BOT achaneni na noti ya 10,000/-

Hapana Mkuu mbona USD zinaishia 100.Cha msingi lazima uchumi wetu uwe Imara huwezi kufanya hicho anachotaka mleta Uzi kwa uchumi wetu huu.
Zinaishia 100 kwa sababu zina thamani.Zetu hazina thamani.Hata euro ipo hadi 500 lakini kuwezi kuitumia kwenye manunuzi, hata kwenye ATM mwisho kutoka ni 50 euro.Ila ukiitaka noti ya 500 inabidi uende bank uombe wakupe bills za 500.
 
tatizo si uwepo wa elfu 10, tatizo ni uwepo wa mia , mia mbili na mia tano nyingi sana katika mzunguko wa fedha kuliko mzunguko wa elfu 1, 2 na 5 na hivyo kufanya upatikanaji wa 10 kuwa mdogo sana na hata upatikanaji wa cheji kuwa wa shida kwa elfu 10 kwa sababu pesa za kuicheji elfu 10 zinakuwa zina mzunguko mdogo.

suluhisho
1. serikali ingeanza utaratibu wa kupunguza mia 1, 2 na 5 kwenye mzunguko ili zibaki hizo nyingine ndo ziwe nyingi.

2. bidhaa zingeanza kuuzwa kuanzia mia 5, kwa maana ya kwamba uwepo wa bidhaa za mia moja zinafanya mzunguko wa mia tano tu wenyewe kuwa wa shida sembuse 10000

3. watu wanatakiwa kufundishwa kuijua thamani ya elfu 10 kuliko thamani ya mia moja, hii itasaidia watu kuachana na mia na kutafuta na kutumia elfu 10
 
Duhh!! Wewe ndiyo zero mwingine!! Kwa hiyo bidhaa ama huduma za mia mia zifutwe zibaki za 1000 hadi 10,000 tu?au nauli zetu hizi za 400 tuzipandishe hadi 2000 ili kubana mzunguko wa mia mia?
 
Huku mtaani hakuna kitu kinasumbua kama chenji.
Watu hawauzi kisa kakosa chenji au auzunguke wee.
5000 na 10000 ni shida,

Mbadala wa efu kumi mprinti 2000 na noti mpya ya 3000 ziwe nyingi za kutosha bila kusahau 500 na 1000.
Chenji ni tatizoo.

Uko mitaa ipi mkuu, maana huku tulipo Msimbazi kama kawaida na chenji unapata
 
Chenji zipo Benki mkuu,wala hakuna hilo tatizo
 
Hapana Mkuu mbona USD zinaishia 100.Cha msingi lazima uchumi wetu uwe Imara huwezi kufanya hicho anachotaka mleta Uzi kwa uchumi wetu huu.
hivi noti za marekani,ZINAANZIA dola ngapi nakuishia ngap?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…