Bravo wabunge wa CHADEMA on katiba! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bravo wabunge wa CHADEMA on katiba!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by W. J. Malecela, Nov 14, 2011.

 1. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #1
  Nov 14, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280
  Well, Mnyonge mnyongeni kwenye hili la kugomea Katiba ninawaunga mkono wabunge wa Chadema kwa 100%, I mean Serikali ya chama changu CCM tufike mahali tulijali taifa at large badala ya kujijali sana sisi, sio siri katiba tuliyonayo sasa iliundwa zamani sana kukidhi mahitaji ya chama kimoja, sasa wakati umefika wa kuibadilisha ili ikidhi mahitaji ya vyama vingi tulivyonavyo na hasa UWAJIBIKAJI WA VIONGOZI WA JUU NA CHINI WA TAIFA!

  - Binafsi nimekuwa nikiwakemea sana Chadema kwa makosa ya kina Mtei, huko mwanzoni ya kukubali kuanzishwa siasa ya vyama vingi under Katiba ya Chama kimoja, now ninashukuru kwamba this time wameliona hilo kwamba wananchi tumechoshwa na kuuuziana mbuzi kwenye gunia, CCM tuache uoga na kukubali kwamba kwenye hili la katiba ni lazima tubadilishe katiba au else, I mean sometimes enough inakuwa enough!


  - KWA HILI LA KATIBA BRAVO CHADEMA TUPO WOTE!

  William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharia!
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,530
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  Tanzania Mbeleee!! Mkuu wakipuuza watajifunza kitu this tyme.inashangaza sana watu kushindwa kusoma alama za nyakati! Ni hatari kuwa na viongozi wasioweza kupima joto halisi!
   
 3. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,980
  Likes Received: 6,624
  Trophy Points: 280
  Wewe unaweza leta mgogoro kwenye familia yako. Tuseme unapingana na mama yako? Umemsikia alivyosema?. Hongera kwa ujasili wa kuongea maneno haya. Kumbe huwa mnafanya makusudi.

  Basi kwa kuwa umeona kosa lilipo tusaidie kuwaelimisha wenzio ambao hawaja ujua ukweli. Mungu awafungue akili wote walio kwenye kundi lako ili wawe na mawazo haya uloyasema.hakika tutafika kwenye Tanzania tuitakayo
   
 4. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Tatizo langu ni pale ambapo watu kama wewe wanaona chama kinafanya upuuzi na kuendelea kulialia eti kwa sababu ni "CHAMA CHANGU"! Kwa nini mnakosa ujasiri wa kuachana nacho hata kama ikibidi mkae uraiani kama watu huru?

  Kwa nini hadi hapa hamuoni damage ambayo chama chenu kimeshatufanyia??
   
 5. W. J. Malecela

  W. J. Malecela Tanzanite Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 15, 2009
  Messages: 13,627
  Likes Received: 1,928
  Trophy Points: 280

  - Tatizo ni kwamba hakuna alternative, yaani chama kingine cha kukiamini!

  William @ NYC, USA: Le Mutuz Baharias!
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Bravo chadema! This time around, the issue was not only to see what CDM observed, but also what great people says on constitutions.
   
 7. A

  Ame JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kwavile anajua yeye na kizazi chake wanamaisha marefu Tanzania kuliko hao wazazi. Billy uwe unatusaidia informally huko nyumbani basi kabla hatujawatimua kwa aibu kupitia njia za Tunisia na Msri...Japo hiyo nayo yaweza tumiwa vibaya kama walivyomfanyia Gadafi..
   
 8. A

  Ame JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Kwanini usianzishe tutakachokiamini? Acha deko kuwa mwanaume kwani baba kama hajajenga nyumba na wewe lazima ulale barabarani kama baba?
   
 9. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,142
  Likes Received: 2,177
  Trophy Points: 280
  Subiri nape akuambie wewe si Raia
   
 10. F

  FJM JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  ha ha ha ha William bana. Well kipo, na kimetoka nje wakati mjadala unaanza, even better hakiongozwi kwa nidhamu ya woga. Nina hakina ndani ya kambi ya wabunge wa ccm wako wengi wasiokubaliana na haya tunayoona sasa lakini ni waoga mno!

  Ukiangalia nchi nyingi Afrika na sasa Middle East zimeingia kwenye machafuko kwa sababu watawala wamekuwa arrogant, hawataki kuwasilikiza wananchi. Muswada uliowasilishwa March ulikuwa kwa lugha ya Kiingereza na hivyo hata baadhi ya wabunge wasingeweza kujua nini hasa kimeandikwa let alone wananchi. Sijui inakuwaje wanausoma kwa mara ya pili kwa sababu wananachi wa Tanzania hawajawahi kupata muswada kwa lugha ya Kiswahili. Hata ule wa Kiingereza uliwasilishwa bungeni kwa hati ya dharura hivyo haukupitia kwa wananchi!
   
 11. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,255
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  tupo pamoja @New York
   
 12. p

  politiki JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  wakina mzee mtei kwa kweli hawaitaji kulaumumiwa bali wanastahili kupewa pongezi kwa kukubali kuingiza mikono yao
  kwenye moto mkali pamoja na kujua moto ni mkali. wamefanya kazi ngumu sana kukataa nchi kuendelea kuwa ya chama kimoja kwa kukubali kuingia ktk mfumo huku wakijua wazi kuwa mazingira ni magumu lakini walijua ni lazima watokee watu wakujitoa ili kuuelimisha umma kuhusu mfumo wa vyama vingi pamoja na ccm kupita nchi nzima na kuupaka matope. Toka vyama vingi vianze mwaka 1992 wapinzani walikuwa wanalilia katiba mpya lakini serikali ilikataa na kama unavyojua vilikuwepo vyama fake vingi kama TPP ambavyo serikali ingeweza kuvitumia kuendeleza mfumo wa vyama vingi kwahiyo mtei na wenzake walisacrifice vitu vingi sana mpaka leo tumefika hapa tulipo na siamini kama tungefika hapa tulipo bila wao kujitoa kwanza na wanastahili Pongezi na siyo lawama kazi kwetu vijana kuhuchukua mpira hapa ulipo mara baada ya kufikishwa na wazee kama akina mtei na kuupeleka mbele . umefika wakati kwa watanzania wote sasa kuvua kofia zetu za uccm, uchadema na ucuf na kuvaa kofia za utanzania kwa ajili ya maslahi ya nchi yetu
   
 13. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,150
  Likes Received: 3,337
  Trophy Points: 280
  Vizuri sana, Tupo Pamoja Mkuu.
   
 14. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  katika siku zote leo umeonyesha ukomavu wa kisiasa. Umeonyesha kuwa wewe ni mwanamume siyo mwanaume. hili ni taifa letu sote
   
 15. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,801
  Likes Received: 83,173
  Trophy Points: 280
  Hongera sana kwa kuuona ukweli kama ulivyo. Kama unahitaji kadi ya CDM basi hujachelewa, nibonyeze tu kwa pembeni nikushughulikie :). Kungekuwa na magamba ambao wanauona ukweli kama ulivyo na kutoogopa kuusema ukweli kama wewe basi labda gamba lingekuwa limeshavuka siku nyingi sana lakini kilichopo sasa ni usanii tu.
   
 16. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Tanzania kwanza. Nalog off
   
 17. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Kwani ni kazima kuwa na chama wakati wote??

  Kama hakuna chama mbadala mnasubiri nini kukianzisha???

  Naanza kumkubali Sitta na CCJ yake...angalau yeye alithubutu hata kama hakufanikiwa na hivyo kurudi nyuma badala ya kusonga mbele!!
   
 18. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  W @ NYC usiniambie na wewe una myopia juu ya vyama vya siasa. Hivi chama ni nini hasa? si ni watu, kama Ariel Sharon aliachana na Likud na kuanzisha Kadima na kushinda, Berlusconi alianzisha chama chake na baada ya mwaka akachukua nchi, sidhani kama watu makini ndani ya CCM hawawezi kufanya hivyo kama hawaoni chama mbadala. Tatizo lenu ndani ya CCM ni unafiki, watu hawakubaliani na CCM ila wamo tu ili mkono uende kinywani.
   
 19. Anheuser

  Anheuser JF-Expert Member

  #19
  Nov 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 1,962
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Usimlaumu Mzee Mtei. Nadhani zaidi tatizo sio kina kina mzee Mtei waliotunga mfumo uliopo bali kina mzee baba yako wakati wa utawala wao ulioisha unceremoniously.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,594
  Likes Received: 1,959
  Trophy Points: 280
  Kamanda kama unavyojuwa mimi sina chama,unafahamu hilo toka nimejiunga JF na wewe kunipokea hapa mimi na wengine wetu.

  Ninaheshimu maoni yako and you know it.

  Ningependa unieleze sababu ya kusema hakuna chama cha kukiamini.

  Ni kweli sina chama ila mwelekeo wangu umejikita zaidi kwenye ushabiki wa chadema,again you know it. because wanapinga mafisadi and that appealed to me.

  Kwasababu hii si thread ya kwanini chama flani si cha kukiamini,badala yake ni ya kukipongeza kwa kutoka bungeni,basi naomba walau kajisababu kamoja ama viwili tu vya kwanini chama cha chadema si cha kukiamini.

  Again,swali langi ni a honest one...
   
Loading...