Boss wa Takukuru Kilimanjaro akiona cha moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Boss wa Takukuru Kilimanjaro akiona cha moto

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Domhome, Jul 29, 2010.

 1. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro aliemkamata DC ahamishwa, ashushwa cheo.

  Taarifa za uhakika zinasema kuwa kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Kilimanjaro ambaye maafisa wake walimkamata Mkuu wa Wilaya ya Kasulu kwa tuhuma za kugawa rushwa hapo juzi, hivi leo amekabidhi barua ya kuhamishwa kituo chake cha kazi na kupelekwa mkoa mwingine lakini akiwa si kamanda tena bali afisa tuu wa kawaida.

  Hii inatosha kuashiria kwamba HOSEAH amebanwa na mkuu wa kaya kwamba kwanini anawazalilisha wateule wake wa kutoka chama tawala, HOSEAH kumbe hana ujanja, na huyo mama hata mchakato wa kumfikisha mahakamani umesimamishwa.


  Chanzo: Mmoja wa wafanyakazi wa Takukuru huko Kilimanjaro.
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  tetesi au kweli?
  unayo hiyo copy ya barua uiweke hapa?
   
 3. Mkeshahoi

  Mkeshahoi JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2010
  Joined: Jan 4, 2009
  Messages: 2,494
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  :shock:
   
 4. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Mkuu nimesema chanzo ni kutoka mmoja wa wana takukuru Kilimanjaro. Bado anajitahidi angalau aidake hyo copy, akiipata basi ntawawekea.
   
 5. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Hili jamvi mmeshalifanya shamba la bibi vile!!! mtu anaweza kukurupuka tuu na kuweka habari zake alizoamua basi. Weka fact ili wajuzi watujuze mengi. SORRY!!
   
 6. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,470
  Likes Received: 5,852
  Trophy Points: 280
  Sasa huyo mkuu wa kaya kwanini asimtimue Hosea?...maana mteule mwingine kadakwa Tabora je na kamanda wa huko ataadabishwa?
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wala sitashangaa iwapo habari hii itakuwa ni ya kweli. Maana hiyo ndo level ya juu kabisa ya uwezo wa serikali ya CCM katika kusimamia shughuli za kitaifa. Hata makamanda wa polisi ambao wamekuwa mstari wa mbele kupambana na majambazi wengi wao huwa wanaishia kufanyiwa haya haya. Kwa hiyo kama hili limefanyika Kilimanjaro basi hiyo ni sahihi kabisa, maana ndiyo hiyo ndiyo hasa kazi ya CCM. Kuwabana watenda kazi makini na kuwabeba mafisadi.
   
 8. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Nadhani hii imeshathibitika sasa. Je, kweli Takukuru watafanyakazi kwa moyo?

  Ni vyema Serikali ya CCM ikawaambia Makamanda wa Takukuru kuwa, wanaopaswa kukamatwa ni wale wote waliokuwa vinara wa kupinga ufisadi tu kuliko kuwafanya hawajui kazi kisa wamewakamata wanamtandao. Shame to you (CCM na Serikali yake).
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hii imeshathibitishwa kuwa ni kweli maana imetangazwa rasmi leo asubuhi. Lakini kwani kosa lake hasa ni nini?
   
 10. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #10
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 2,004
  Likes Received: 1,054
  Trophy Points: 280
  Huenda Mama ni mwana mtandao!

  Na kwa hili hata ungekuwa wewe unge-react vice versa na hasa kama uko CCM.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Dah kumbe wengine hawagusiki ukiwagusa tu kazi huna.
  Sasa si waseme wazi tu TAKUKURU ni kwa ajili ya wale wanao pinga wanamtandao.
   
 12. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #12
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli basi waweza kuona kama kweli hiki chama kinatufaa hata siku moja. Ni ufisadi tu!
   
 13. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #13
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,525
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  NI KWELI ACHA UBISHI. Soma magazeti ya leo
   
 14. L

  Lubaluka JF-Expert Member

  #14
  Jul 30, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 496
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ni kweli habari hii imethibitishwa na kutangazwa asubuhi hii, na Takukuru wenyewe wamedai zoezi
  la uhamisho kabisa. Uhamisho unafanyika wakati wowote bila kujali ni kipindi cha kiangazi au ni kipindi cha
  mavuno kama hikiii !!!! Wacha weweeee!!! yaani sipati pichaa !!!!
   
 15. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  mmmh hii ndo nchi ya wenye meno, wenye mapengo ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...............................:lalala:
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Pamoja na haya yote bado utawakuta watanzania, tena wakiwemo wasomi, wanaishabikia CCM. :fear:
   
 17. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,944
  Likes Received: 2,091
  Trophy Points: 280
  Hata Mwananchi ya leo (30/07/2010) ina habari hii!
   
 18. O

  Omumura JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni silent move ya kuwaambia TAKUKURU kwamba, sasa mwisho kuwagusa wateule, chenge na wenzake
  sasa watapumua, hii ndo Tanzania lakini sio ile aliyoiacha MWALIMU!
   
 19. X

  Xavery Member

  #19
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 30, 2010
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli basi nawaasa maafisa wa TAKUKURU kuwa "if you can't beat join them"
   
Loading...