanzania wana hasira na Nduli Kikwete kupita kawaida.