Boniface Wambura, naombeni msamaha

First Born

JF-Expert Member
Jul 11, 2011
5,310
1,473
Imesikika sauti ya Boniface Wambura afisa habari TFF, kwamba anawaomba radhi kwa kitendo cha umeme kukatika wakati wa utoaji wa zawadi, nina wasiwasi na huu msamaha. Lakini pia Sendeu Luis amewapa pole baadhi ya wachezaji wa Simba waliozimia baada ya kichapo juzi jumapili tar 4. July. Sasa wasiwasi wangu ni kwamba kama walisema watafanya uchunguzi ikiwa ni pamoja na Nchimbi kuunda kamati, afu leo wanasema samahani, hii inamaanisha nini? Kwamba tupotezee!
 
Ubalozi wa China umethibitisha kuna jenereta pale lenye uwezo wa kuwaka hata wiki kama MAFUTA YAMEWEKWA.Hapo kwenye mafuta ndio utata na haina haja ya uchunguzi 'PAKA AFUNGWE KENGELE'.
 
Ubalozi wa China umethibitisha kuna jenereta pale lenye uwezo wa kuwaka hata wiki kama MAFUTA YAMEWEKWA.Hapo kwenye mafuta ndio utata na haina haja ya uchunguzi 'PAKA AFUNGWE KENGELE'.
Nani atamfunga paka kengele?
 
Ile issue haihitaji tume wala ndugu yake. Kinachotakiwa wote wanaohusika na uwanja ule watimuliwe na ikibidi wapigwe faini. Sidhani kama TFF wanahusika ktk hili, lakini kilicho wazi ni kuwa kila mechi uwanja hupata % fulani ya mapato, sasa kama wasimamizi wa uwanja hawawezi kuhakikisha kuwa kuna umeme 24 hrs bila kujali dharura hawafai na wala tusijidanganye kuilaumu TFF. Wao nana madudu yao lkn siyo hili.
 
Back
Top Bottom