Boxing ni mchezo wa hatari, huku watu hawafagilii ujinga kama kwenye michezo mingine

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,464
21,195
Kuna hii tabia iliyopo kwenye boxing, huku kwenye boxing watu watakushabikia ukiwa unashinda tu, ukipigwa imekula kwako.

Kwenye boxing shinda hata mapambano 100, ila kaa ukijua siku ukijichanganya ukapigwa basi tegemea kupoteza mashabiki zako zaidi ya 85%. Ukipigwa tena pambano linalofuata basi tarajia kusahaulika kabisa kwenye ulimwengu wa boxing na hata mashabiki zako waliokuwa wanakuimbia nyimbo za mapambio tarajia hao hao kukuzomea.

Tuangalie mfano pambano lililochezwa hapo jana kati ya Terence Crawford na Big Fish (Errol Spence), Crawford kupitia pambano lake na Spence amefanikiwa kuvuna mashabiki lukuki huku Spence akikimbiwa na mashabiki wake na kuzomewa juu. Amezomewa kana kwamba hawakuwa naye kipindi chake cha furaha 😂.

Hii pia ingekuwa vice versa kama Crawford naye angepigwa, basi bila shaka naye tungetarajia kukimbiwa na hao wanaojiita big fans wake.

Mbali na huyo, mfano mwingine tumuangalie AJ. Huyu naye baada ya kupigwa na Andy Luiz (Destroyer) mashabiki wakamkimbia, baada ya kupigwa tena na Usyk watu wameshamsahau kama kuna mtu anaitwa AJ 😂.

Mfano mwingine ni Saul Alvarez (Canelo), huyu jamaa naye baada ya kupigwa na Bivol sifa zote alizokuwa nazo zote zimewekwa kapuni, yaani umaarufu wake wote umeporomoka.

Nakumbuka miaka ya nyuma kidogo nilimsindikiza rafiki yangu (sitamtaja kwa jina) kwenye pambano lake, alikuwa anapigana na mtu ambae wakati huo alikuwa tishio sana na ana mashabiki wengi sana, wakati huo mshikaji wangu yeye mapambano yake hayazidi matatu kwenye pro hivyo alikuwa hajulikani na wengi.

Kipindi pambano linaanza jamaa yangu alikuwa anazomewa sana na mashabiki, piga hilo Novice, piga hilo Novice 😂. Sasa kadri muda unavyoenda yule jamaa mkongwe tukawa tunamzidi, mashabiki zake wote wakahamia kwetu wakaanza tena "piga hilo lizeee, piga hilo lizeee"😂.

Kwa kifupi hii ndio boxing, tupo na wewe ukishinda tu, ukishindwa jua utabaki peke yako.😂
 
Back
Top Bottom