- Source #1
- View Source #1
JamiiCheck ni kweli kuwa BoniYai kahamia CHADEMA?
- Tunachokijua
- Madai
Julai 11, 2025 imezuka taarifa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii ikieleza kuwa mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Boniface Jacob amehamia CHAUMMA na kutangaza kugombea ubunge jimbo la Ubungo.
Taarifa hiyo imeambatana grafiki zenye utambulisho wa baadhi ya vyombo vya habari vya mtandaoni ikiwemo Jambo TV na Millard Ayo.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umebaini na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Hakuna ushahidi owte unaoonesha kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Pwani, Boniface Jacob ametangaza kuhamia CHAUMMA. Katika ukurasa wake wa X, July 11, 2025 amechapisha machapisho kadhaa yanayoashiria uwepo na kushirki katika shughuli za chama hicho ikiwemo kukosoa mwenendo wa kesi zinazomuhusu Mwenyekiti wao Taifa, Tundu Lissu.
Grafiki zinazotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi kwani zina baadhi ya mapungufu yanayozitafautisha na grafiki halisi za vyanzo hivyo yaani Jambo TV na Millard Ayo. Mbali na hayo grafiki hizo hazijachapishwa na vyanzo hivyo.
Boniface kupitia ukurasa wake wa X amekanusha pia Taarifa hizo kwa kuandika;
"EPUKA MATAPELI
EPUKA MATAPELI
EPUKA MATAPELI
MATAPELI wakiandika vipeperushi feki kama hivi ujue Serikali au CCM inataka kutapeliwa na wahuni...!
Nipo CHADEMA na nitaendelea kuwa CHADEMA.
Kwa sasa tunapigania REFORMS na Mwenyekiti wetu Tundu Lissu awe huru arudi uraiani kuendeleza mapambano."