Bongo movie kukosa uwakilishi mpana unaidumuza tasnia, uswahili na u-Dar ni mwingi kupitiliza.

NAONA MOJA YA SBB YA KUSHINDWA KUINUKA KWA HIYO SANAA NI
UKOSEFU WA MGAWANYO WA KAZI, MAJUKUMU NA UKOSEFU WA UTAFITI.
MTU MMOJA NAWEZA KUWA NDIO:

  • MTUNZI
  • MUONGOZAJI/DIRECTOR
  • MZALISHAJI/PRODUCER
  • SOUND PRODUCER
  • PRINCIPAL CAST
  • EDITOR
  • MUSIC EDITOR
  • CAMERA AND LIGHTING
  • MAPAMBO NA UREMBO
  • LOCATION MANAGER
  • TRANSPORT OFFICER
  • MWEKA HAZINA!
😅
 
Vijana wa mikoani acheni kulalamika bila vitendo.....Anza wewe kufanya hayo mabadiliko.
 
Hapana, si kweli, shida ni CCM.

Setting ya kila kitu hapa Tanzania haiko sawa maana kila kitu kiko kwenye mlengo wa kisiasa.
 
Sababu mojawapo tasnia ya bongo movie imekuwa dumavu, mbovu na isiyofanya vizuri kwa muda wote tangu nchi ipate uhuru inaweza kuwa ni kutokana na kutawaliwa na watu/waigizaji wa pwani na kusini zaidi. Upande wa maudhui na mazingira ni hivyo hivyo pia, ni ya kipwani, Kusini na Uswahili zaidi.

Kinachotakiwa sasa ni wadau wafanye jitihada binafsi kuifanya sekta hiyo kuwa jumuishi zaidi na yenye uwakilishi mpana kwa kuhakikisha watu wa jamii nyingi tofauti zaidi kama Wahaya, Wasukuma, Wakuria, Wambulu, Wamasai, Wanyakyusa, Wasafwa, Wakinga n.k wanashiriki katika kuigiza bongo movie ili kutanua wigo wake, kuvutia watu wengi zaidi na kuongeza ubunifu na tija.

Pia wajaribu kufanyia kazi zao katika mazingira tofauti na ya Dar au pwani. Nchi kubwa kama hii ni ujuha kazi zote za bongo movie kuigizia mazingira ya ki'Dar es Salaam na Kipwani tu. Igizieni hata huko Katavi, Mbeya, Arusha, Kigoma, Mbeya, Mara, Mwanza.
Unakumbuka kina saradini, wale wangeendelea wangekua mbali sana, support tu ilikosekana. Nadhan hata shumileta na nsyuka hazikua za dar
 
Kuna chaneli moja nilikua naifuatilia YouTube kipindi cha nyuma siikumbuki jina lake,ila ilikua inaonesha movies za wasanii wa Morogoro,wanajitahidi sana kuanzia acting,stori, location nzuri, quality ya picha inaonekana ilikua na producers na directors wazuri,haya Kuna movies zingine tatu ziliigiziwa sijui ni mkoa gani ila waliohusika ni wale wazungu waliotengeneza tamthilia ya Siri ya mtungi, zinaitwa hadithi za kumekucha "Fatuma",bahasha,hadithi za kumekucha "Tunu" ni nzuri kupitiliza.Kitu ambacho bongo movies wanakosea sio tu ufinyu wa bajeti hapana ila hata kuchagua waigizaji wazuri hawana kipaji hicho cha kuwajua, directors na producers hawajifunzi vitu vipya kulingana na wakati,wengi wanatoa kazi ili wapate pesa tu.
 
Back
Top Bottom