Boss wa UBA Bank akamatwa na police

Wasiwasi mkubwa juu ya mwenendo wa hiyo kesi, nawahakikishieni huyo jamaa hatafungwa na atakimbia nchi, tusubiri tutasikia tu.
 
Japo sishabikii tabia ya unyanyasaji, lakini mtu kukutwa na dawa za kulevya imekuwa 'fashion' DSM kuna boss Moevenpick alikutwa nazo, kuna rafiki yangu pia alikutwa nazo baada ya kuachisha kazi wafanyakazi 2 kisheria

Kuna boss mwingine wa multinational naye aliwekewa madawa ya kulevya madawa yote wanayokutwa nayo thamani haizidi laki moja

Swali ni kama kweli wanatumia au ni mchezo mchafu ? Kama ni mchezo mchafu , Mungu aturehemu na roho hizi za visasi
 
Kati ya vitu alivyokutwa navyo O'bay kwenye appartment yake ni dawa za kulevya swali hatujui kama ni za kuuza au ni pamoja na kutumia. Tusubiri report ya police leo jioni.

Nijuavyo mimi mtu akidakwa na madawa haya hapewi dhamana moja kwa moja mahabusu kama amepewa dhamana basi imesha kula kwenu amesha wazidi kete mtasikia hana hatia hayo mapolisi tayari yamekamata kitu kidogo.
 
Kwnn apelekwe Kilwa road police post wakati anakaa Oysterbay?
Alafu unaongelea unyanyasaji bila kueleza kwa undani ni wa namna gani.
Watanzania ni wavivu na akitokea mtu akawabana kidogo basi tunapiga kelele za kunyanyaswa.
Kilwa Road ndio wana deal na mihadarati
 
Dhamana? Media coverage? Madawa ya kulevya? Mtuhumiwa yuko mtaani na si raia wa TZ? subirini sinema ya bure hapa hapa JF live!
 
Tazania ndio nchi peke yake Diniani kwa kuwapa wageni wahalifu dhamana kuliko wenye nchi yao, Masharti ya Mgeni kupata Bail ni rahisi kuliko Mzawa, Aibu hii nchi
 
Police wetu saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaafi kwa ushirikiano,manake mtu kwao jamani.Ukidharauliwa kwenu nani atakuhifadhi.
 
Why General Mbona kwenye hili ? Na ni kweli kwamba ni madawa ya kulevya hayo na baadaye dhamani anapewa haraka namna hii ?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
I can smell a business opportunity hapa.........

Ya kuwawekea Tags za GPS watu ambao ni watuhumiwa na ambao pamoja na dhamana wanaonekana wanaweza kutoroka. Kwa kuwa dhamana ni haki inabidi serekiali iangalie uwezekano wa kuinga gharama za GPS tags watuhumiw hatari wtaakuwa wanavaa wakiwa nje kwa dhamana

Cartrack wako katika nafasi nzuri zaidi kuuza huduma hii ya human track kwa serikali specifically vyombo vya usalama.

changamoto ni investment hii itawasaidiaje watanzania kitenolojia zaidi ya kuwaongezea mzigo wa uedeshaji.......
 
Kuna connections gani kati yake na mboma na madawa ya kulevya na bailout!
 
Ndipo tutakapoambiwa na mkulu kwamba wasambazaji na watumiaji wa dawa za kulevya tunawajua,tunaomba wajirekebishe!
 
Yaani dhamani za sikuhizi hasa kwa wawekezaji hazieleweki..kama kweli wanakingiwa kifua hata ha Gen Mboma basi hapo watachakachua tu...nashindwa kuelewa kwa nini watanzania wanawakumbatia mafisadi na wanyanyasaji wa wananchi wetu?tena kama hao wanajeshi wanakubalije kutumiwa??kweli nchi haina mwenyewe na uzalendo umeisha miongoni mwetu!!
 
Police wetu saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaafi kwa ushirikiano,manake mtu kwao jamani.Ukidharauliwa kwenu nani atakuhifadhi.

Serikali yenu inawalaza mapolisi na familia zao kwenye nyumba za mabati, kwanini wasichukue kitu kidogo?
 
Back
Top Bottom