Bora nikate tamaa ili niwe salama

Bora nikate tamaa ili niwe salama

hii logic ya maisha hupangwa na Mungu ngumu sana kuelewa,tunafundishwa kwamba Mungu anachukia maovu,je kama ni hivyo kwa nini anapanga watu wafanye maovu?au kaandaa moto kutukomoa??watu wengi wanaingia kwenye maovu sababu kuu ikiwa ni Mungu,mtu anamuomba Mungu miaka na miaka hamjibu,mtu anaona bora aende kwa shetan tu ambapo atapata majibu kwa muda huo huo,na hapo ndio mwanzo wa maovu!!
Kuna mdau mmoja huku alichangia uzi wa kifo cha Ali Mufuruki kwa kusema nanukuu “Kuna nyakati maisha yanakosa maana”. Ni kweli kabisa maisha ni zaidi ya tunavyofikiria kama wanadamu kwa imani yangu. Maisha ya kila mtu yamepangwa kabla kabisa na Mungu. Baada ya wewe kutekeleza lile lililokuleta hapa duniani unaondoka. Hizi stori za kwamba nitafute pesa,nijenge nyumba nzuri ni mipango yetu sisi wanadamu ila kwa Mungu halipo hivyo. Pia sijui unatumia kipimo gani kusema wewe upo situation mbaya,kuna watu wako vibaya achaa. Ushauri acha kuona huishi mpaka upate pesa,shukuru Mungu kwa kila jambo,kwani hamna mwanadamu mwenye uwezo katika haya maisha zaidi yake
 
Nlipokuwa mdogo (before 20yrs) ilikuwa kila nikitaka kitu nikapima na kuamini naweza kuwa ama kupata basi ilikuwa ni lazima nifanikishe ningeacha vyote nifocus na hicho tu mpaka ieleweke. Sasa nimekuwa mkubwa bado ni mtu wa strong desires yaani nikitaka nimetaka akili yangu itaumia kutafuta namna ya kufanikisha ninachotaka kwa nguvu zote lakini mambo yamekuwa magumu mno hayaji kirahisi na si tu kirahisi bali hata kwa nguvu zote ninazoapply ambazo nilipima nikaona inawezekana lakini mambo hayawezekani.

Maisha yangu ni kama yamesimama, mateso yanaongezeka , changamoto hazivumiliki (ugonjwa/ulemavu) nimeshindwa kufanikisha nilivyofikiri itawezekana lakini nashindwa kupotezea na kumuachia Mungu. Msemo wa Mungu hachelewi wala hawahi haufanyi kazi kwangu, siwezi kabisa vumilia zaidi kuendelea na maisha ya hivi lakini nifanye nini sielewi, nikweli ninayoyataka yapo nje ya uwezo wangu, mengine nje ya uwezo wa binadamu lakini napata machungu kuona kwanini isiwe yaani milango yote imefungwa sasa nitokee wapi, halafu kwanini iwe mimi tu?

Agrrrh... Nahisi kuchanganyikiwa! hii strong desire ya kuwa mtu fln kuishi katika level fln licha ya hali yangu sasa inanitesa vilivyo. Nikikaa kutwa nzima kichwa kinawaka moto nifanya nini na kila ninachoamini nikijaribu sifanikiwi, sitakiwi kuwa hapa nilipo, sitakiwi kuishi hivi, Huu ni mtihani mzito sana kwangu. Nawaza pengine uzito hasa unakuja kutokana na aina ya mtu niliye. Bora ningekuwa mtu nisiyeamini katika mafanikio, kama ningekuwa mtu wa kukubali kushindwa walahi nisingeteseka hivi pengine ningekuwa cool nimemwachia Mungu lakini kiukweli nimeshindwa kukata tamaa.

Nimejaribu kujiwekea miiko kwamba No social networks hasa hasa FB, whatsap groups labda zinaniongezea anxiety kwasababu kule wengi ninaowahamu naona ni kama wote wameridhika wanafurahia maisha yao. Nikiwaza hivi kweli namimi niridhike na hali hii BIG NO! Nikasema wacha niachane na mambo ya Inspirations, Motivations huko IG nikiingia watu wanafanya big moves, hata wauza sura wanaoshine kwa kufake life still wanaEnjoy life, wakina Ontario kila siku kutusema tunaosindikiza maisha, Quote yake moja anasema "Maisha hayajawahi kuwa selective, hayajui kama baba yako ni maskini au wewe ni kilema, kipofu, yatima. Maisha ni kama mvua ikinyeesha haiangalii kama kuna mtu kaanika mpunga, kuna mtu anajenga nyumba, kuna mtu anaanika nguo, haiangalii chochote same as life.

Ni jukumu lako kuwa na mwamvuli " Basi nikiona hivyo moyo unauma sana naona bora nihamie kwenye kushabikia udaku na story za kina Mondi kusogeza siku lakini nazo zinachosha big times. Sina rafiki, sina mpenzi wala sidhani kama nataka kuwa nao kwasasa maana hata marafiki niliokuwa nao hatumatch tena kama zamani na urafiki umefifia. Sifurahii kabisa kuishi hivi, bila kuwa ninavyotaka seriously sijioni kuumaliza mwaka 2020.

Nimekosa alternative ya vipi nibadili attitude niliyonayo, niiambie nini nafsi yangu ili iridhike akili yangu itulie just to be calm and patient nisisumbuke tena kujiwazia chochote. Kama kuhold endurance nimehold sana nimefika mwisho kabisa sasa nahisi hata naweza kujifanyia kitu kibaya. Two times this year nilichukua hatua kadhaa toward self suicide lakini nikaghairi na kuishia kutokwa na machozi, nilimfikiria mtu mmoja anayenipenda sana lakini hana namna ya kuweza kunisaidia. Nahisi nguvu kubwa inanivuta kwenye self suicide kwakuwa seriously sioni care wala love kutoka kwa watu wanaopaswa kunicare na mimi ni mzigo wao.

Lakini siyo makosa yao pengine wanahisi I'm strong to handle the situation by myself. Should I tell them I need more love and care from them than this how they take me for granted now? Masculinity feelings stops me. Nahisi mwanaume sitakiwi kuomba mtu anipende wala siwezi kulazimisha mtu anijali. Is this right? How can I change this attitude. I feel worthless hilo halipingiki na tatizo langu hasa ni kutambua hilo. How can I fix this? Haya mawazo yasije kuniletea brain tumor ni bora nikubali kushindwa, nikate tamaa lakini nawezaje? Nitaweza kweli kujitenga na kila kitu, kila mtu? Si ndo mwisho wa siku nitajua mimi .

Lakini nitaweza kweli kuassociate na society katika hali tofauti nikiwa mtu wa chini ninayehisi kupoteza thamani niliyokuwa nayo mwanzo ? Sipendi kuwa looser, well nimekuwa looser lakini sipendi kuonekana kama looser, sipendi kuwa worthless hivi. Dah, masikini mimi... Bora nikate tamaa!
#badmood #disabilityfeelings #poverty
Kabla hujafikisha miaka 20, ulikuwa ukisaidiwa, sasa unajitegemea. Ndio maisha yalivyo, endelea kuwa na matamanio, kitakachowezekana furahia, kitakachoshindikana kisikufanye ukate tamaa ya /na kutamani mengine, wala kisikupotezee muda kukilazimisha.
 
Dah kweli mkuu inawezekana naanza kuyumba stress zinaniendesha lakini najaribu tu kupunguza sumu pengine hata sijui kama nimeandika kutafuta msaada au nimeandika kwasababu gani mnisamehe bure kuwaandikia ujumbe mrefu usioeleweka
Daaah kwani maradhi yalikupata hayana tiba? Sijui kwanini najihisi kama nimeguswa sana na story yako. Kama yana tiba focus on kutibiwa kwanza na epuka sana mambo ya bwana anaweza and alike
 
Daah nakuelewa mkuu nimepita humo...... No one is coming to save u... Save urself tuliza kichwa usiwaze sana kukankwa urefubwa kamba yako kwa sasa kama ipo ipo tu usifos sana kingi utazidiwa na stress
 
Usipojieleza vizuri hakuna mtu atakayeweza kusaidia chochote.

Naona unazunguka zunguka tu.

Jibu swali la Compact kuhusu nini tatizo.
 
Maisha hayatakaa yatosheleze. Hivyo ni budi na kushukuru kwa ulichonacho. Those who are the happiest never did have everything, but they are thankful for everything they do have.

When you learn to appreciate the little you have, then the big things are soon to happen. Please learn to be grateful.

Anza kwa kushukuru na kufurahia pumzi uliyonayo, shukuru kwa amani, shukuru kwa kila kitu huku ukijilinganisha na wasio nacho kabisa na utapata amani ya moyo sana.

Then, lower or have less expectations from someone and you will never be disappointed. If you love someone, then don't expect to be loved back. If you give, don't expect the return. If you help, don't expect a thankful hand. On whatever you do to others, have no expectations. You will have peace within you.

Pole sana Da Vinci, Mondray. Paprika angekuwepo bila shaka ungekuwa na amani.
well said
 
Bwana Daviie kwanza pole na sio kwamba watu hawayapitii unayopitia wewe NO. Wanapitia ila katika muktadha tofauti ila sijui katika haya nitakayo kushauri lipo litakalo leta maana kwako lakini kwa upande wangu baada ya kuyaona haya ya uyaonayo wewe leo kupitia JF nilitafuta namna nini nifanye watu wamefanyaje au watu wanasemaje kuhusu Uvumilivu wengi ukisoma wanafanya yote ila wanasoma sana vitabu na Mimi nikasema ngoja nijaribu kusoma miongoni mwa watu walinishawishi kusoma vitabu huyo kijana umemtaja nikaanza kusoma sana vitabu wakati huu mambo Bado magumu na sio kwamba sasa yamefunguka lakini kuna tumaini na vitabu ambavyo hasa nimesoma na ningekushauri kwa hali yako na wewe wewe Soma labda kuna kitu utakipata kama nilivyopata
1. The Morning miracle hasa kwa hali yako
2. Magic/ secret cha Rhonder kama sijakosea
3.Think and Grow rich
4. The success principle cha Jack

Kwenye hivi vitabu vinaonyesha hatakiwi kukata tamaa na tena tunaweza kutatua yetu kwa Imani

Kwenye T&R kuna Mtu anaitwa Barnes yeye alicha Mgodi wa Dhahabu kwa vile tu haliona hapati anachotaka na akauza Mgodi kwa bei ya hasara ila mnunuzi alifanya Exploitation ndogo na akakutana nayo Bwana bana kutoka na lile alihapa lolote atakalo panga kufanya haijalishi Gumu kiasi gani ila hataacha mpaka apate matokeo
Hatutakiwi kukata tamaa kwa lile tunaloliamini japo haliwezi kuja kwa Urahisi kama tunatataji
 
Kuna mdau mmoja huku alichangia uzi wa kifo cha Ali Mufuruki kwa kusema nanukuu “Kuna nyakati maisha yanakosa maana”. Ni kweli kabisa maisha ni zaidi ya tunavyofikiria kama wanadamu kwa imani yangu. Maisha ya kila mtu yamepangwa kabla kabisa na Mungu. Baada ya wewe kutekeleza lile lililokuleta hapa duniani unaondoka. Hizi stori za kwamba nitafute pesa,nijenge nyumba nzuri ni mipango yetu sisi wanadamu ila kwa Mungu halipo hivyo. Pia sijui unatumia kipimo gani kusema wewe upo situation mbaya,kuna watu wako vibaya achaa. Ushauri acha kuona huishi mpaka upate pesa,shukuru Mungu kwa kila jambo,kwani hamna mwanadamu mwenye uwezo katika haya maisha zaidi yake
sawa nakubaliana na unachosema ila iko hivi, nilipofikisha miaka 20 nikapooza miguu mwaka 2014 mpk leo nipo ndani mlemavu haitoshi nikaanza kupata changamoto zingine za kiafya. Nimeishi siku zote nikivumilia matumaini yangu nitapona na dalili zilikuwepo lakini haijawa hivyo, nje na kesi ya ulemavu nikajaribu kuendesha biashara na mambo mengine mengi madogo madogo kwa kutumia watu wengine, almost kila kitu kinafeli thus why nikaona labda nisifanye tena chochote, nisiwe na malengo yoyote wala matumaini yoyote nibaki tu kujiuguza kwasababu ninapojipa matumaini na hakuna kinachofanikiwa siponi na mambo yote ni kama hayaendi sasa hii kitu inaumiza zaidi
 
Kabla hujafikisha miaka 20, ulikuwa ukisaidiwa, sasa unajitegemea. Ndio maisha yalivyo, endelea kuwa na matamanio, kitakachowezekana furahia, kitakachoshindikana kisikufanye upate tamaa ya nautamani mengine wala kisikupotezee muda kukilazimisha.
nilichokuwa nasaidiwa ni kusomeshwa na chakula lakini vitu vingine vingi niliachieve mwenyewe, the same same nilivyofanikisha zamani nilidhani nitafanikisha hata leo lakini sasa nimekuwa mgonjwa/mlemavu nipo tu ndani mambo yamebadilika
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Daaah kwani maradhi yalikupata hayana tiba? Sijui kwanini najihisi kama nimeguswa sana na story yako. Kama yana tiba focus on kutibiwa kwanza na epuka sana mambo ya bwana anaweza and alike
uti wa mgongo ulisinyaa (spinal stenosis), zikaja complications nyingine kibao viungo vikaanza kufeli. Labda nipate pesa nyingi sana nearly 50M ili nikajaribu kutibiwa nje ya nchi, uhakika wa kupona ni 50/50
 
Daah nakuelewa mkuu nimepita humo...... No one is coming to save u... Save urself tuliza kichwa usiwaze sana kukankwa urefubwa kamba yako kwa sasa kama ipo ipo tu usifos sana kingi utazidiwa na stress
Thanks mkuu nahisi umenielewa sana kuliko watu wengi, mimi nilizoea kuwa mtu wa kuforce kingi sasa hali ni tofauti ninavyoforce kingi mambo yaende na hayaendi hii inaniyumbisha zaidi naona labda nijaribu kuachana na hizi missions kibao nilizonazo kwa muda ili kujiokoa mwenyewe maana sometime napanick sana hadi natamani kujifanyia kitu kibaya, halafu nabaki kujiambia nakufaje kizembe hata sijafanya kitu cha maana duniani.
 
Never ever give it up, pigania unachokiamini kubadili mbinu za kufikia malengo toka zile zilishndwa awali n jambo la msingi pia, amini utatoboa katika hali zote bila kujali una hali gani sasa kwan wewe ni wa kipekee na una uwezo wa kutimiza uwazayo, fikiri tofauti kidogo tu
 
Yeah hebu pitia na thread zangu zilizopita utapata picha kamili
Pole saana mkuu, ila ni bora kushindana na wewe mwenyewe kuliko kushindana na mtu mwingine,

Namaanisha jaribu kupambana kuvuka mafanikio yako ya jana bila kuangalia jirani kafanikiwa vipi.

Watu wananjia zao ambazo huzijui so ukijaribu kuwaiga utaishia kuumia kila siku
 
Yesu yupi? Au yule mzungu mnayeweka picha zake kwenye magari na nyumba zenu?
Nauza ustaadhi akisalisha muumini wake hapo.
tapatalk_1575690240411.jpeg
 
sawa nakubaliana na unachosema ila iko hivi, nilipofikisha miaka 20 nikapooza miguu mwaka 2014 mpk leo nipo ndani mlemavu haitoshi nikaanza kupata changamoto zingine za kiafya. Nimeishi siku zote nikivumilia matumaini yangu nitapona na dalili zilikuwepo lakini haijawa hivyo, nje na kesi ya ulemavu nikajaribu kuendesha biashara na mambo mengine mengi madogo madogo kwa kutumia watu wengine, almost kila kitu kinafeli thus why nikaona labda nisifanye tena chochote, nisiwe na malengo yoyote wala matumaini yoyote nibaki tu kujiuguza kwasababu ninapojipa matumaini na hakuna kinachofanikiwa siponi na mambo yote ni kama hayaendi sasa hii kitu inaumiza zaidi
Usikate tamaa,kuna anko wangu mmoja alikuwa mlemavu Wa miguu kama wewe alizaliwa mzima baadae akapooza,alikuwa anafanya biashara zake kwa kuagiza watu na mambo yake yalikuwa yanaenda vizuri jaribu kutafuta watu sahihi wakukusaidia shughuli zako.
 
Thanks mkuu nahisi umenielewa sana kuliko watu wengi, mimi nilizoea kuwa mtu wa kuforce kingi sasa hali ni tofauti ninavyoforce kingi mambo yaende na hayaendi hii inaniyumbisha zaidi naona labda nijaribu kuachana na hizi missions kibao nilizonazo kwa muda ili kujiokoa mwenyewe maana sometime napanick sana hadi natamani kujifanyia kitu kibaya, halafu nabaki kujiambia nakufaje kizembe hata sijafanya kitu cha maana duniani.
Pamoja kaka hatuna tofauti sana me na wewe... Am still fucked up najifunza kupunguza mambo kichwani.....
unakua na plans nyingi na hakuna unachotimiza......

One step at a time.... Kuna muda unaloose motivation kabisa ya kufanya chochote bkoz huoni mwanga huko mbele.... Tuwe na amani tu ya moyo either we nake it or not
 
Back
Top Bottom