Bomu laua watoto 7 Karagwe, Kagera | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu laua watoto 7 Karagwe, Kagera

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kajunju, Oct 30, 2012.

 1. k

  kajunju JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 986
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 45
  Habari nilizozipata punde toka karagwe ni kuwa, bomu limeua watoto 7 kijiji cha Ihanda maeneo ya Bugene. Bomu hilo liliuzwa kwenye vyuma chakavu. Leo ndipo walikuwa wanapima mzigo ili ununuliwe.

  Watoto waliokufa ni wa familia 3 tofauti.

  Habari hizi ni za uhakika kwani nimepigiwa na jamaa yuko eneo la tukio.

  Nawasilisha

  #########
  UPDATE:

  JUMATANO, OCTOBA 31, 2012 | NA RENATHA KIPAKA, KARAGWE | Mtanzania

  *Lilikuwa kwenye vyuma chakavu, lawasambaratisha vibaya
  *Wamo wanne wa familia moja, ni vilio na huzuni tupu Karagwe


  WATU saba katika Kijiji cha Rugarama kata ya Ihanda Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, wamefariki dunia baada ya kulipukiwa na kitu kinachofiwa kuwa ni bomu la kurushwa kwa mkono.

  Taarifa zilizotolewa na Jeshi la Polisi wilayani Karagwe jana, zinasema kati ya watu wanne ni wafamilia moja.

  Tukio hilo la kusikitisha, lilitokea jana saa 4 asubuhi, wakati watu hao wakiwamo watoto wadogo walipokuwa wakiokota vyuma chakavu.

  Waliofariki katika tukio hilo na umri wao kwenye mabano ni Eladius Robert (15),Fenius Frank (3), Faraja Frank (1), Scatus Kamali (15), Nelson Alphonce (14), Edger Gidion (14) na mmoja wao ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja, lakini anakisiwa kuwa na umri wa miaka 17.

  Taarifa hizo, zilidai watoto hao walilipukiwa na bomu wakati wakiokota vyuma chakavu kwa ajili ya kwenda kuviuza.

  Mmoja wa wazazi ambaye amepoteza Frank Robert (35),alisema wakati watoto hao wakiokota vyuma hivyo, ghafla alisikia mlipuko mkubwa ambao hakufahamu ulitokana na nini.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, ambayo awali ilikuwa wilaya moja na Karagwe Luteni Kanali Benedict Kitenga alikiri kutokea kwa vifo hivyo.

  Luteni Kanali Kitenga ambaye ni mtaalam wa kulipua mabomu, alisema vifo hivyo vinahofiwa kusababishwa na bomu la kutupwa kwa mkono.

  "Tukio hili limetokea wakati watoto na watu wazima, wakiota vyuma chakavu, ghafla kulitokea mlipuko mkubwa wa bomu na kuwauawa hapo hapo,"alisema.

  Kutokana na tukio hilo, Luteni Kanali huyo aliwashauri wakazi wa wilaya hiyo kuwa watulivu wakati huu ambao Serikali ikiendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

  Pia aliwaonya wananchi kuacha tabia ya kupokea wageni, wasiowafahamu ambao hufika vijijini na kuwataka wawasaidia kuokota vyuma chakavu.

  Alisema wilaya hizo, zinapakana na nchi nyingi za Rwanda, Burundi, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),hivyo kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa watu ambao hawawataki mema.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuahidi kutoa ufafanuzi zaidi leo.
   
 2. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #2
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,911
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Habari ya kusikitisha sana, pumzikeni kwa amani watoto,poleni wafiwa
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Haya mabomu yanayozagaa hovyo yanatoka wapi? R.I.P WATOTO
   
 4. C

  Campana JF-Expert Member

  #4
  Oct 30, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Katika azma ya kutimiza wito wa kujiajiri, watoto wakiwa ktk kuokota/kukusanya vyuma chakavu wamelipukiwa na bomu asubuhi ya leo. Hii imetokea katika kijiji cha Ihanda Karagwe. Inahofiwa kuwa 6 kati yao wamepoteza maisha. Watoto hawa walihitimu darasa la saba mwaka huu. Wwalioko Kagera wanaweza kufuatilia habari hii kwa undani.
   
 5. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Endelea kuleta Kiburi Mama Joyce Banda, tena ikiwezekana urushe mabomu kama watu walivyozusha juzijuzi naona huku tuna silaha mpaka zinatulipukia hatuna pakuzipeleka, silaha zetu wenyewe zinatumaliza kila kukicha! Komaa Mama Banda utusaidie wenzio huku.
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,349
  Likes Received: 19,530
  Trophy Points: 280
  vita vya kagera...
   
 7. M

  Mtoto wa tembo Senior Member

  #7
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 4, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  So sad....poleni wafiwa na jamaa kwa ujumla.
   
 8. M

  Mundu JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Inasikitisha sana...
   
 9. K

  Katufu JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 433
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Jaman poleni kwa wafiwa. Hii biashara ya chuma chakavu inabidi iwekewe mwongozo sasa maana itataketaza watu wengi na pengine kuharibu miundombinu yetu kama mifuniko ya majitaka inavyoibiwa
   
 10. cacico

  cacico JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 8,392
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Whhaaaaattttt! Poleni wazazi, rip watoto!! Awamu ya nne, full mikosi!
   
 11. Mwiyuzi

  Mwiyuzi JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2012
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 861
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 80
  UAMUSHO hawajahusika katika hili kweli?
   
 12. a

  ambagae JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 1,655
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Poleni wafiwa na Mungu aziweke mahali pema roho za Marehemu
   
 13. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,733
  Likes Received: 354
  Trophy Points: 180
  Kuna uwezekano nchi hii kukawa na mabomu mengi sana yaliyoachwa nyakati za vita. Nasema hivyo kwa kuwa, kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, leo asubuhi nilipata habari kupitia BBC juu ya kufungwa kwa uwanja wa ndege wa Japan kutokana na kupatikana kwa bomu lililoachwa wakati wa vita ya pili ya dunia.
   
 14. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  mungu alaze roho za marehemu pema peponi,serikali iangalie sana hii biashara ya vyuma chakavu,iliwa tokea dar lakin bomu alikulipuka
   
 15. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,047
  Likes Received: 3,080
  Trophy Points: 280
  Mkuu mbona umeingilia habari
   
 16. mbota

  mbota JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 742
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 60
  Mungu wewe ni mwema wakati wote. WALAZWE PEMA PEPONI AMEN
   
 17. Goheki

  Goheki JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2012
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 270
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hapa sijui tumlaumu nani?poleni wafia na Mungu awape pumziko la milele.
   
 18. K

  Kamarada Senior Member

  #18
  Oct 30, 2012
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  So SAD news...may God R.I.P hao wapendwa wote. Mungu awape faraja wazazi, ndg na jamaa wote.
   
 19. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  nashauri sua wapeleke panya wao maeneo kama haya hasa ya mipakani, kwani vita ya burundi, rwanda, congo drc, na vile vya uganda lazima vinaacha masalia hatari kama haya, sasa kuliko kukazania kuwapeleka huko angola, sijui msumbiji na wapi, bora tuanzie maeneo kama haya. "charity begins at home"
  poleni bana ndungu zetu wa bhukobha kule kwa kina rwebhangira, na rugaiyumukamu
   
 20. a

  awuyegani Senior Member

  #20
  Oct 30, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 147
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  R.I.P WATOTO. Hii nchi babomu nje nje.
   
Loading...