Boss wa Wrong Parking ashindwa kuongea Kiingereza

Boss wa Wrong Parking ashindwa kuongea Kiingereza

chingas

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2014
Posts
261
Reaction score
113
Mzungu akamatwa na watu wa wrong parking, akataa kulipa faini akidai aonyeshwe alama inayomzuia yeye asipaki gari mahali hapo, watu wa wrong parking washindwa kuongea english na kumpigia bosi wao ambae nae ni mbulula pia, Raia waingilia kati wakitaka mzungu huyu aachiwe kwa vile ni mgeni hajui utaratibu wa kupaki gari awapo mjini, vile vile mjerumani huyu akadai mara nyingi dereva huongozwa na alama za barabarani lakini pale hakuna alama iliyomzuia, bosi aamuru kwa simu mzungu aachiwe.

Je wewe mwenzangu umejifunza nini hapa?

Kwa upande wangu nimeona kama vile kuna uonevu mkubwa sana kwa hawa jamaa wakiwalipisha watu sh 50,000 kwa makosa ambayo hata serekali haiwezi kukuadhibu hivyo, alafu kwa nini wanawaadhibu watu kwa makosa ambayo si ya makusudi, nasema si makusudi kwa vile sehemu nyingi wanazoadhibiwa watu hazina alama so mtu anapaki bila kujua kama kapaki vibaya kwa vile kosa la makusudi ni lile ambalo mtu anakiuka kwa makusudi angali anajua anachofanya ni kosa.

Ushauri: Wrong parking Arusha wekeni kwanza alama kwanye sehemu zote zisizoruhusiwa kupaki magari, la sivyo tutaanzisha kampeni ya kuwapinga kwa nguvu ya umma.
 
ni sawa na wewe unavyolipa sevisi chaji tanesco wakati hata hawakujui
_au vile unalipa kodi tra alafu huduma za afya hakuna
 
Kalasinga mmoja alinifurahisha sana moshi alifungwa pale mbele ya NBC roundabout aliwaomba nimeshuka na hela nyingi nipaki mbali ili niporwe wakadinda wanataka fiu,akapiga simu garage likaja gari na cilinder za gas akakata chuma vipande,tulishangilia utadhani giroud kafunga
 
yea,mzungu yupo sahihi,huwezi kulipa fine kwa kupaki sehemu ambapo haina alama wala maandishi yanayokataza kupaki ni umbulula wetu tu kukubali hizo fine
 
Uwa nashangaa watu wengi kulalamika kuonewa na vijimtu wa wachache,na muonewe mpaka akili yenu itakapofunguka na kukaa sawa
 
kwa upande mungine nimegundua kuwa, bado mzungu ataendelea kuwa special kwa wabongo kwa sababu mbona tumeona wabongo wengi wakikamatwa na hawa mambulula lkn atuwapi sapoti ya kuwatetea
lkn ikitokea kwa mzungu watu hujitoa sana tu na kuwatetea
kwa iyo ile kasumba ya kutokusaidiana wenyewe kwa wenyewe bado ipo, lkn kwa ngozi nyeupe ni yes tu
kwa nini tusionyeshe ushirikiano ule alioupata mzungu kwa watu wote? au teseme ni kweli mzungu ni mtu special kwetu?
 
Maegesho ya magari yana tabu sana. Ni kweli sehemu zingine hakuna alama yoyote inayokuzuia wewe kuegesha gari lako, ila ukiegesha tu utawaona hawa hapa. Tena kuna watu wamekaa maalum kwa ajili ya kuwapigia simu hawa watu waje kukukamata.
 
Back
Top Bottom