Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,214
- 3,587
Magazeti dada mawili ya The Citizen na Mwananchi yameripoti ukwepaji kodi wa kupindukia (Tzs.3.3 tr) huku tukikuza deni la taifa kwa kukopa hadi Mhimili wa Bunge unastuka. Magazeti haya yamejizolea sifa lukuki kwa uandishi wenye weledi.
Kauli ya Rais ni Sheria
Kaulimbiu ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake inaligharimu taifa na kuleta madaraja ya maisha (stations or life) yanayostawisha matabaka kwenye jamii.
Hivi sasa watu wanakula mlo mmoja maana unga umetinga 2000/ kg, maharagwe 4000/ kg, mchele wa gredi ya chini 3000/ kg, sukari tangu enzi ya Dr. Omar VP imeshinda awamu zote 4 kushusha bei.
Mafuta ya kula hivi sasa ni anasa, watu wanakula chukuchuku kwenye nchi inayolima mawese, pamba, mahindi, karanga, minazi, ina samaki na wanyama vyote hivyo vinatoa mafuta ya kula.
Nchi inaenda kwenye uchaguzi bila agenda. Vyama havina agenda ilhali wananchi wana agenda ambayo vyama haviioni.
Haiyumkiniki kwamba hata miradi ya kimkakati ya maendeleo imekwama kumalizika kuelekea 2025 licha ya ela iliyokopwa Tzs.42 tr ni zaidi ya thamani-jumla ya miradi yote mikubwa.
Znz kuna paa hadi umeme wanaopewa hauwatoshi wamelazimika kuomba waongezewe kiwango cha umeme.
Znz hiyo hiyo bei ya bidhaa na huduma zimebaki kuwa himilivu wkt bara uwezo wa mlaji kununua (purchasing power) umeanguka hadi kula mlo mmoja. Znz na Tz Bara ni nchi moja.