Je, mnaishi kama mume na mke au mnaishi kama wanandoa?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,916
Kuna tofauti kubwa ya kuishi kama mume na mke, kuishi kama wanandoa na kuishi kwenye ndoa

Ukaribu
Kushare hisia njema na mbaya
Kushare fikra na matamanio binafsi, ndoto na maono
Uaminifu
Upendo
Heshima na kujali
Fadhaa na fanaka nk
Haya mambo huamua aina ya mahusiano yenu mliyonayo

Utambulisho wa mwenza mbele ya hadhira
Muito/namna ya kumuita mwenza wako
Majina ya utani mnayopeana
Mavazi yenu
Kula ye nu
Kunywa yenu
Tembea yenu
Kila kimoja huwatambulisha afya ukaribu, ukweli na patano kati yenu..

Huyu ndio mume/mke wangu mpenzi
Huyu ndio mwenza wangu
Huyu ndio baba/mama watoto wangu
Huyu ndio shemeji yako/yenu
Huyu ndiye niliyefunga naye ndoa
Huyu ndiye ninayeishi naye
Huyu ndio asali, pumzi ya mtima wangu..!

Utambulisho hufanyika kwa bashasha na furaha ama kwa sauti ya chini na kuona haya kidogo?

Kuna wakati wa kuzoeana
Kuna wakati wa kuchokana
Kuna wakati wa kuchunguzana
Kuna wakati wa kuoneana mapungufu yaliyokuwa yamejificha hapo nyuma
Kuna nyakati za kugundua kumbe ulimpata mtu sahihi na kuzidisha upendo mara dufu

Heshima na upendo havioneshwi kwa kupeana shikamoo na bali kwakuwa mwaminifu kwa mwenza wako kwa kuheshimu utupu wako na kuulinda kwa gharama zote ukimtunzia yeye tu..!
dfabf1d810972e46c3b7559371a1ed4f.jpg
 
Hakuna ukweli tena
Hakuna uaminifu tena
Hakuna upendo wa kweli tena
we fikiria tu taasisi ya familia kumekuwa na damage beyond repair. Watoto wanalelewa na wasafi tv . Ngono baina ya binti na baba yake n.K Ndio useme kutakuwa na family bond? Talaka imekuwa kama fasheni nowdays, pesa imekuwa kipimo cha utu. Udhalimu ndio unapewa nafasi na kupigiwa chapuo.
 
Bali kwakuwa mwaminifu kwa mwenza wako kwa kuheshimu utupu wako na kuulinda kwa gharama zote ukimtunzia yeye tu..!


Hapo pagumu sana
 
Ndoa nyingi za sasa tunatoka background tofauti na watu hawapeani muda wa kujuana na kuchunguzana vema ni kubebana tuu
Mkuu mbona wazazi wetu walikua wanaoana pasipo kupitia kipindi cha cohabitation lakini ndoa zao zipo imara mpaka leo.

To my view naona ni bora tukarejelea mila zetu za zamani za kuchaguliwa wachumba na ndugu kama wazazi, shangazi and the like.

Ni vigumu sana kuachana na mke au mume ambae familia yako imeona ndie anaekufaa, contrary to that ni aibu kwa familia husika na hamna familia iliyo tayari kupokea iyo aibu.

Mbona familia za kitajiri still wanachaguliana wachumba, sisi tia maji sijui tunakwama wapi
 
Back
Top Bottom