Kindimbajuu
JF-Expert Member
- Jul 8, 2009
- 710
- 245
Jamani niko mbioni kutafuta mke mwingine baadaya shemeji yenu kukataliwa na boss wake kuja kuja kuishi na mimi.
Ni takribani miaka miwili sasa tangu nifunge ndoa takatifu na shemeji/wifi yenu,lakini kulingana na mazingira ya kazi nimekuwa nikiishi mbali na mke wangu na tunakutana mara moja moja kama wanafunzi na shemeji/wifi yenu.Hii yeto inatokana na ukiritimba pamoja na urasimu ninaofanyiwa na boss huyu, ambaye ni Afisa Elimu katika Wilaya ya Bahi.Angekuwa mwanaume ningesema anamtaka mke wangu,bahati nzuri ni mwanamke.
Hata hivyo nashindwa kuelewa mama huyu ana mpango gani na maisha ya ndoa yangu,eti anadai hawezi kumpa uhamisha hadi wilaya yake itakapo kuwa na walimu wa kutosha! kwa hakika bado wapo viongozi wasio tambua wala kuamini kuwa Dunia huzunguka Jua
Naomba ushauri na muongozo wa kisheria kwenu kuhusu vigezo vya mtumishi kuhama kumfuata mwenza wake.
kuna vitu viwili mbele ya shemeji yetu, naomba umfikishie maswali haya ninayokuuliza. jibu atakalokupa ndio litakalokufanya uamue ndoa ivunjike au la.
1. kati ya kazi na ndoa kwake muhimu nini?- hapa jibu kama ni kazi basi mwulize swali hili la pili. lakini kama jibu lake kuwa ndoa ni muhimu basi aandike barua ya kuacha kazi
2. yupo tayari kuacha kazi ili aje atafute kazi ya ualimu hapo ulipo wewe?