Bora kufa kuliko hivi!

God bell

JF-Expert Member
May 13, 2011
590
210
Wana Jf ni kisa cha ajabu. Mahali nipokuwa nafanya kazi nilikutana na dada 1 nikampenda, akanipenda nikawa naishi nae tukaendelea kufanya kazi. Mapenzi yakakolea nikazaa nae mtoto1 huku tukiwa tunaendelea na kazi. Cku 1 akaniambia anataka akasome kozi flani ili abadilishe kazi apate yenye maslahi kidogo. Nikamkubalia akaacha kazi akaenda kozi ya mwaka 1 akamaliza, shule alokuwa anasoma ilikuwa karibu na nyumban hivyo ckupata shida. akapata kazi World vision maslahi yakaanza kuwa mazir. Baada ya mda nikahamishwa kikaz nikawa nakuja nyumban baada ya mwez1. Tukaona tusiendelee kuishi kikapera bora twenda kwa wazazi ili tufunge ndoa. Wazaz wakatukubalia tukaanza mipango ya kufunga ndoa. Kazin kule nikaomba mchango nikapewa. Tukiwa kwenye process cku 1 cm yangu ikaita mtu akaniambia 'uctake kujua mm ni nani ila nakutaarifu tu kuwa mke wako ndo kaingizwa gest sasa hivi. Nikamjibu acha ujinga huo ni wivu.' wakati huo tayari tumeshaweka mambo sawa nikimaanisha, kitchen party tayari, send off tayari. Zikiwa zimebaki wiki 2 yule mtu akanipigia tena ananiambia 'njoo nyumbani ukashuhudie mke wako anavyofanywa'. Nikaondoka kimya kimya nikaenda nyumbani. Ckumwambia mke wangu chochote zaid ya kupanga mambo yetu ya ndoa itakavyokuwa cku hyo. Nakumbuka ilikuwa saa 12 mchana kesho yake nikiwa nikiwa nyumbani nikijua mke wangu yuko kazini yule mtu akanipigia akaniambia cku zote ulikuwa uhamini, sasa njoo gest flani ujionee mwenyewe. Nikaenda kufika pale nikambipu yule jamaa akajitokeza kumbe ni mtu na mfaham tunakaa nae mtaa1. Akaniambia 'nilishindwa kuvumilia hiki kitu sasa kaa hapa ujionee mwenye'. Maskini mke wangu namuona anatokea gest na njemba kubwa nisilolifaham. Nikamjibu jamaa 'asante kwa msaada wako' nikaondoka nikamchukua mtoto wangu nikampeleka kwa ndugu yangu nikamweleza yaliyonikuta nikaa huko kama masaa 4 nikiwa nimechanganyikiwa nalia tu. Kurudi nyumbani nikakuta ameshabeba nguo zake amekimbia. Nikakatiza kila kitu, hakuna haruc tena. Nakaziomba zile kamati za maandaliz ya haruc kurudisha michango ya watu. Ha nilipo ni mgonjwa wa kulazwa.
 
Pole ndg.
Kwanza kabisa mshukuru mungu kwa kumuumbua huyo mnafiki kabla ya ndoa kwani angekusumbua sana.
Pole sana.
 
Mungu alikuonyesha kabla ya ndoa hebu kamuangalie na huyo mtoto DNA may be kakaubambikia
 
Pole sana imenisikitisha sana, Usikate tamaa Yuko wako ulopangiwa na mungu na atakuja tu na utasahau hayo yote! Pole sana!
 
Pole ndg.
Kwanza kabisa mshukuru mungu kwa kumuumbua huyo mnafiki kabla ya ndoa kwani angekusumbua sana.
Pole sana.
Asante ndgu. Ndugu zake, wazazi wake wameona aibu hata kunipigia cm wameshindwa kwani alikokimbilia hajulikani manake baada ya tukio tu niwapa taarifa hadi nao wakachanganyikiwa kwan ilikuwa ni cku chache tu baada ya kulipa mahari.
 
You're so lucky bro. Kuna wengi bado hawajapata bahati ya kufahamu uhalisia wa wapenzi wao. Sahau na anza upya.
God bless you
 
pole sana kaka....sasa fundisho hapa na kwa wengini ni kwamba wanandoa/wachumba kuishi mbali mbali ni kujidanganya na kukaribisha majaribuni tuu!!!
 
wewe si bora ujamuoa ungekuwa umemuoa ungekufa kabisa ila pole sana mkuu..
 
Mungu alikuonyesha kabla ya ndoa hebu kamuangalie na huyo mtoto DNA may be kakaubambikia

huu ushauri utaleta hasara kwa mtoto acha tu mlee dogo coz shetani ni mama yake sio dogo.
 
pole sana kaka....sasa fundisho hapa na kwa wengini ni kwamba wanandoa/wachumba kuishi mbali mbali ni kujidanganya na kukaribisha majaribuni tuu!!!
Lakini ndugu tutaacha kufanya kazi mbali tukitafuta maisha kwa ajili ya mwanamke mpumbavu anaebomoa nyumba yake mwenyewe? Kwani alishindwa nn kuvumilia kama wanawake wengine ambao waume zao wako mbali na nyumbani jamani?
 
hiyo lugha ya' mkeo anavyofanywa'

ni mtu mzima so nafikiri 'amefanya'
 
Mkuu vumilia na ujue mungu alikuonyesha kabla vinginevyo usikute ungemdhuru huyo kiumbe pindi mngekuwa mmeshaoana
 
Ila mkuu usinichekesha, yaani unaona maisha yako hayana maana mpaka umefika mahali unaona bora ufe, mbona sikuelewi! Na huyo mwanamke sio rahisi tena kuolewa maeneo ya karibu na unakoishi. Muoaji atapopata taarifa zake ni lazima atakimbia kwa kasi ya Usain Bolt!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom