Boss anataka kuniangamiza kimapenzi

Boss anataka kuniangamiza kimapenzi

Wanajamii habari za mchana?
Namshukuru mwenyezi mungu kwa hatua niliyofikia, kimjumla nimeoa na nina watoto wawili na ninafanyakazi katika sekta ya Afya, nimeajiriwa mwaka mmoja uliopita (Ni Ajira ya Kudumu) na nipo maeneo ya Mkoa wa Kagera. Katika Idara yetu ya Afya kuna Vitengo mbalimbali na mkuu wa Idara ya Afya.

Kipindi nilichoajiliwa nilikutana na watu wa aina mbalimbali na makabila ya aina mbalimbali kazini ila kuna mdada mmoja yeye alikuwa mratibu wa kitengo fulani ndani ya Idara. Sikuwa namfahamu kwa undani kwani sikuwa na muda wa kumsoma mtu.

Siku moja tulisafiri kikazi kwenda Mwanza naye kwenye gari ya ofisi, tulipofika Mwanza Dereva alituacha Kantema Hotel ili tufanye mpango wa kupata malazi, yule mdada aliniomba tuchukue chumba kimoja tulale pamoja ili tupunguze gharama za huduma ya malazi, mimi nilipinga kwa nguvu zangu zote hilo suala nikijua outcome yake itakuwa mbaya, ila mwisho ilibidi awe mkweli kwa dhamira yake hiyo ya kulala chumba kimoja nami ili kumtimizia mahitaji yake ya kingono nilikataa kabisa na nikahamua kutoka nje na kuchukua taxi hadi Planet Hotel nikachukua chumba. Hakufanikiwa na dhamira yake japokuwa katika wiki moja tuliyokaa Mwanza hakuwa na ushirikiano nzuri na mimi wa kikazi haswa kazi tuliyoenda kifanya kwa kiwango kikubwa kazi hile niliifanya peke yangu na ugeni niliokuwa nao kazini na kuimaliza na tukarudi wote, japo dereva alishangaa mie kubadilisha Hotel lakini sikuwahi kumwambia nini kilitokea.

Ikapita miezi miwili mkuu wetu wa Idara ya Afya alipata na matatizo ya kikazi, yule mdada alichaguliwa kuwa mkuu wa idara kwa muda mpaka hapo mambo yakatapoenda vizuri.

Ilipita miezi nane kuteuliwa Mkuu Mpya wa Idara, yule mkuu mpya wa Idara hakuwa miongoni mwa wakuu wa vitengo ilimbidi afanye kazi kwa karibu na huyu dada ili kuweza kuzoea na kuyasoma mazingira ya kazi. Katika kipindi hicho cha mpito hawa wakawa wapenzi japokuwa mkuu wa Idara aliyeteuliwa alikuwa ameoa na ana watoto watatu.

Toka kipindi cha huyu dada kuwa anakaimu ukuu wa Idara hadi sasa hivi amekuja mkuu wa Idara mwenye mambo yangu ya kikazi hayaendi vizuri kabisa, nipo neglected kazini hata shughuli inayonihusu mimi anapewa mtu mwingine aifanye.

Wanajamii natamani niache kazi, ila siwezi, naombeni ushauri wenu plsss!!!!

This is your private business. I am out!
 
Usiogope kwa jinsi ulivyomheshimu Mungu na ndoa yako Mungu naye atakuheshimu pia, hongera kwa kushinda jaribu la kwanza, endelea usikate tamaa hao ni ngazi ya ww kupanda juu, Mungu atakulinda na mabaya yote, usilegeze hata kidogo,endelea kumwomba Mungu huku ukiomba uhamisho,ikishindikana pia usijali jua Mungu amekusudia ili akupatie ushindi mkuu.
 
It happens a lot, hasa kwetu sisi wanawake. Anyway, ungekuwa kwenye mashirika ni rahisi kuacha kazi na kutafuta kungine; lkn serikalini kuacha mafao yako because of that. Kama unaweza kwenda wizarani (adm) ukawaeleza matatizo yako na chanzo chake (ingawa ni ngumu kwa mwanamume kuaminika ktk hili) wangekusaidia kukupa uhamisho. You did a brave thing in Mwanza, wewe ndio unastahili kuitwa MWANAUME. Cheers!

Inawezekana na wala sio ngumu kuomba uwamisho
Cha msingi ajipange vzr atakapokwenda wizarani au aseme yuko idara gani uwendo kuna au yuko mtu umu anaweza kumsaidia kwa hilo
Kwa kweli ni kero haswa kwa wakina dada na upande wetu sisi wanaume mambo yanakuwa magumu bosi akiwa anamgegeda mwanamke aliekuwa asimu wako aisee kazi utaiyona chungu
 
Back
Top Bottom