Brazil pia kuna Mlima Kilimanjaro!

Brazil pia kuna Mlima Kilimanjaro!

johnsonmgaya

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
2,818
Reaction score
3,731
Habarini wana jamvi, habarini za siku nyingi.

Jioni ya leo nilikuwa nafatilia vipindi kadhaa kwenye televisheni baada ya kurudi kazini mapema, hakuna mipira (hata mfuko pia hauko vizuri)

Station ya "Discovery family" (channel yangu pendwa baada ya super-sport) kuna kipindi kimoja kinaitwa "Xtreme water slides" huwa wanaonyesha water slides kubwa duniani na ambavyo watu huwa wanafurahi na kuogopa pindi wazitumiapo!

Ndipo nilipobahatika kuiona slide iitwayo "mount kilimanjaro water slide" kwanza nilishtuka nikajisemea ni kwamba sijasikia vizuri hilo jina au sijaelewa lugha hii pendwa ya malkia?

Nikajiongeza kugoogle endapo nilikuwa sahihi au lah, nikaikuta kweli ipo na inaitwa hivyo hivyo mount kilimanjaro,
tena ni slide namba 4 duniani kwa urefu!

Kwa elimu yangu ndogo kuhusu masuala ya kibiashara nafahamu ni kosa kisheria kutumia brand au jina la kampuni jingine kwenye biashara yako!

Je, wahusika wanalifahamu hili?
kama hawajui walifatilie
nawasilisha!

IMG_7703.JPG


Seeking the tallest water slides in the world? Here is our top 5...
 
Ikulu tu bongo ipo mtaa/driveway inaitwa Barack Obama Dr
 
Kwani we huoni tofauti ya majina?
Mt Kilimanjaro na Mto Kilimanjaro Water Slide?🤦🏻‍♂️🤦🏻‍♂️🤦🏻‍♂️
 
Kwani mkuu kutumia brand name kwa nchi tofauti sio swala ila swala lipo kwa nchi moja alaf watu tofauti ndio swala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom