nashauri sua wapeleke panya wao maeneo kama haya hasa ya mipakani, kwani vita ya burundi, rwanda, congo drc, na vile vya uganda lazima vinaacha masalia hatari kama haya, sasa kuliko kukazania kuwapeleka huko angola, sijui msumbiji na wapi, bora tuanzie maeneo kama haya. "charity begins at home"
poleni bana ndungu zetu wa bhukobha kule kwa kina rwebhangira, na rugaiyumukamu
Habari nilizozipata punde toka karagwe ni kuwa, bomu limeua watoto 7 kijiji cha Ihanda maeneo ya Bugene. Bomu hilo liliuzwa kwenye vyuma chakavu. Leo ndipo walikuwa wanapima mzigo ili ununuliwe.
Watoto waliokufa ni wa familia 3 tofauti.
Habari hizi ni za uhakika kwani nimepigiwa na jamaa yuko eneo la tukio.
Nawasilisha
update: Watoto waliokufa na family zao ni: robert kapoteza watoto 2, alfonce kapoteza mtoto mmoja, prim kapoteza mtoto 1<mjukuu wake>,sili kamali kapoteza mtoto 1. Jumla waliokufa ni 5 na mmoja kakatika miguu,bado hajafa ila hali mbaya. Taarifa hiz nimepewa na mwl wa ihanda p/school
hivi huwa hayana ku-expire!!vita vya kagera...