Bongo Movies na wanafunzi wa Kibongo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo Movies na wanafunzi wa Kibongo

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Manyanza, Jun 4, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Jun 4, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wana JF
  kuna member siku za nyuma alishawahi kuleta thread inayohusu kipindi cha Skonga kinachoonyeshwa EATV (Channel 5) ni kipindi kinachofurahisha, elimisha na kuchangamsha sana
  naweza nikasema na mimi nimelazimika kuja na thread ambayo inaweza ikawa imefanana na member mwanzangu.
  Jana nilikuwa naangalia kipindi cha Skonga, muendesha kipindi Allan
  akamuuliza swali mwanafunzi mmoja wa kike ni kitu gani anachopendelea? mwanafunzi akajibu kuangalia Movies
  akaulizwa swali jingine ni movie gani inayozungumzia Maisha ya Idd Amini Dikteta aliyewahi kutawala Nchi ya Uganda, Mwanafunzi akajibu MISUKOSUKO"(MISUKOSUKO ni movie ya Kibongo), Presenter akabaki kinywa wazi akamuuliza nani kacheza Badi" kwa waliokiangalia kipindi walijionea mengi. (jina sahihi la movie ni THE LAST KING OF SCOTLAND)
  lakini lengo langu ni hapo kwa huyo mwanafunzi kusema ni Mpenzi wa Movies halafu Movie zenyewe za Kibongo,
  wadau naomba tusaidiane kwa hili hivi Movie za kibongo zinamsaidiaje au zinamwelimishaje Kijana wa Kitanzania katika Dunia ya sasa??
  hivi hata kama ni wewe unaweza ukasimama mbele za watu tena kwenye television kama Channel 5 na kusema ni shabiki wa Bongo Movies???
  yawezekana jibu likawa ndio/hapana!
  Movies za kibongo zina maudhui gani katika ulimwengu wa kisasa?
  ni zinamjenga vipi kijana ambae anajiandaa kuwa mtu mzima?
  Asanteni!!!
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Wewe huwa unaangalia movies za kibongo au huangalii?
   
 3. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Siangalii!!
   
 4. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Bongo hakuna 'movie' kuna 'video'. Tafauti sana hivi vitu
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Jun 6, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  sasa kama huangalii inakuwaje unaziponda na unasema hazina mafundisho?
   
 6. Good Guy

  Good Guy JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 4,511
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kweli bhana,huyu atakua hajaona ile ya Aunt,Binti kikojozi inamaudhui mengi sana,na ni ya maadili mno,am i wrong! LOL
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,025
  Likes Received: 3,051
  Trophy Points: 280
  Kwanza wanafunzi kuwa busy na muvi si utani inalamba kwao
  pili ukimuuliza kajifunza nini (meseji) kwenye muvi flani hawezi kuelezea
  tatu hizi bongo muvi ambazo 80% ni vichupi,ngono na uzandiki kimaadili mtoto anagrasp nini mle...anywy,if something can possibly,go wrong it will go wrong!
   
 8. m

  mcndimbo New Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  naaangalia sana muviz na za kibongo pia naangalia...ukizungumzia muvi za kibongo unazungumzia muvi za kiafrika...muvi mara nyingi huakisi maisha halisi ya watu wa jamii husika...wazungu jamii zao kwa upana wako busy na mambo ya maendeleo ya sayansi na teknolojia...muvi zao utaona zina-reflect uhalisia ule...hata kama ni sinema ya wizi,basi wizi ule unakua wa kutumia teknolojia ya hali ya juu pia...muvi nyingi za kiafrika zinaakisi maisha ya kiafrika pia....nyingi ni habari za kifamilia na makandokando yake...angalia muviz za Nigeria na Ghana...South Africa na Botswana...ayo ndio maisha yao....ukitaka kujua maisha ya jamii fulani....muviz zinazungumza mengi sana...kusema KAZI FULANI YA SANAA HAINA MAFUNDISHO ni ngumu sana....usiangalie muvi na huku ukitaka ifundishe kitu fulani...angalia muvi ili ujiulize mwandishi alikua ana fikra gani...yawezekana kweli zinaonesha wasichana na vichupi ila je katika uhalisia hao wanawake humu mitaani hawavai nguo hizo? muvi imeonesha athari za vichupi au zimeshabikia? hata huko ulaya na India kuna muvi nzuri na mbaya na Bongo vivo ivo...Indian muviz za sasa zina umarekani mwiiiingi na maa-actors wa zamani kama kina Amittha Bachan wanapiga kelele kila kukicha....na Bongo vivo ivo...suala la athari za utamaduni wa kimagharibi ni suala MTAMBUKA na halipo katika muviz tu....meeen angalia muviz za kibongo...kuna maisha meeeeengi ya wabongo usioyajua,,,,,,,jifunze na ukemee hali io katika jamii na sio kusema Muvi za kiboooongo...MUVI ZA KIBONGO ZINA-REFLECT MAISHA YA KIBONGO :confused2:
   
 9. C

  Cremo joe joe Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Jun 5, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hzo movie zenu me zinantia hashk 2. Na kunifanya nimwaze mbeibe wang.
   
Loading...