Nakurekebisha kidogo, kweli Sheria hutu gwa na bunge. Lakini bunge halitungi sheria muuza nguo dukani alipe sh ngapi. TRA wao kutumia taalumayao ndio wana kazi ya kutafsiri Sheria
Kwenye kutafsiri ndio hapo inaonekana kuna tatizo, maana Kuna muuza nguo dukani anatozwa mfano mil 2 kwa mwaka. Alafu Kuna muuza nguo mwingine mwenye duka mwingine anatozwa laki 4
Ukadiriaji kod huwa unafanyika kwa macho, alafu mtu wa TRA ndio anasema unatakiwa kulipa kiasi gani. Hapa ndio kuna wale wasio waaminifu huomba rushwa ili kukadiria kidogo
Sio yote wayafanyayo hawa watumishi huwa ni kosa la taasisi bali huwa ni kosa la mmoja mmoja ndio maana wengine huchukuliwa hatua.