God bell
JF-Expert Member
- May 13, 2011
- 590
- 210
Wana Jf ni kisa cha ajabu. Mahali nipokuwa nafanya kazi nilikutana na dada 1 nikampenda, akanipenda nikawa naishi nae tukaendelea kufanya kazi. Mapenzi yakakolea nikazaa nae mtoto1 huku tukiwa tunaendelea na kazi. Cku 1 akaniambia anataka akasome kozi flani ili abadilishe kazi apate yenye maslahi kidogo. Nikamkubalia akaacha kazi akaenda kozi ya mwaka 1 akamaliza, shule alokuwa anasoma ilikuwa karibu na nyumban hivyo ckupata shida. akapata kazi World vision maslahi yakaanza kuwa mazir. Baada ya mda nikahamishwa kikaz nikawa nakuja nyumban baada ya mwez1. Tukaona tusiendelee kuishi kikapera bora twenda kwa wazazi ili tufunge ndoa. Wazaz wakatukubalia tukaanza mipango ya kufunga ndoa. Kazin kule nikaomba mchango nikapewa. Tukiwa kwenye process cku 1 cm yangu ikaita mtu akaniambia 'uctake kujua mm ni nani ila nakutaarifu tu kuwa mke wako ndo kaingizwa gest sasa hivi. Nikamjibu acha ujinga huo ni wivu.' wakati huo tayari tumeshaweka mambo sawa nikimaanisha, kitchen party tayari, send off tayari. Zikiwa zimebaki wiki 2 yule mtu akanipigia tena ananiambia 'njoo nyumbani ukashuhudie mke wako anavyofanywa'. Nikaondoka kimya kimya nikaenda nyumbani. Ckumwambia mke wangu chochote zaid ya kupanga mambo yetu ya ndoa itakavyokuwa cku hyo. Nakumbuka ilikuwa saa 12 mchana kesho yake nikiwa nikiwa nyumbani nikijua mke wangu yuko kazini yule mtu akanipigia akaniambia cku zote ulikuwa uhamini, sasa njoo gest flani ujionee mwenyewe. Nikaenda kufika pale nikambipu yule jamaa akajitokeza kumbe ni mtu na mfaham tunakaa nae mtaa1. Akaniambia 'nilishindwa kuvumilia hiki kitu sasa kaa hapa ujionee mwenye'. Maskini mke wangu namuona anatokea gest na njemba kubwa nisilolifaham. Nikamjibu jamaa 'asante kwa msaada wako' nikaondoka nikamchukua mtoto wangu nikampeleka kwa ndugu yangu nikamweleza yaliyonikuta nikaa huko kama masaa 4 nikiwa nimechanganyikiwa nalia tu. Kurudi nyumbani nikakuta ameshabeba nguo zake amekimbia. Nikakatiza kila kitu, hakuna haruc tena. Nakaziomba zile kamati za maandaliz ya haruc kurudisha michango ya watu. Ha nilipo ni mgonjwa wa kulazwa.