Boss kuweka mshahara mezani

Machepele

JF-Expert Member
Jun 28, 2019
288
418
Habari zenu wana JF.

Ni kitambo kimepita tangu nimeajiriwa Kwenye kampuni moja la masuala ya printing.

Mwezi wa kwanza kuajiriwa nililipwa mshahara na boss wangu mkono kwa mkono.

Lakini kwa mwezi uliofuata aliweka mezani akaniambia nichukue, nikachukua sikushituka kwa lolote.

Mara ya pili pia akaniita ofisini kwake nikaenda, akahesabu pesa kisha akaweka mezani, hapo ndipo nikaanza kupatwa na ufahamu na kumbukumbu za mishahara ya nyuma.

Mara ya tatu, boss alifika akaweka pesa mezani akatoka alipofika nje akapiga simu kuwa pesa ipo mezani nitachukua.

Wakuu nimeamua nije kwenu walau nipate ufafanuzi juu ya hali kama hii, ni nini maana yake? Vipi hii ni dalili mbaya juu ya ile pesa. MSAADA.

Wenu mtiifu
MJUZI WA JUZI
 
Hela ni roho, sasa fahamu roho zina sifa zipi, moja huishi milele, husikia na kukaa na mtu au watu na pia humtoka mtu ....

Hofu yako ndo itakuletea uhalisia wa unachokihofia na ujasiri wako hukuletea na unachokiamini, kumbuka imani ina nguvu kuliko matendo.

Kwa hali ya kawaida tuu, isemeshe hiyo hela ikiwa hapo mezani na iamrishe ikutumikie wewe na isahau maagizo yote iliyopewa toka huko ilikotoka na kuwa kuanzia hapo wewe ndo mmiliki wake maana ni mshahara na uko kwa matamshi ya jina lako. Kisha hapo waweza ichukua kwa kujiamini na kuitumia kwa maarifa na akili. Itume na isemeshe hela ikutumikie sio wewe uitumikie.

Sio ndumba wala kichumio, ndio maana sadaka kule madhabahuni huwa inaombewa na kubarikiwa maana inatolewa kma sadaka lakini imetoka kwa watu wengi mbalimbali.
 
Piga hela Mzee Baba hiyo ni halali yako, yeye (Boss) anachofanya kinamsaidia katika mambo yake na wala haihusiani kabisa na hela yako, ni kama anachofanya Jiwe, kutwa kuzunguka Kwa waganga ili mambo yake ya kiutawala yaende Sawa, lakni wafanyakaz wa serikali wenyewe wanajua kupokea mwisho wa mwezi, hawajui hyo hela imetoka wapi na jamaa (Jiwe) anaisoteaje ili awalipe...mambo ni mengi sana duniani hapa
 
Chamaana ukishaichukua wewe hesabu kisha zigawe mafungu kumi yanayolingana, fungu moja peleka sehemu yako ya ibada au kwa wahitaji. Ni ya Mungu hiyo. Mitego yote inakwisha.
 
Acha hizo mkuu jiwe huyuhuyu tunaye sali naye kila Jumapili
 
Hela ni roho, sasa fahamu roho zina sifa zipi, moja huishi milele, husikia na kukaa na mtu au watu na pia humtoka mtu ....

Hofu yako ndo itakuletea uhalisia wa unachokihofia na ujasiri wako hukuletea na unachokiamini, kumbuka imani ina nguvu kuliko matendo.

Kwa hali ya kawaida tuu, isemeshe hiyo hela ikiwa hapo mezani na iamrishe ikutumikie wewe na isahau maagizo yote iliyopewa toka huko ilikotoka na kuwa kuanzia hapo wewe ndo mmiliki wake maana ni mshahara na uko kwa matamshi ya jina lako. Kisha hapo waweza ichukua kwa kujiamini na kuitumia kwa maarifa na akili. Itume na isemeshe hela ikutumikie sio wewe uitumikie.

Sio ndumba wala kichumio, ndio maana sadaka kule madhabahuni huwa inaombewa na kubarikiwa maana inatolewa kma sadaka lakini imetoka kwa watu wengi mbalimbali.
kasie
 
Chamaana ukishaichukua wewe hesabu kisha zigawe mafungu kumi yanayolingana, fungu moja peleka sehemu yako ya ibada au kwa wahitaji. Ni ya Mungu hiyo. Mitego yote inakwisha.
I wish mtoa post asome hi
 
Nakupa mshahara unanitangaza huku jamiiforums kesho usikanyage kazini katafute bosi mwingine
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom