Nyox official
JF-Expert Member
- Feb 12, 2019
- 597
- 455
afu lela ulela,stor za tangia tunasoma primary huko
Hakuna adhabu inauma sana kama ya kisaikolojia.Kuna kipindi enzi hizo nimemaliza advance nasubiri kwenda chuo nilikuwa naishi kwa bro alimpa mkewe adhabu kama hiyo, japo wao issue haikuwa cheating. Huyu shem wangu alikuwa hana time na kujali afya ya mumewe. Every time jamaa anatoka long safari anajinyima sana anabana hela walau afike nyumbani na mapocho pocho mengi. Unakuta njiani hali msosi akifika home hakuna hata uji wala chai. Mke yuko busy na normal family routine za msosi. Jamaa anaweza fika saa kumi jioni, akajikuta anasubiri tule msosi kwa ratiba ya saa mbili usiku, alafu ukute pamepikwa wali ambao jamaa siyo chakula chake.
Siku aliyochoka kuvumilia mateso, aliniita, akaniambia mdogo wangu, hawa wanawake ni mataira sana. Omba Mungu upate mke anayekujali la sivyo vidonda vya tumbo viko karibu. Akaniambia kuanzia sasa jifunze kuficha hela, mwanamke asijue kama una hela ya ziada, wakati mwingine upite sehemu ule chochote ili ukifika home hata kama mnachelewa kula usiteseke maana wewe unashinda shamba, la sivyo iko siku utazimia kwa njaa. Kweli bro akawa ananipa hela ya ziada tukiwa peke yetu bila shem kujua.
Ilifika kipindi uvumilivu ulimshinda bro. akaamua kujihudumia kwa kila kitu, kufua nguo zake, kupika chakula chake, kupasha maji ya kuoga asubuhi, ananyoosha nguo zake akienda ofisini, anaandaa breakfast, akirudi jioni anapita sokoni ananunua mahitaji, akifika nyumbani anaingia jikoni. Sasa kila kinachopikwa na mke jamaa hagusi. Hata kama pamepikwa ugali na yeye anataka ugali ataenda kupika wa kwake. Issue ilienda kama wiki moja hivi, mke aliblow, kuna siku alilia kama mtoto mdogo, akataka arudi kwao, jamaa akasema sawa nenda. Baadaye walisuluhishana na tangu siku hiyo mwanamke alinyooka. Then bro akaja kuniita tena akaniambia ukija kuoa, usije ukampiga mkeo... kama unaweza adhabu kama hizi ni bora mara mia. Aisee, wee acha tu inauma sana. Sasa nina miaka zaidi ya 10 sijawahi kupiga mtu, naitumia hii mbinu lakini kwa uchache sana maana nikigusa tu mtu chali...
Adhabu ya kisaikolojia ni mbaya kuliko adhabu zteMmmh, hatua hapana yaani ukae kimya tu ,we ndege ungefanya hivyo kweli?
Kabisa mkuu kuna nyingine ilitokea mkoani kwetu uko mke alienda gesti kuchepuka theb mume wake akapewa taarifa naye fasta akataka tu ashuhudie lile tukio akaenda mpaka gesti akawakuta akawaangalia tu then akaondoka akaendelea na mishe zake. Jioni wamekutana home mume kama hana habari kabisa anaongea na mke wake vizuri tuu anaomba apikiwe chakula, kuwekewa maji na walikua na watoto wawili anakaa na watoto anacheza nao yani kama hakufumania! Tatizo lilikua kwa mke tangu kafumaniwa hajawahi kukaa home na amani anaomba ushaur kwa marafiki zake kwann mme wake amemfumania na hajaongea kitu ! Yaani anatamani mume wake aongee au amtwange kwa kuchepuka but jamaa kama hana habari. Ilimtesa yule mama acheni tu! Mwisho wa siku baada ya kushindwa kuvumilia aliamua kujiua kwa kujichoma kisu jamaa akiwa kazini! Alifariki ameacha yatima wawili! Hii mbinu hatari sana yani ni one shot harudii tena maishani! They call it psychological torture!Adhabu ya kisaikolojia ni mbaya kuliko adhabu zte