mkuu meningitis nimefuatilia thread yako from begining mpaka mwisho, you are a great thinker.
nimekuja kugundua wanaoupinga ukweli unaoongea ni wale wale waliotoka vyuo vya kata, na ukweli unaoongea hawawezi kukubaliana nao, its common sense kwamba hawawezi discredit vyuo walivyosoma coz wataonekana vilaza ila ukweli wanaujua kimya kimya.
muhas will still and always stand the best..
Ni kawaida ya mtanzania kujidai anaweza na kujua kila kitu!
Hawafahamu kuwa maisha bila changamoto yangekuwa mafupi na yanayoboa!
Hawajui kuwa hata pale MUHAS tuliwahi kuwaeleza juu ya athari za kudahili wanafunzi wengi kulinganisha na resources zilizopo.
Ni muhimu sana kukubali ukweli,kujitathimini na kuweka mikakati ya kutatua changamoto ulizonazo ...poor insight inahitaji insight orientation,kwangu mimi hawa wabishi wasiokubali ukweli wanahitaji kushawishiwa na kufundishwa kuukubali ukweli hata uwe mchungu kiasi gani ndipo hatimaye tuwape mbinu za kupambana na ugonjwa walionao au tuseme mbinu za kutegua hayo mabomu.
Watu hawataki kabisa kuuchukua ujumbe muhimu kwamba
Serikali inataka kuongeza idadi ya wavaaji makoti na stethoscope kwenye mahospitali bila kujali wamewiva kuchukua jukumu hilo adhimu.mwisho wa siku tunarudi kuhamaki ooh madaktari wala rushwa,manesi wana roho mbaya na malalamiko kama hayo.
Wenzetu wa uingereza wamejikita katika kuboresha maslahi na usimamizi mkali katika sekta ya afya....yaani wameweka mshahara mnono kwa watumishi wa sekta ya afya na hivyo hawahitaji sana kutoa ufadhili wa kusomesha wanafunzi katika vyuo vikuu.Lakini wameweka regulations ngumu waweza sema wako conservative ili kuzuia makapi au wale wa vyuo vya kata wasiingie kuchachua sekta ya afya.
Hapo tusije kusingizia eti uingereza wameendelea ndio maana wanafanya hivyo..bali inatakiwa kuiga hayo kwani matokeo yake ni kuwa na mfumo imara wa afya.
Kwa kuruhusu makapi yaingie kwenye sekta ya afya au hata elimu bado tutaendelea kulibeba tatizo...yaani baada ya miaka kumi na ushehe utahitaji kubadilisha mfumo mzima!
Ushauri wangu kwa serukali ni mmoja tu ...kwamba iweke maslahi mazuri kwa sekta ya afya au hata elimu,itoe sponsorship kwa wale waliofaulu kikwelikweli ili vijana walioko sekondari waongeze bidii kwenye masomo ya sayansi.
Haiwezekani watanzania wote tukawa na uwezo wa masomo ya sayansi,haiwezekani wote walioko kwenye field ya afya tukawa madaktari au maspecialists,ni lazima kuwe na mgawanyiko na kila mtu akiwa vizuri katika kada yake tutafika.
Serikali ni lazima iwe kali,vyombo kama MCT,MAT,PHARMACY COUNCIL ni lazima viamke na kupata meno ya kuuma kwani katika dunia hii ya kijasiliamali si tu ma.gabachori bali hata wachaga,wakinga,wasukumu yaani kwa ujumla kila mtu anatazama fursa ya kuingiza kipato bila kujali madhara atakayosababisha katika jamii.kila mtu anataka kufungua hospitali,chuo cha afya au duka la dawa,sasa tukiacha mambo haya yakiendelea bila kuyasemea ndio mabomu haya yanayotulipukia.