Kifo hakitibiki na mauti hayana dawa ndugu zangu,kifo cha huu mziki unaitwa bigji kpo na ipo siku utakufa tu...wanasaidia nini zaidi ya kuwaharibu wanetu kifikra?eti kioo cha jamii,sharobaro awe kioo wa nani..nauliza awe role model wa nani?wafe kabisa wala sitaki kuwaskia
Ndoto za Mchana!!!
Kila zama na mambo yao...kwa vijana wa kileo, mambo yao ni bongo fleva..hata kama unaona haikufunzi kitu, ni wewe...wenyewe inawafunza na wanao role models wao..tazama kama mnyoo wao wa kiduku jinsi ulivyobamba...all over sasa ni kiduku mpaka ma-footballer wa Europe ni hivyo hivyo...ndiyo zama zao hizi kaka...kama nyinyi mlivyokuwa na zenu za panky, denge n.k.
We kama hutaki kuwasikia basi kufa na kijiba chako cha roho...wapo, na wataendelea kuwapo...Alianza Saleh Jabir kwenye early 1990s akiimba kwa mabiti ya uzunguni na america, wakati huo tulidhani hizo ni tafsiri za nyimbo za kimarekani kumbe ni instrumental ikatiwa mashairi ya kiswahili...kama unaikumbuka OPP(naughty By nature) n.k.
Muziki ukakua(call it evolution) pale studio za kutengeneza music kwa computers zilipoanza...wakati huo wengine wakajiita wana-hip hop(Rap) na majina kama walume ndago, wagumu nk yakawa ni common, hip hop ilipoonekana kufikia saturation, vijana wakabuni mchanganyiko wa hip hop na kuimba(hapo ukawaona kina juma nature wakiimba lakini kiugumu ugumu bila kubana pua), vijana walipogundua kubana pua kuna ladha yake wakaanza kubana pua one-way mpaka leo tuna akina Diamond ukipenda muite Platinum, wabana pua mahiri, Ally Ulaya(Kiba), Barnaba nk...
kwa ujumla ni kuwa muziki ni utamaduni, na ilivyo kila utamaduni una watu wake..ili utamaduni huo ufe ni mpaka pale wenye-utamaduni huo watakapotoweka na bahati mbaya kwako ndugu ni kuwa hilo halitotokea kwa sababu tu wewe na wengine wenye mawazo mafupi kama yako mngetamani litokee...POLE!!!
Nawasilisha!!!