Breaking News: Boko Haram wafanya mauaji ya kutisha!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
16,216
2,000
Taarifa kutoka mjini Buni Yadi katika jimbo la Yobe Kaskazini mwa Nigeria, zinasema kuwa watu 24 wakiwemo wanajeshi 11 wameuawa katika shambulizi dhidi ya kambi za wanajeshi.

Inaarifiwa kuwa kundi la Boko Haram ndilo linashukiwa kufanya mashambulizi hayo.
Habari zinazohusiana

Wananchi wanasema washambuliaji waliwasili katika eneo hilo kwa magari kumi ya kawaida na gari moja la kijeshi.

Waliwaambia wanakijiji kutokuwa na hofu kwani nia yao haikuwa kuwadhuru raia bali maafisa wa usalama.

Wanajeshi 11, polisi 13 akiwemo mwanamke mmoja waliuawa.

Pia waliteketeza majengo na magari ikiwemo makazi ya kiongozi mmoja wa kijadi na kituo kimoja cha polisi.

Taarifa zaidi bado zinajitokeza pole pole hasa kwa kuwa mawasiliano yamekuwa magumu kutokana na miundo mbinu mibovu.

Jimbo la Yobe ni moja ya majimbo matatu ambayo serikali imeweka sheria ya kutotoka nje usiku. Licha ya sheria hiyo mashambulizi ya mara kwa mara yamekuwa yakishuhudiwa mengi yakifanywa na Boko Haram.

boko haram.jpg
Wasichana waliotekwa na Boko Haram
:yield:

Source: BBC
 
Kigogo

JF-Expert Member
Dec 14, 2007
20,534
2,000
Nigeria hawana jeshi kabisa....wko busy ku act movie ru..tofyakwaaa
 
mossad007

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
1,165
1,250
Nigeria hawana jeshi kabisa....wko busy ku act movie ru..tofyakwaaa

Ndugu yangu vita dhidi ya ugaidi ndio vita ngumu zaidi kuwahi kutokea duniani.. Vita usiyojua adui anatokea wap saa ngap yupo wapi ana nini.. Nia yake sio kushinda nia yake ni kuleta hofu.. Target yake sio jeshi yeye ana deal sana sana na raia wasio na hatia ambao ndani yake humo humo pia adui yumo. Unahitaji miaka kadhaa kusafisha nchi sio miez wala mwaka mmoja.
 
BINARY NO

JF-Expert Member
Dec 29, 2011
2,051
2,000
conspiracy theory at work...another false flag to justify foreign intervetion in Africa...BH ni kina nani? BH wanauwezo wa kijeshi na magari jeshi na operation zao wanazifanya mchana mbona hawakamatwi? kuna taifa moja kubwa limeiaminisha Nigeria kua BH wananguvu kuliko jeshi lenu na ikabid GOODLUCK JONATHAN akubar msaada wa kunyonywa mafuta...Ni kweli BH wanapower kuliko jesh? Na mbona hatuon jesh likiwa na dhamira ya kulinda nchi? aya majibu anayo VLAMIN PUTIN kwan anapinga new word order under the guise of fighting terrorism,human right, ICC,foreign aid,IMF,world bank etc...BH NI NANI?
 
Otorong'ong'o

JF-Expert Member
Aug 17, 2011
35,505

Kumbe tayari ni conspiracy theory...!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom