Binti Asnat Philbert atwaa taji la Miss Karagwe 2026

Binti Asnat Philbert atwaa taji la Miss Karagwe 2026

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,315
Reaction score
15,804
WhatsApp Image 2026-09-29 at 08.56.49.jpeg
Binti Asnat Philbert ametwaa taji la Miss Karagwe 2026 katika shindano lililofanyika usiku wa kuamkia Septemba 27, 2026, chini ya maandalizi ya The Boom Vibe.

Asnat mzaliwa wa Kata Kayanga alifanikiwa kuwashinda washiriki wenzake, katika shindano lililowakutanisha jumla ya warembo nane wakiwemo washiriki watano kutoka Karagwe na watatu kutoka Wilaya ya Kyerwa.
WhatsApp Image 2026-09-29 at e.jpeg

rr.jpeg

Ushindi huo unamuweka Asnat katika nafasi ya kuiwakilisha Karagwe kuelekea hatua inayofuata ya mashindano ya urembo ya Miss Kagera 2026, yanayotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa baada ya shindano hilo, washindi watatu bora kutoka katika mashindano hayo wataungana na washindi kutoka wilaya nyingine za Mkoa wa Kagera, kwa ajili ya kushiriki katika tamasha la Miss Kagera 2026.
 
Hizi burudan zingine aisee,mbona ni ujinga sana!
Watu huwa wanaburudika na nini hasa kwenye huu umiss?
 
Hizi burudan zingine aisee,mbona ni ujinga sana!
Watu huwa wanaburudika na nini hasa kwenye huu umiss?
Mkuu, mambo yao waachie wenyewe. Duniani kuna watu 7B+, interest haziwezi kufanana.

Yajue ya kuzingatia, ili uachane na yasiyokuhusu.

Let them be, utaishi maisha ya Furaha sana.
 
Back
Top Bottom