Boss anataka kufungua biashara kupitia kitambulisho changu. Je, kuna madhara?

Sidhani kwanza taratibu za nchi zinaruhusu mtu A afungue biashara kwa kutumia jina la mtu B. Anaweza kufanya mambo mengi katika biashara yake ambayo hayaruhusiwi akijua fika kwamba wakimstukia basi si yeye atakayekamatwa.
Nimkwepe kwa njia gani nzuri mkuu ili nisije nikamkwaza halafu akaanza figisu na ukichukulia kuwa kazi yake ndo inaniweka hapa mjini kwa sasa?
 
Greetings Great Thinkers!

Nilianzisha huu uzi,

Naondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha, naenda Iringa kwanza. Mwenye kazi au connection tafadhali na hatimaye nilifika salama.

Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, nimekuja kupata kazi kwenye LODGE fulani hapa Iringa mjini na nina wiki kama 2 hivi tangu nianze kazi.

Kazi yangu huwa napiga usiku halafu mchana napiga vibarua vya hapa na pale.

Katika siku chache hizi, boss wangu ametokea kuniamini kwa kiasi fulani ambapo amesema kuna biashara yake anataka kuifungua ila ameniomba kitumike kitambulisho changu.

Je, hii ipoje wakuu? Ni sahihi? Nini madhara yatakayoweza kutokea labda huko mbeleni lets say nikiamua baadae kuondoka au kuacha kazi?

Naombeni ushauri & nawatangulizia shukurani!
Yaan hapo unaidanganya Jamhuri.
 
Alitaka kitambulisho cha mpiga kura.

tukiachana na maswala ya kuwa anacho au hana kitambulisho.

Je, ni madhara gani yanaweza kujitokeza endapo kitatumika cha kwangu?

Je, namna nzuri ya kuukwepa huu mtego ni ipi? Maana alikwishampigia mkewe ila nikamwambia asubiri kesho tuzungumze vizuri.
Wewe ni mtu mzima. Unaweza kumkwepa kwa kumwambia ukweli haupo tayari kwa kumwambia kuwa kitambulisho chako na Kaka yako anakitumia pia.

Madhara yake ni kwamba endapo akifungua biashara na kupata TIN NAMBA ya biashara kwa jina lako na baadae akakwepa kulipa kodi maana yake wewe ndio mmiliki halali wa hiyo TIN itakubidi wewe ndio ulipe Hilo then hautauweza kufungua biashara yoyote katika mfumo rasmi wa biashara

CHAGUO N LAKO KUMPA AU KUSITISHA

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Huu msala, kuna jamaa tumekutana naye mahabusu yeye kakaa siku zaidi ya 20 ndani bila dhamana alisajilia mtu laini na mhusika akawa anatapeli watu mtandaoni kupitia hiyo line na taarifa ni za mwana. Jamaa katapeli zaidi ya 60M ndipo walipofuatilia taarifa za line wakakuta ni za huyu mchizi wakajua ni yeye alienda bebwa na maafisa. Jamaa hajui lolote.

So mtu kutumia taarifa zako ni very risk.

Kuwa naye makini kama ni ndugu na kama humuamini kwa mwenendo wake fanya maamuzi chukua line yako.
Asipokuelewa hapa basi yeye ni sikio la kufa

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Greetings Great Thinkers!

Nilianzisha huu uzi,

Naondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha, naenda Iringa kwanza. Mwenye kazi au connection tafadhali na hatimaye nilifika salama.

Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, nimekuja kupata kazi kwenye LODGE fulani hapa Iringa mjini na nina wiki kama 2 hivi tangu nianze kazi.

Kazi yangu huwa napiga usiku halafu mchana napiga vibarua vya hapa na pale.

Katika siku chache hizi, boss wangu ametokea kuniamini kwa kiasi fulani ambapo amesema kuna biashara yake anataka kuifungua ila ameniomba kitumike kitambulisho changu.

Je, hii ipoje wakuu? Ni sahihi? Nini madhara yatakayoweza kutokea labda huko mbeleni lets say nikiamua baadae kuondoka au kuacha kazi?

Naombeni ushauri & nawatangulizia shukurani!
Kitambilisho sana sana kinahitajika TRA unavyochukua TIN namba na hivyo basi wewe mwenye kitambilisho ndio utakuwa unatambulika kama mlipa Kodi na ikitokea boss halipi Kodi ni wewe utakayedakwa yeye hawezi kuguswa kwa sababu hamna sheria inayoruhusu kufungua biashara kwa kitambilisho kisicho Cha mmiliki

USHAURI WANGU
Sio vizuri sana kumkubalia ila kama unamuamini kubali tu pengine utaongezewa mshahara au kupandishwa cheo kabisa
 
Ahsante sana Mkuu.

Kitambilisho sana sana kinahitajika TRA unavyochukua TIN namba na hivyo basi wewe mwenye kitambilisho ndo utakuwa unatambulika kama mlipa Kodi na ikitokea boss halipi Kodi ni wewe utakayedakwa yeye hawezi kuguswa kwa sababu hamna sheria inayoruhusu kufungua biashara kwa kitambilisho kisicho Cha mmiliki
USHAURI WANGU
Sio vizuri sana kumkubalia ila kama unamwamini kubali tu pengine utaongezewa mshahara au kupandishwa cheo kabisa
 
Greetings Great Thinkers!

Nilianzisha huu uzi,

Naondoka nyumbani kwenda kutafuta maisha, naenda Iringa kwanza. Mwenye kazi au connection tafadhali na hatimaye nilifika salama.

Baada ya kukaa kwa siku kadhaa, nimekuja kupata kazi kwenye LODGE fulani hapa Iringa mjini na nina wiki kama 2 hivi tangu nianze kazi.

Kazi yangu huwa napiga usiku halafu mchana napiga vibarua vya hapa na pale.

Katika siku chache hizi, boss wangu ametokea kuniamini kwa kiasi fulani ambapo amesema kuna biashara yake anataka kuifungua ila ameniomba kitumike kitambulisho changu.

Je, hii ipoje wakuu? Ni sahihi? Nini madhara yatakayoweza kutokea labda huko mbeleni lets say nikiamua baadae kuondoka au kuacha kazi?

Naombeni ushauri & nawatangulizia shukurani!
Labda kama anataka muwe Partners.Inawezekana Ila kama anataka wewe ndo uwe mmliki kwa 100% basi hakikisha unajiridhisha kwamba kuna maslahi kwako ya kukufanya urisk kwa kiwango hicho
 
Alitaka kitambulisho cha mpiga kura.

tukiachana na maswala ya kuwa anacho au hana kitambulisho.

Je, ni madhara gani yanaweza kujitokeza endapo kitatumika cha kwangu?

Je, namna nzuri ya kuukwepa huu mtego ni ipi? Maana alikwishampigia mkewe ila nikamwambia asubiri kesho tuzungumze vizuri.
Mfano jamaa anataka kitambulisho chako ili afungue kiwanda. Jina likitumika maana yake wewe ndiye mmiliki.

Sasa baadae huko ikajulikana kiwanda kilicho funguliwa kwa id yako kinakwepa kodi atakaye tafutwa ni mwenye jina (wewe)

Mfano mwingine..

Jina lako likatumika kufungulia kiwanda alafu huko badae ikatokea kazi au chance inayo taka mtu asiye jiweza kiuchumi..

Wakaja kicheki kwenye mfumo ukaonekana kuna kiwanda kina jina lako mpaka hapo unakosa nafasi maana wataona tayari una miliki kiwanda.

All in all jiulize kwann anataka kutumia id yako wakati na yeye anayo?

NB: Akili za kuambiwa changanya na zako.
 
Alitaka kitambulisho cha mpiga kura.

tukiachana na maswala ya kuwa anacho au hana kitambulisho.

Je, ni madhara gani yanaweza kujitokeza endapo kitatumika cha kwangu?

Je, namna nzuri ya kuukwepa huu mtego ni ipi? Maana alikwishampigia mkewe ila nikamwambia asubiri kesho tuzungumze vizuri.
Kama ni kitambulisho cha mpiga kura na unaona ukimkatalia utaharibu mahusiano yenu, mpe then kachukue Loss report police kaa nayo.

Utatunza ajira yako na mahusiano yako na boss na

Utakuwa salama endapo kitambulisho chako kitafanyiwa uhalifu.
 
Ukijua maana ya neno KITAMBULISHO utajua ni jinsi gani uko Karibu na hatari.......

Kwa kifupi ni kwamba utawajibika kwa kila matokeo yatakayotokana na matumizi ya hicho kitambulisho......lakini bahati mbaya mimi na wewe hatujui mini kitatokea kwenye matumizi ya hicho kitambulisho baada ya kufungua hiyo biashara........

NB;
Mtu isipomfaa akili yake basi utamdhuru ujinga wake........

Wahenga wanasema....PENYE KHERI SHARI HAIPO MBALI NA PENYE SHARI KHERI HAIPO MBALI.......maamuzi ni yako.....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom