BOT toka Slaa 'aweke mpira kwapani' na kuurusha 'uwanja wa wazi'

John Mnyika

JF-Expert Member
Jun 16, 2006
712
1,240
MATUKIO MBALIMBALI KUHUSU TAARIFA ZA BoT

Desemba 20: Inaripotiwa kuwa Gavana Balali ameandika barua ya kujiuzulu akiwa nje ya nchi, Ikulu na Wizara ya Fedha zinasema kuwa hazina taarifa.

Desemba 19: Meghji anatetea kuchelewa kwa ripoti ya BOT.

Desemba 01: Dk Wilbrod Slaa anaelezea kukerwa na usiri wa Ripoti ya ukaguzi wa hesabu za BoT.

Novemba 29: ukaguzi wa hesabu za BoT unakamilika na inaelezwa ripoti hiyo kufika kwa mkaguzi mkuu wa mahesabu ya serikali.

Septemba 22: wafadhili wanadai ufafanuzi wa tuhuma za ufisadi zinazoihusu BoT.

Septemba 20: Hali ya Gavana Balali inaripotiwa kuendelea vizuri.

Septemba 16: Wananchi wataka msimamo wa tuhuma za BoT na nyinginezo kutoka kwa Rais Kikwete.

Sept 15: Dk Slaa wanahutubia mkutano wa hadhara Mwembe Yanga Temeke, kisha anataja orodha ya waliowaita mafisani wanaotafuna nchi, akimjumuisha na Balali.

Septemba 14: Afya ya Gavana Balali inagubikwa na utata, lakini inaelezwa kuwa yuko nje nchi kwa matibabu.

Septemba 11: Kampuni ya Ernst&Young iliyoteuliwa kupitia hesabu za BOT katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ili kubaini ukweli kuhusu ubadhirifu wa fedha, inaanza kazi.

Septemba 09: Inaripotiwa kuwa hali ya Gavana si nzuri, hivyo amepelekwa nje ya nchi kwa uchunguzi na matibabu.

Agosti 19: CHADEMA inajibu mapigo ya Spika dhidi ya Slaa na hoja ya BoT.

Agosti 18: Spika anamtuhumu Dk Slaa kuwa ameghushi nyaraka alizotaka kuzitumia dhidi ya BoT na kutishia kumshitaki.

Agosti 16: Slaa anachomoa hoja binafsi ya BoT Bungeni akidai kuwa inaonekana hakuna nia njema, hasa baada ya mbunge mwenzake Zitto Kabwe kusimamishwa baada ya kuwasilisha hoja yake iliyokataliwa na wabunge wa CCM. Anaahidi kuipeleka kwa wananchi na kwa wafadhili, lakini pia anadai kutishiwa maisha.

Agosti 12: Muda wa Balali kustaafu uliainishwa kupitia vyombo vya habari, muda huo uliainishwa kuwa ni Juni mwaka 2008.

Julai 13: Gavana Balali anakataa hoja iliyoelekezwa kwake na wapinzani waliomtaka kujiuzulu kwa manufaa ya umma. Yeye anasema hajiuzulu kamwe.

Julai 12: Balali anapunguziwa mzigo na alipewa manaibu watatu kumsaidia.

29 Juni: Serikali kupitia kwa Waziri wake wa Madini na Nishati inamsafisha mke wa Gavana Daudi Balali aitwaye Ana Muganda kuhusu tuhuma ya yeye kutumia nafasi ya mumewe na kisha kuwa mkurugenzi katika moja ya makampuni ya madini ya dhahabu hapa nchini.

27 Juni: IMF inatoa taarifa kupitia kwa Naibu Mkurugenzi wake Murilo Portugal akitaka uwazi uwepo katika suala la kuichunguza BoT.

Juni 26: Mjadala unatanuka kuhusu tuhuma za ufujaji fedha BoT na safari hii mbunge wa CCM Ole Sendeka anataka iundwe tume ya kuichunguza BoT.

Juni 25: Mbunge wa Karatu Dk Wilbrod Slaa anatoa dai Bungeni akitaka Gavana wa Benki Kuu David Balali ajiuzulu.

Juni 15 Bunge la Bajeti linakaa na Bajeti ya mwaka 2007/08 inasomwa na Waziri wa Fedha Zakhia Meghji

Chanzo: http://www.mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=3542
JJ
 
Tunakumbuka nyakati nzuri kipindi kile vijana walipenda siasa na walipenda kujenga hoja .

Saizi vijana wamekuwa kama wagonjwa...
 
Siku hizo katika utawala wa Ben mawaziri wote walikuwa majizi, na hata makatibu akuu walikuwa majambazi, ukija kwa maded walikuwa viwavi jeshi. Ubunge wa kuteuliwa ulikuwa wa vitanda maalum
 
Uzi una miaka kenda aisee
Hapo ndiyo ufahamu kuwa ufisadi nchi hii haukuanza leo na hauwezi kwisha endapo CCM ikiendelea kutawala.Hiyo ripoti hadi le haikuwahi kuwekwa hadharani na kufanyiwa kazi kama ilivyostahili.
Maigizo yanayoendelea sasa ni zaidi ya hayo na sauti ya Wananchi inazidi kubinywa ili wasisikike.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom