"Boys 2 Men", kwanini msiiache Tanzania ipumue?

Mkuu sijui tunafanyaje waingie watu wapya wenye fikra mpya, na wawe huru bila mizizi ya nyuma huko!
Mkuu matatizo ya Tanzania hayakuanza na Raisi Jakaya wala Raisi Magufuli, yana mzizi mrefu sana. Pia hatuwezi kudharau kabisa mchango wa hawa wazee wala ushauri wao, japo mimi naamini kwamba wao wananufaika na huu mfumo hivyo ni nadra kwa wao kufanya maamuzi magumu yenye maslahi kitaifa. Wengi wao ni wahafidhina huku wengine wakiwa ni walafi mno. Sasa hilo la tutapataje fikra mpya ni jingine ambalo ukilizungumzia hadharani huwezi kukosa kuitwa mhaini, mchochezi au gaidi.......
 
N
Genge la mafisadi likiongozwa na Kiranja wao mkuu JK ni tishio kwa ustawi wa hii nchi.

Mtandao wao umeshikamana kutoka ndani mpaka kwa waume zao mabeberu.

As a country, we need strong measures to keep these monsters at bay.

Nani anajua kwa hakika hawa ni watu wa aina gani na chimbuko lao ni lipi!!!
Kijana utakufa na presha
 
Mkuu matatizo ya Tanzania hayakuanza na Raisi Jakaya wala Raisi Magufuli, yana mzizi mrefu sana. Pia hatuwezi kudharau kabisa mchango wa hawa wazee wala ushauri wao, japo mimi naamini kwamba wao wananufaika na huu mfumo hivyo ni nadra kwa wao kufanya maamuzi magumu yenye yenye maslahi kitaifa. Wengi wao ni wahafidhina huku wengine wakiwa ni walafi mno. Sasa hilo la tutapataje fikra mpya ni jingine ambalo ukilizungumzia hadharani huwezi kukosa kuitwa mhaini, mchochezi au gaidi.......
Umemaliza mkuu

Sent from my SM-N920C using JamiiForums mobile app
 
Tanzania itakuwa huru hadi pale kizazi cha tanu kifutike chote kipindi ambacho generation Z ndio watakuwa senior citizens
Tunataka katiba ibadilishwe kabla hatujabadili chama tawala maana bila hivyo watapoingia na wao wataweka ngumu ya kutoka huku wakitugalagaza zaidi ya CCM. Mfano halisi ni mwenyekiti wao ambaye hataki kung’atuka kwenye nafasi hio miaka nenda rudi.

I would suggest under new constitution:
-Raisi asiwe mwenyekiti wa chama kuepusha kujikita na interest za chama kuliko taifa na kuvua watu uanachama kwa kukomoa.

-Budget ya bunge isitegemee serikali.

-baraza la mawaziri litoke kwa wananchi.

-wabunge kwa wananchi.

-Tume ya uchaguzi isiwe appointed na rais.

-Watoto wa wastaafu wawe banned kushika nafasi influential za serikalini kama urais, uwaziri atleast waishie kwenye ubalozi labda na hii si kwa ubaya bali kwa manufaa ya umma. Kwa kampuni binafsi wako free kuwa hata wakurugenzi.

-Ajira za serikalini ziwe za mkataba wa 3-5 years huku maslahi yakiboreshwa ili watu wakipata uzoefu warudi kujiajiri. Mikataba iwe extended kulingana na utendaji kama mtu ana perform aongezewe muda.

-Raisi aweze kufunguliwa mashtaka na wananchi direct bila approval ya DPP.
 
Dawa ni kuipiga chini CCM, miaka zaidi ya 60 kila siku ni porojo tu! Tuwape wengine nao wakizingua wapigwe chini! Ccm wamejipa hatikiliki ya nchi hii kwa hiyo wanafanya watakavyo! Ndio mana wanafunga watu kwa ajili ya kutetea katiba mpya!
Mliletewa katiba bungeni mkawa mnatoka nje
 
Back
Top Bottom