BOT na pesa mpya vipi?

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,219
370
Wana JF,

Naja tena na muswaada huuu wa Pesa Mpya ambazo BOT walizi pigia debe sana kuwa ni za ubora na kiwango cha hali ya juuu saana na sio rahisi kughushi hizo pesa mpya.

Mbali na hilo BOT walitangazia Bank zote za hapa nchi kuwa wahakikishe wame badirisha Cassette za ATM (zamani) na waweke mpya hizo Cassette za ATM ile ziweze ku load pesa mpya na zoezi hili lilifanyika vyema ila cha ajabu nashindwa elewa kila nikienda kwa ATM kutoa pesa still pesa zatoka mchanganyiko mara za zamani na mpya.

Nika pata muda ni kaweza mhoji mfanya kazi wa Bank Mmoja vipii kulikoni mbona siku hizi ninaona pesa za zamani ndizo zatumika sana kuliko mpya ??? akanidokeza akasema bwana eeeeh hawa BOT walichemka sana hizo pesa mpya zina matatizo kumbe ni zachakaaa haraka sana kuliko pesa za zamani, Khhhhaaaa nika staahajabika sana sasa Pro: Benno Ndullu alikuwa anajigamba nini ???? sasa huyu bwana akaniambia hapo BOT inaingia gharama nyingine tena kuzirekebisha hizo pesa which means ni kuzichapa tena upya na hili BOT wamekaaa kimya kumbe wanalifanya kwa siri.

Nchii hiii jamani dhuuuuuu!!!!!

Karibuni kuchangia Hoja
 
Ulikuwa ni mradi wa mtu kama hizi mashine za tra ni miradi ya ulaji wa kimjinimjini hii nji inatia kinyaa
 
Kuna makosa kidogo ya kiufundi yalifanyika kwa mfano yule mjusi kwenye noti kuonekana kwa uwazi sana. Lakini marekebisho yanafanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza ukubwa, uzito, harufu etc. Habari nyingine ni za kiintelejesia zaidi kwahiyo siwezi kuziweka hapa.
 
kwa hiyo unadhani zitakuwa bora zaidi kuliko zile za mwanzo au hayo ni mawazo yakisiasa zaidi..
 
Hela mpya hazikidhi ubora, zina ghushiwa kirahisi na zina ubora hafifu.
Pesa za zamani ni bora kuliko mpya
Unajua ukitaka kula pesa pesa ya serikali ni lazima uanzishe ka-activity fulani ka ku-justfy malipo. Wengine wanaanzisha visemina kwa mamilioni ya pesa na wengine wanaanzisha zoezi la kutengeneza pesa mpya japo hazihitajiki ki vile ilimradi tuu mchakato huo utapelekea malipo fulani. Ndiyo maana unaambiwa uongozi serikalini ni mtamu ndugu yangu
 
Kuna makosa kidogo ya kiufundi yalifanyika kwa mfano yule mjusi kwenye noti kuonekana kwa uwazi sana. Lakini marekebisho yanafanyika ikiwa ni pamoja na kuongeza ukubwa, uzito, harufu etc. Habari nyingine ni za kiintelejesia zaidi kwahiyo siwezi kuziweka hapa.

Hapo hamuoni kuwa ni kufuja pesa za UMMA wakuuu, Mwanzoni watu wali hoji kwanini mwatengeneza pesa Ndullu akajitetea kuwa kila miaka 7 twatakiwa badirisha na wadau wakamwambi mbona noti hizi ni nyepesi na akazi sifia zaidi na kuzitete huku wananchi walisha anza kuzi lalamikia sasa leo hiii warudi kiwandani tena kwa gharama za nani hizo pesa kulifanyika upoembuzi makinifu mwanzo kabla ya pesa mpya kutengenezwa au kulikuwa ni kujitafutia umaarufu au kujitafutia ulajia.

My Take:

Serikali ni inafanya uzembe mkubwa na hapo ndipo inapo kosa imani kwa watanzania na kuhisi serikali inafanya magumashi mengi sana, serikali iache kukurupuka kwa kila jambo inafanya mambo mengi kwa wakati mmoja haina mfumo wa kimstari kuanzia moja hadi mwisho.

BOT wakitengeza pesa huwa wanatuambia pesa inashuka thamni au inapanda thamani?? au huwa wanapotezea wananchi wanabaki kama mazuzu vili??

Isije mlilipa kiwango tofauti na mlicho ambiwa na matokeo yake yakawa haya ya noti zilizo na kasoro kibao na pesa zingine mkazikimbizia kwenye kampeni maaana muda huu kuiamini serikali yetu ni 20% kabisa hakuna mtu anae iamini serikali kwa 90% kwa hivi sasa na mambo inavyo yapeleka na mtu anae iamini serikali iliyopo madarakani kwa sasa atakua ana matatizo ya ubongo esp kwenye kufikilia
 
Unajua ukitaka kula pesa pesa ya serikali ni lazima uanzishe ka-activity fulani ka ku-justfy malipo. Wengine wanaanzisha visemina kwa mamilioni ya pesa na wengine wanaanzisha zoezi la kutengeneza pesa mpya japo hazihitajiki ki vile ilimradi tuu mchakato huo utapelekea malipo fulani. Ndiyo maana unaambiwa uongozi serikalini ni mtamu ndugu yangu

Teh teh teh amakweli wajinga ndio tuliwao, kwahiyo mkuu nkianzisha ka mradi tu nakimbia zangu hapo BOT/au kwingineko tu na v-evidence fulani fulani tu hapo na mkono wa mtu mkuu na vinapitishwa faster naenda kuwa pumbaza watu huko kwetu interior au matongo ghete ghete!!!!
 
huu ulikuwa ni mradi wa watu fulani katika kuidhinisha ulafi wao
 
Ni heri wabadilishe noti ya sh elfu kumi iwe ktk mfumo wa sarafu na sarafu ya sh 200 iwe ndo noti vivyo hivyo kwa noti ya sh elfu tano na elfu mbili natumai hapo uchakachuaji utakwisha.Kwa sababu haitakuwa rahisi kugushi sarafu ya sh elfu kumi na pia mtu hawezi kujiangaisha kwa ajili ya kugushi noti ya sh mia mbili. Ni mtazamo wangu.
 
Duh!! Sasa KIBURUDISHO hapa utakuwa umetumia masaburi kutoa hili wazo!!
 
Nguvu waliyoitumia kuzisifu hizp noti ilinifanya niamini kuwa noti hizo zina kiwango cha chini sana, huku mtaani ndivyo tulivyokuwa tunaziona lakini wao waliendelea kusisitiza kuwa ni noti nzuri, ile ya jero ukiishika mkononi dakika 30 inapauka, BOT ni wezi wakubwa wa mali ya umma
 
Hawa viongoz ni wapuuz sana. Lkn watakuwa wamesaidia nchi kuingia kwenye historia ya kutumia currency mbili tofauti at once.
 
Katika hz pesa mpya inayotia fora kwa kuwa ovyo kabisa ni sh mia tano.sijui walitengenezea material gan sijui toilet paper au nin,iko full ya kichinachina,inachakaa mapema kupita maelezo,ile ribon yake ya pembeni inanyofoka yenyewe na kutoka wth 2wks.hii ni hatari
 
Hawa viongoz ni wapuuz sana. Lkn watakuwa wamesaidia nchi kuingia kwenye historia ya kutumia currency mbili tofauti at once.
<br />
<br />
mkuu hapo kuna pengo la hela zilizotumika kiholela limejaziwa,umesahau enzi za mwinyi? Au kama ilivyokuwa zimbabwe?mambo ya uchaguz hayo,funguka ufahamu wako.
 
Kiukweli noti mpya ni balaa tupu. Hata kaisari hawezi zipokea

Mara nyingi tumekuwa wagumu kuelewa somo. Umeambiwa pesa hizi zina ubora zaidi na zina security features ambazo haziwezi kughushiwa kiurahisi lakini hatuelewi. Au mtu akivaa sarawili ya kitambaa kizito ndo anakuwa amevaa nguo yenye ubora. Hizi hela niza kisasa zaidi isipokuwa matumizi yetu ndo mabaya. Mfano; mnaenda kanisani kutoa sadaka mmekunja noti, mnaficha noti sehemu za siri zinapata ukungu, wengine wanachimbia pesa chini ya shimo, wengine wanazikunja kwenye pembe za kanga, hatutumii wallet, mikono yetu inakuwa na unyevu wa maji na jasho lakini tunashika pesa. Hayo ni baadhi tu ya matumizi mabaya ya pesa zetu. Ukiangalia American Dollar---huwezi kuikunja kwa sababu unajua inaweza kukataliwa either na benki au ikagoma kupita kwenye mashine ndo maana mnazitunza vizuri.
Mie nakubaliana na Ndullu kabisa kuwa hizo noti ni bora kabisa kuliko zote zilizowahi kutoka hapa TZ.
 
Ndullu was the wrong appointment as BOT Governor!! Alisema it was wrong kuweka reserve zetu kwenye dhahabu na sasa dhahabu ndio inapaa kwa thamani kuliko hivyo vidola vyao!! He is a world bank product what do you expect? Kama mnasema watu hawajui jinsi ya kuzitumia kwani zile za zamani walizitumia kitofauti; kama kuzichimbia na kuzificha sehemu za siri zilifichwa lakini ubora wake haukuathirika.
 
jamani hii hali inasikitisha sana. sijui nchi itapoteza fedha kiasi gani kwa mchezo wa BoT, maana itakuwa kila baada ya muda mfupi wanatengeneza fedha mpya kureplace zilizochakaa. BoT lazima wakiri ukweli na wachukua hatua, maana hata mtu ambaye hana utaalamu kihivyo anajua jambo hili!
 
Mara nyingi tumekuwa wagumu kuelewa somo. Umeambiwa pesa hizi zina ubora zaidi na zina security features ambazo haziwezi kughushiwa kiurahisi lakini hatuelewi. Au mtu akivaa sarawili ya kitambaa kizito ndo anakuwa amevaa nguo yenye ubora. Hizi hela niza kisasa zaidi isipokuwa matumizi yetu ndo mabaya. Mfano; mnaenda kanisani kutoa sadaka mmekunja noti, mnaficha noti sehemu za siri zinapata ukungu, wengine wanachimbia pesa chini ya shimo, wengine wanazikunja kwenye pembe za kanga, hatutumii wallet, mikono yetu inakuwa na unyevu wa maji na jasho lakini tunashika pesa. Hayo ni baadhi tu ya matumizi mabaya ya pesa zetu. Ukiangalia American Dollar---huwezi kuikunja kwa sababu unajua inaweza kukataliwa either na benki au ikagoma kupita kwenye mashine ndo maana mnazitunza vizuri.
Mie nakubaliana na Ndullu kabisa kuwa hizo noti ni bora kabisa kuliko zote zilizowahi kutoka hapa TZ.

Kweli nimeamini kuna watu wanawaza kwa "Masaburi"!!
 
Back
Top Bottom