"Boys 2 Men", kwanini msiiache Tanzania ipumue?

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Habari Wana JF,
Naomba kuuliza swali,
Je, "Boys 2 Men" ndio wazalendo wakubwa wa nchi hii?

Je, ni kwamba "Boys 2 Men" wanaipenda sana Tanzania?

Najenga hoja. Mnaoipenda nchi hii. Tuache u_CCM , u_CHADEMA. Tuulizane.
Je, "Boys 2 Men" ndio mwarobaini wa matatizo ya nchi hii?!

Je, Kuna uhusiano gani kati "Boys 2 Men", na "CCM INA WENYEWE"?

Naomba tuongee kama Taifa la watanzania. Je, nchi hii inamilikiwa?

Tafadhali sana, tuweke makundi ya kisiasa pembeni.

Binafsi nilimponda sana JK, nikamponda sana JPM, na Sasa najiuliza nianze kumponda na Samia? Au kuna tatizo sehemu Mimi sijajua? Nitaponda wangapi?

Nchi hii ni maskini sana. Je, "Boys 2 Men" ndio watakaoipeleka mbele nchi yetu?

Naomba kuwasilisha.

Karibuni tujadili Tanzania yetu ipone na kupaa kimaendeleo.
 
Dawa ni kuipiga chini CCM, miaka zaidi ya 60 kila siku ni porojo tu! Tuwape wengine nao wakizingua wapigwe chini! Ccm wamejipa hatikiliki ya nchi hii kwa hiyo wanafanya watakavyo! Ndio mana wanafunga watu kwa ajili ya kutetea katiba mpya!
 
Mimi nikisema huwa nachukiwa na kuonekana mwendawazimu, lakini niwaambieni ndugu zangu: Hawa wazee wa Cold-War na Ujamaa ni watu hatari mno kwa mustabali na ustawi wa taifa letu. Hiki kizazi kimerivuruga sana hili taifa na kitaendelea kufanya wanachokitaka mpaka tutapoamua kuwatoa kinguvu. Bila hivyo tutapiga mbizi kwenye lami....
 
Mkuu hayo ni majoka ,,,yaliona ili yaibe yaanze na Mzee WA lupaso .Sasa hivi yanajitawala na yanakula yatakavyoo ..ni MDA WA kusali kila mmoja Kwa Imani yake ili siku Moja yafie kwenye kichuguu Kwa pamoja ( MTU Kama vice president & prime minister ni WA kukaaa kimya Kama vile hawapo.hii inatoka kuwa wameona mijoka mikubwa kwenye kichuguu ukileta za kuleta unaliwa kichwa
 
Genge la mafisadi likiongozwa na Kiranja wao mkuu JK ni tishio kwa ustawi wa hii nchi.

Mtandao wao umeshikamana kutoka ndani mpaka kwa waume zao mabeberu.

As a country, we need strong measures to keep these monsters at bay.

Nani anajua kwa hakika hawa ni watu wa aina gani na chimbuko lao ni lipi!!!
 
Mkuu sijui tunafanyaje waingie watu wapya wenye fikra mpya, na wawe huru bila mizizi ya nyuma huko!
 
Genge la mafisadi likiongozwa na Kiranja wao mkuu JK ni tishio kwa ustawi wa hii nchi.

Mtandao wao umeshikamana kutoka ndani mpaka kwa waume zao mabeberu.

As a country, we need strong measures to keep these monsters at bay.

Nani anajua kwa hakika hawa ni watu wa aina gani na chimbuko lao ni lipi!!!
Sasa kama haya majitu ndio yamejichimbia hivi! Tunafanyaje? Nchi inageuzwa kama chapati!!? Kweli?
 
Mkuu hayo ni majoka ,,,yaliona ili yaibe yaanze na Mzee WA lupaso .Sasa hivi yanajitawala na yanakula yatakavyoo ..ni MDA WA kusali kila mmoja Kwa Imani yake ili siku Moja yafie kwenye kichuguu Kwa pamoja ( MTU Kama vice president & prime minister ni WA kukaaa kimya Kama vile hawapo.hii inatoka kuwa wameona mijoka mikubwa kwenye kichuguu ukileta za kuleta unaliwa kichwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Siasa za CCM zenyewe zimekuwa kama vita!!

CCM INA WENYEWE eti! Dah, pole Dr. Mpango
 
Back
Top Bottom