Boss anataka kuniangamiza kimapenzi

Boss anataka kuniangamiza kimapenzi

Mahmetkid

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2012
Posts
732
Reaction score
444
Wanajamii habari za mchana?
Namshukuru mwenyezi mungu kwa hatua niliyofikia, kimjumla nimeoa na nina watoto wawili na ninafanyakazi katika sekta ya Afya, nimeajiriwa mwaka mmoja uliopita (Ni Ajira ya Kudumu) na nipo maeneo ya Mkoa wa Kagera. Katika Idara yetu ya Afya kuna Vitengo mbalimbali na mkuu wa Idara ya Afya.

Kipindi nilichoajiliwa nilikutana na watu wa aina mbalimbali na makabila ya aina mbalimbali kazini ila kuna mdada mmoja yeye alikuwa mratibu wa kitengo fulani ndani ya Idara. Sikuwa namfahamu kwa undani kwani sikuwa na muda wa kumsoma mtu.

Siku moja tulisafiri kikazi kwenda Mwanza naye kwenye gari ya ofisi, tulipofika Mwanza Dereva alituacha Kantema Hotel ili tufanye mpango wa kupata malazi, yule mdada aliniomba tuchukue chumba kimoja tulale pamoja ili tupunguze gharama za huduma ya malazi, mimi nilipinga kwa nguvu zangu zote hilo suala nikijua outcome yake itakuwa mbaya, ila mwisho ilibidi awe mkweli kwa dhamira yake hiyo ya kulala chumba kimoja nami ili kumtimizia mahitaji yake ya kingono nilikataa kabisa na nikahamua kutoka nje na kuchukua taxi hadi Planet Hotel nikachukua chumba. Hakufanikiwa na dhamira yake japokuwa katika wiki moja tuliyokaa Mwanza hakuwa na ushirikiano nzuri na mimi wa kikazi haswa kazi tuliyoenda kifanya kwa kiwango kikubwa kazi hile niliifanya peke yangu na ugeni niliokuwa nao kazini na kuimaliza na tukarudi wote, japo dereva alishangaa mie kubadilisha Hotel lakini sikuwahi kumwambia nini kilitokea.

Ikapita miezi miwili mkuu wetu wa Idara ya Afya alipata na matatizo ya kikazi, yule mdada alichaguliwa kuwa mkuu wa idara kwa muda mpaka hapo mambo yakatapoenda vizuri.

Ilipita miezi nane kuteuliwa Mkuu Mpya wa Idara, yule mkuu mpya wa Idara hakuwa miongoni mwa wakuu wa vitengo ilimbidi afanye kazi kwa karibu na huyu dada ili kuweza kuzoea na kuyasoma mazingira ya kazi. Katika kipindi hicho cha mpito hawa wakawa wapenzi japokuwa mkuu wa Idara aliyeteuliwa alikuwa ameoa na ana watoto watatu.

Toka kipindi cha huyu dada kuwa anakaimu ukuu wa Idara hadi sasa hivi amekuja mkuu wa Idara mwenye mambo yangu ya kikazi hayaendi vizuri kabisa, nipo neglected kazini hata shughuli inayonihusu mimi anapewa mtu mwingine aifanye.

Wanajamii natamani niache kazi, ila siwezi, naombeni ushauri wenu plsss!!!!
 
Wanajamii habari za mchana?
Namshukuru mwenyezi mungu kwa hatua niliyofikia, kimjumla nimeoa na nina watoto wawili na ninafanyakazi katika sekta ya Afya, nimeajiriwa mwaka mmoja uliopita (Ni Ajira ya Kudumu) na nipo maeneo ya Mkoa wa Kagera. Katika Idara yetu ya Afya kuna Vitengo mbalimbali na mkuu wa Idara ya Afya.

Kipindi nilichoajiliwa nilikutana na watu wa aina mbalimbali na makabila ya aina mbalimbali kazini ila kuna mdada mmoja yeye alikuwa mratibu wa kitengo fulani ndani ya Idara. Sikuwa namfahamu kwa undani kwani sikuwa na muda wa kumsoma mtu.

Siku moja tulisafiri kikazi kwenda Mwanza naye kwenye gari ya ofisi, tulipofika Mwanza Dereva alituacha Kantema Hotel ili tufanye mpango wa kupata maradhi, yule mdada aliniomba tuchukue chumba kimoja tulale pamoja ili tupunguze gharama za huduma ya maradhi, mimi nilipinga kwa nguvu zangu zote hilo suala nikijua outcome yake itakuwa mbaya, ila mwisho ilibidi awe mkweli kwa dhamira yake hiyo ya kulala chumba kimoja nami ili kumtimizia mahitaji yake ya kingono nilikataa kabisa na nikahamua kutoka nje na kuchukua taxi hadi Planet Hotel nikachukua chumba. Hakufanikiwa na dhamira yake japokuwa katika wiki moja tuliyokaa Mwanza hakuwa na ushirikiano nzuri na mimi wa kikazi haswa kazi tuliyoenda kifanya kwa kiwango kikubwa kazi hile niliifanya peke yangu na ugeni niliokuwa nao kazini na kuimaliza na tukarudi wote, japo dereva alishangaa mie kubadilisha Hotel lakini sikuwahi kumwambia nini kilitokea.

Ikapita miezi miwili mkuu wetu wa Idara ya Afya alipata na matatizo ya kikazi, yule mdada alichaguliwa kuwa mkuu wa idara kwa muda mpaka hapo mambo yakatapoenda vizuri.

Ilipita miezi nane kuteuliwa Mkuu Mpya wa Idara, yule mkuu mpya wa Idara hakuwa miongoni mwa wakuu wa vitengo ilimbidi afanye kazi kwa karibu na huyu dada ili kuweza kuzoea na kuyasoma mazingira ya kazi. Katika kipindi hicho cha mpito hawa wakawa wapenzi japokuwa mkuu wa Idara aliyeteuliwa alikuwa ameoa na hana watoto watatu.

Toka kipindi cha huyu dada kuwa anakaimu ukuu wa Idara hadi sasa hivi amekuja mkuu wa Idara mwenye mambo yangu ya kikazi hayaendi vizuri kabisa, nipo neglected kazini hata shughuli inayonihusu mimi anapewa mtu mwingine aifanye.

Wanajamii natamani niache kazi, ila siwezi, naombeni ushauri wenu plsss!!!!

Sijaelewa unamaanisha nini hapo nilipoweka rangi nyekundu mkuu? rekebisha au fafanua vizuri kisha tuendelee
 
It happens a lot, hasa kwetu sisi wanawake. Anyway, ungekuwa kwenye mashirika ni rahisi kuacha kazi na kutafuta kungine; lkn serikalini kuacha mafao yako because of that. Kama unaweza kwenda wizarani (adm) ukawaeleza matatizo yako na chanzo chake (ingawa ni ngumu kwa mwanamume kuaminika ktk hili) wangekusaidia kukupa uhamisho. You did a brave thing in Mwanza, wewe ndio unastahili kuitwa MWANAUME. Cheers!
 
Duuh uko katika hali ngumu Mkuu ila kuna wakati inabidi u-take drastic measures kulinda kitumbua.. Ushauri wangu kuhusu kitendo kilichopita ungemvalia kinga na kumpelekea alichokitaka.. Ila kwa sasa wewe piga kazi yako hapo na wala ucimuweke kichwani.. Akileta chokochoko andika barua ya malalamiko citing a past misunderstanding between u two.. Ila uciende deep kwenye hiyo barua lakini kwa yeye mpe live kwamba ushahidi unao kwamba alikutokea ukampa kibuyu..

Ila mkuu una mcimamo.. Mwanamke amekuhamisha hoteli..?
 
Acha complication ambazo hazina maana,umeelewa sana mkuu!!hayo ni matatizo kdg tu ya lugha
Toa ushauri?
 
Pole sana mkuu!
Jambo hilo ni serious sana kwa mtu mbaye yuko commited na familia yake.
Yaelekea huyo dada anatumia ngono kama silaha ya kuwateka wafanyakazi ili wamridhishe yeye na tamaa zake.
Kuwa na msimamo mmoja kaka, komaa usiingizwe kwenye mapenzi ya kulazimishwa, huwezi jua huyo mama ana tatizo gani!
 
duuuu cjawah öna mdada analazimishwa kupewa dushelele kinguvu.
 
It happens a lot, hasa kwetu sisi wanawake. Anyway, ungekuwa kwenye mashirika ni rahisi kuacha kazi na kutafuta kungine; lkn serikalini kuacha mafao yako because of that. Kama unaweza kwenda wizarani (adm) ukawaeleza matatizo yako na chanzo chake (ingawa ni ngumu kwa mwanamume kuaminika ktk hili) wangekusaidia kukupa uhamisho. You did a brave thing in Mwanza, wewe ndio unastahili kuitwa MWANAUME. Cheers!

Asante kwa Mchango wako Kaunga, hata mimi nilikuwa nawaza kutafuta uhamisho.
 
Duuh uko katika hali ngumu Mkuu ila kuna wakati inabidi u-take drastic measures kulinda kitumbua.. Ushauri wangu kuhusu kitendo kilichopita ungemvalia kinga na kumpelekea alichokitaka.. Ila kwa sasa wewe piga kazi yako hapo na wala ucimuweke kichwani.. Akileta chokochoko andika barua ya malalamiko citing a past misunderstanding between u two.. Ila uciende deep kwenye hiyo barua lakini kwa yeye mpe live kwamba ushahidi unao kwamba alikutokea ukampa kibuyu..

Ila mkuu una mcimamo.. Mwanamke amekuhamisha hoteli..?

Asante kwa ushauri wako Mkuu, nimemvumilia sana huyu dada, huwa tunavikao vya kila mwezi nimeshawai kulizungumzia juu kwa juu kuhusu kuwanyanyasa wafanyakazi walio chini yetu ila safu yenyewe ya oungozi ndiyo hivyo tena.
 
Pole sana mkuu!
Jambo hilo ni serious sana kwa mtu mbaye yuko commited na familia yake.
Yaelekea huyo dada anatumia ngono kama silaha ya kuwateka wafanyakazi ili wamridhishe yeye na tamaa zake.
Kuwa na msimamo mmoja kaka, komaa usiingizwe kwenye mapenzi ya kulazimishwa, huwezi jua huyo mama ana tatizo gani!

Thanks PakaJimmy, unafikiri ni mmama, ni mdada niliyemzidi miaka mitano ya umri
 
Komaa tu mbona hayo yana mwisho akizidisha kubana itafahamika tu kama ulivyodhihirisha ujasiri wako kwa kukataa ngono onesha pia ujasiri kwenye kuipita hiyo hali ngumu.MATATIZO HUWA HAYAKIMBIWI BALI HUTAFUTIWA SULUSHENI KAKA.
 
kweli mwanawane nimekukubali!!! hongera sana maana huyo alitaka kukupakazia ngoma tuu hana lolote
 
Asante kwa ushauri wako Billie, bado nakomaa nao japokuwa nao bado wananifuatilia kwa ukaribu na kuvizia wapi niharibu wao wanichukulie hatua.
 
kweli mwanawane nimekukubali!!! hongera sana maana huyo alitaka kukupakazia ngoma tuu hana lolote

Hata mie nilikuwa najiuliza sababu haswa ya kufanya ilichokitaka kikifanya nini? Bado sijapata jibu hana nini haswa, ila muda utakapofika nitapata jibu kwa hao aliotembea nao.
 
yeah mwana vumilia tuu huku anaanza tafuta other means za kupata kazi sehemu nyingine
 
Back
Top Bottom