kaka mi naomba kuuliza kwani Original maana yake nini. mi nafikiri kwenye swala la Jezi neno Original ni "Irrelevant" word. mfano simba au Yanga wakiamua wawe wanachapisha jez watakazovaa wachezaji hapa hapa Bongo kutoka kiwanda cha kanga kile cha mbagala wakatumia malighafi za kamba za katani.
na wakaamua waanze kuziuza hizo jezi shilingi 5000. na wewe ukaamua kununua jezi yenye mfanano ule ule kama wa jezi ya simba au yanga. ila ww ukanunua ya Ulaya iliotengenezwa kwa pamba Grade A. jezi yako itakuwa FAKE na alienunua ile iliotengenezwa kwa katani mbagala inayouzwa na Simba au Yanga hiyo itakuwa OG. maana ndio hiyo wanayovaa wachezaji bila kujali ubora.
mfano chukua jezi halisi iliovaliwa na mathalani England wakati wanachukua Kombe la Dunia 1966. mtu akitengeneza jezi kama ile sasa hivi haijalishi ataitoa ya Ubora gani. ila itabaki Fake kwa kuwa sio halisi iliovaliwa na timu kipindi kile. ingawa inawezekana Quality ni mbovu kuliko itakayotolewa sasa hv.
nafikiria ungesema Jezi zetu QUALITY ni mbovu kwa maana imetengenezwa chini ya kiwango. ila sio fake maana ukisema fake inamaana hiyo OG inatoka wapi na inavaliwa na nani. ikiwa hiyo unayooita fake ndio hiyo wanazovaa wachezaji
NAJARIBU KUWAZA KWA SAUTI TU