computer engineer
Member
- Mar 26, 2018
- 76
- 38
Habari wana JF leo nimeona nitoe ya moyoni mwangu kuhusu Bongo Movie. Kumekua na matusi mengi na malalamiko mengi sana kuwa Bongo Movie hamna kitu na watu hawapendi kutazama Bongo movie. Mm nachopenda kusema hapa ni kwamba vipaji vipo na watu wana uwezo japo kweli wapo wazinguaji lakin wazuri wapo kama kina hemed, gabo, mlela, hisan muya, bad boy. wema, wolper, jenifer kyaka, na wengineo wengi sana. Na pia kwa. upande wa uandishi wa stories of coz wapo waandishi wazuri tuu hapa bongo.
Sasa Twende kwenye vikwazo vikubwa vya tasnia hii ambavyo vinafanya watu wengi waone kama Bongo movie wazinguaji, kwa muono wangu mimi, kitu kikubwa sana ni budget na kitu cha pili ambacho pia kinaweza kuwa ndani ya budget ni Utaalam katika Movie production hapa tunazungumzia utaalam wa best softwares katika video editing, grapgics desigingna production kiujumla
Suala la Bajeti au Pesa, hapa kiukweli ni tatizo kubwa sana hili, katika uandaaji wa movie zetu za kibongo kiukweli kuna ufinyu wa pesa mkubwa. hii ndio hupelekea igizo kupunguza baadhi ya mambo ambayo mwandishi aa stori ameweka ili waendane na bajeti iliyopo na pia hata mazingira (setting) kuibadilisha yaani kutokuendana na mwandishi wa stori kwa sababu ya bajet finyu. Mbali na setting pia kuna ishu kama za mavazi, kutokana na ufinyu wa bajet unakuta kila mtu anavaa nguo zake tuu ambazo zingine haziendani na scene aliyocheza, Mfano kuna movie moja nimeiangalia unakuta mtu amecheza nafas ya Ugaidi, lakin for sure muonekano wake hauridhishi kwa sabab amavaa katisheti fulani yani kiujumla haileti uhalisia kabisa hiyo ni kwamba muandaaju hana bajet nzuri kiasi kwamba anashindwa kudesidn clothing style ya characters wake. Kwa hiyo katika bajeti ni tatzo kubwa sana hasa kwa movie ambazo zipo katika maudhui ya mambo ya watu wenye fedha na maisha mazuri au watu wenye nafas kubwa serikalin. Angalau zile za kuonyesha utamaduni wetu japo nazo bado kuna tatzizo hili la bajeti.
Tatizo la wataalamu, kiukweli nimewahi kutazama uandaaji wa movie ya Avatar, hiyo movie ukiangaalia wanavoindaa na ukiangalia ilipokamilika huwez amini kabisa utakuta kuna mchango mkubwa sana wa teknolojia hasa ya kubadilisha muonekano wa wale characters na matukio. Hapa kwetu bado hatuna wataalamu wengi wenye kujua kwa weledi hayo mambo japo wapo wanaofanya lakin hawawez kufika huko, na labda kitu kingine tunaweza kurudi kwenye bajet tena maana kuna vifaa ambavyo pia inatakiwa hawa wataalamu wetu wa upande wa cameras na editing za video na graphics designing hawana, kwahiyo ndomaana movie zetu zitazido kufunikwa na movoe za kutoka nje kama za kikorea. laiti kama bajeti ingekuepo ni rahisi kutafuta wajuzi wa haya mambo na kuwaajiri katika kampuni zetu za film production na kuweka vifaa vyote
Maoni yangu, kwa vikwazo hivo nadhani kitu kikubwa ambachi unatakiwa kifanyike ni kwamba watu wenye pesa za kutosha kabisa wakiinvest katika movie na wakaamua kufanya mambo makubwa kiukwel tunaweza kufika mbali sana katika tasnia hii na pia ifanyike scholarship za watu kwenda nje kwenda kusomea uaandaaji wa movie tuu naamini hawa wataalam wakirud na wakakuta kuna investment nzurii katika movies basi kutakua na changes kubwa sana. Bongo movie kuna vipaji ila for sure kuna watu wanaharibu mambo kwani hawawezi kuigiza na wanajifanya waigizaji hawa ndo ambao wanafanya bongo movie ionekane sio kitu.