Bomu la CHADEMA kwa Pinda hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bomu la CHADEMA kwa Pinda hadharani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 17, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,591
  Likes Received: 82,147
  Trophy Points: 280
  Bomu la CHADEMA kwa Pinda hadharani

  Mwandishi Wetu
  RAIA MWEMA
  Februari 16, 2011
  [​IMG]Polisi wamchuuza kwa taarifa zao

  [​IMG]Mbunge Lema awasilisha hoja 10


  [​IMG]Spika ataka iwe kwa maandishi


  SAKATA la vurugu na mauaji yaliyotokana na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Arusha linaelekea kumuelemea Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Hiyo inatokana na taarifa ya kuwa kauli ya Waziri Mkuu Pinda ya wiki iliyopita iliyokituhumu CHADEMA kuhusika na vurugu hizo zilizoishia katika mauaji ya watu watatu, ilitokana na maoni ya Polisi ambao katika matukio hayo wao ni watuhumiwa.
  Baada ya Pinda kutoa taarifa kuhusu tukio la Arusha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, aliomba Mwongozo wa Spika, akitaka kujua mbunge anaweza kufanya nini akibaini ya kuwa “kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya Taifa na Bunge ”.
  Baada ya kuomba Mwongozo wa Spika, Spika Anne Makinda, alimtaka Lema kuwasilisha bungeni ushahidi wa “uongo wa Waziri Mkuu”, ifikapo juzi Jumatatu.
  Hata hivyo ilipofika Jumatatu Spika Makinda aliliambia Bunge kwamba badala ya kuwasilisha bungeni, sasa Lema alitakiwa awasilishe utetezi wake kwa Spika mwenyewe kwa maandishi.
  Habari za ndani na nje ya Bunge zinasema kwamba suala hilo la Lema na Waziri Mkuu Pinda limeibua makundi ambayo yameanzisha kampeni za siri zikilenga kuonyesha kuwa kwa kauli yake kuhusu vurugu na mauaji ya Arusha ambazo zilielemea utetezi wa Polisi pekee, yeye si mtu makini.
  Taarifa za hakika zinasema tayari Lema amekwishakuwasilisha utetezi wake unaopingana na yale aliyoeleza Waziri Mkuu Pinda bungeni akianzia na taarifa ya kuwa waliofikwa na mauti katika vurugu na mauaji hayo ni Watanzania watatu kama alivyoeleza Waziri Mkuu Pinda ingawa ukweli ni kwamba waliofariki dunia ni Watanzania wawili, Dennis Michael Shirima na Ismail Omary, na Mkenya, Paul Njuguna.
  Hoja nyingine katika utetezi wa Lema inaelezwa ni juu ya utaratibu wa maandamano ya Arusha kama alivyoeleza Waziri Mkuu Pinda kwamba Jeshi la Polisi lilipendekeza njia moja ya maandamano itumike lakini viongozi wa CHADEMA walikataa.
  Katika utetezi wake Lema anadai kwamba si kweli kwamba Polisi walielekeza hivyo, na kwa mujibu wa nyaraka ambazo Raia Mwema imafanikiwa kuona, Lema anasema si kweli pia kwamba waandamanaji walikaribia mita 50 kutoka Kituo cha Polisi ambako ndiko kulikozuka mauaji yale kwa vile CHADEMA kina ushahidi wa picha za video zinazoonyesha ya kuwa mmoja wa waliouawa alifikwa na mauti eneo la mbali na Kituo cha Kati cha Polisi.
  “Kama ni kweli hatua zote zilichukuliwa na Jeshi la Polisi basi ni wazi kwamba watu waliouawa au kujeruhiwa waliuawa au kujeruhiwa kwenye uzio au mlango wa Kituo cha Kati cha Polisi mjini Arusha,”anasema mwanasiasa mmoja ambaye ameona sehemu ya utetezi wa Lema akirejea taarifa ya Polisi inayoashiria kuwa waandamanaji walikaribia kabisa eneo la Polisi.

  Anaongeza mwanasiasa huyo: “Taarifa ya Jeshi la Polisi (aliyonukuu Pinda bungeni) haisemi ukweli wa jinsi matukio yalivyokuwa Arusha. Kwa ushahidi wa picha za video uliopo marehemu mmoja aliuawa eneo la Mianzini ambalo liko zaidi ya kilometa tatu kutoka Kituo cha Polisi cha Arusha.


  “ Aidha, marehemu wa pili alipigwa risasi katika eneo la Kaloleni ambalo nalo liko zaidi ya kilometa moja kutoka kituo hicho. Ushahidi wa video unaungwa mkono na ushahidi wa watu walioshuhudia mauaji hayo wenyewe”.
  Kwa mujibu wa vyanzo kasha vya habari Lema atakosoa pia utaratibu wa jinsi Meya wa Arusha alivyopatikana, utaratibu ambao kwa mujibu wa Waziri Mkuu Pinda ni halali.

  Anasema Lema katika utetezi wake kuhusu utaratibu huo: “ Chini ya kanuni ya 8(3) ya Kanuni za Halmashauri, akidi katika mkutano wa kawaida wa mwaka na mkutano wa kwanza wa Halmashauri itakuwa theluthi mbili ya wajumbe wote wa Halmashauri.

  “ Kwa kusoma kanuni ya 8(3) pamoja na kanuni ya 9, ni wazi kwamba Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri wanatakiwa kuchaguliwa na mkutano wa kwanza wa Halmashauri.
  “ Ili kukidhi matakwa ya kanuni hizi, mkutano wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Arusha ulipaswa kuwa si chini ya wajumbe 21 ambao ni theluthi mbili ya wajumbe wote wa Halmashauri hiyo. Kwa maana hiyo, mkutano wa tarehe 18 Desemba haukuwa mkutano halali na viongozi wa Halmashauri waliochaguliwa na mkutano huo hawawezi kuwa halali”.


  Kipengele kingine cha utetezi wa Lema kinahusu kauli ifuatayo ya Waziri Mkuu aliposema; “Mheshimiwa Spika, yaani hata kwa hesabu tu za kawaida za mtoto wa darasa la kwanza hakuna namna ambavyo kwa hali ilivyokuwa kwamba mna CHADEMA wajumbe 14, mna CCM 16, utashindaje?”
  Anajibu kauli hiyo Lema akisema: “Hapa Waziri Mkuu alitaka kuaminisha Bunge kwamba hata kama wajumbe wa CHADEMA wangehudhuria kwenye mkutano huo
  bado wasingeshinda kwa sababu wajumbe wa CCM walikuwa wengi zaidi ya wajumbe wa CHADEMA”.  Anaendelea: “Lakini kwenye hotuba hiyo hiyo Waziri Mkuu alitoa kauli kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Naibu Meya wa Halmashauri hiyo ya Arusha: ‘ wakaingia awamu ya pili ya kumtafuta Naibu Meya, wakapiga kura, mjumbe wa kutoka TLP akashinda, CCM alishindwa hakupata kura hata moja, CHADEMA hawakupata kura hata moja’.

  “Kama iliwezekana kwa mgombea wa TLP ambaye yuko peke yake katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kupata kura za wajumbe wote wa CCM na kumshinda mgombea wa CCM ambaye – kwa kauli ya Waziri Mkuu – hakupata kura hata moja, je, ingeshindikanaje kwa mgombea wa CHADEMA yenye wajumbe 14 kushinda? “Swali hili ni muhimu hasa kwa vile chini ya kanuni ya 9(1) ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Arusha inasema kwamba kura ya kumchagua Mwenyekiti na Makamu wake itakuwa ni ya siri! Na kama inavyofahamika, katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, ni mgombea wa CHADEMA ndiye aliyeshinda pamoja na kwamba CCM ina wajumbe wengi zaidi katika Halmashauri hiyo.”
  Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Raia Mwema mjini Dodoma, wamesema hakukuwa na sababu kwa Spika kumlazimisha Lema kuwasilisha ushahidi na badala yake angetumia busara zaidi kuimaliza hoja hiyo bila kuathiri pande zote.

  “Spika ameteleza ama anakusudia kumdhalilisha Waziri Mkuu kwani hakuwa na haja ya kumlazimisha Lema awasilishe ushahidi maana hakuwa amesema Waziri Mkuu ni muongo bali aliomba mwongozo. Sasa ndiyo maana tena amebadili na kumtaka awasilishe ushahidi kwa maandishi,” anasema Mbunge mmoja wa CCM, ambaye ameomba asitajwe.
   
 2. d

  dmalale Member

  #2
  Feb 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2009
  Messages: 34
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  [​IMG]Polisi wamchuuza kwa taarifa zao
  [​IMG]
  Mbunge Lema awasilisha hoja 10
  [​IMG]Spika ataka iwe kwa maandishi

  Mwandishi Wetu
  Februari 16, 2011

  SAKATA la vurugu na mauaji yaliyotokana na maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), mkoani Arusha linaelekea kumuelemea Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

  Hiyo inatokana na taarifa ya kuwa kauli ya Waziri Mkuu Pinda ya wiki iliyopita iliyokituhumu CHADEMA kuhusika na vurugu hizo zilizoishia katika mauaji ya watu watatu, ilitokana na maoni ya Polisi ambao katika matukio hayo wao ni watuhumiwa.

  Baada ya Pinda kutoa taarifa kuhusu tukio la Arusha bungeni, Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema, aliomba Mwongozo wa Spika, akitaka kujua mbunge anaweza kufanya nini akibaini ya kuwa "kiongozi mkubwa kama Waziri Mkuu analidanganya Taifa na Bunge ".

  Baada ya kuomba Mwongozo wa Spika, Spika Anne Makinda, alimtaka Lema kuwasilisha bungeni ushahidi wa "uongo wa Waziri Mkuu", ifikapo juzi Jumatatu.

  Hata hivyo ilipofika Jumatatu Spika Makinda aliliambia Bunge kwamba badala ya kuwasilisha bungeni, sasa Lema alitakiwa awasilishe utetezi wake kwa Spika mwenyewe kwa maandishi.

  Habari za ndani na nje ya Bunge zinasema kwamba suala hilo la Lema na Waziri Mkuu Pinda limeibua makundi ambayo yameanzisha kampeni za siri zikilenga kuonyesha kuwa kwa kauli yake kuhusu vurugu na mauaji ya Arusha ambazo zilielemea utetezi wa Polisi pekee, yeye si mtu makini.

  Taarifa za hakika zinasema tayari Lema amekwishakuwasilisha utetezi wake unaopingana na yale aliyoeleza Waziri Mkuu Pinda bungeni akianzia na taarifa ya kuwa waliofikwa na mauti katika vurugu na mauaji hayo ni Watanzania watatu kama alivyoeleza Waziri Mkuu Pinda ingawa ukweli ni kwamba waliofariki dunia ni Watanzania wawili, Dennis Michael Shirima na Ismail Omary, na Mkenya, Paul Njuguna.

  Hoja nyingine katika utetezi wa Lema inaelezwa ni juu ya utaratibu wa maandamano ya Arusha kama alivyoeleza Waziri Mkuu Pinda kwamba Jeshi la Polisi lilipendekeza njia moja ya maandamano itumike lakini viongozi wa CHADEMA walikataa.

  Katika utetezi wake Lema anadai kwamba si kweli kwamba Polisi walielekeza hivyo, na kwa mujibu wa nyaraka ambazo Raia Mwema imafanikiwa kuona, Lema anasema si kweli pia kwamba waandamanaji walikaribia mita 50 kutoka Kituo cha Polisi ambako ndiko kulikozuka mauaji yale kwa vile CHADEMA kina ushahidi wa picha za video zinazoonyesha ya kuwa mmoja wa waliouawa alifikwa na mauti eneo la mbali na Kituo cha Kati cha Polisi.

  "Kama ni kweli hatua zote zilichukuliwa na Jeshi la Polisi basi ni wazi kwamba watu waliouawa au kujeruhiwa waliuawa au kujeruhiwa kwenye uzio au mlango wa Kituo cha Kati cha Polisi mjini Arusha,"anasema mwanasiasa mmoja ambaye ameona sehemu ya utetezi wa Lema akirejea taarifa ya Polisi inayoashiria kuwa waandamanaji walikaribia kabisa eneo la Polisi.

  Anaongeza mwanasiasa huyo: "Taarifa ya Jeshi la Polisi (aliyonukuu Pinda bungeni) haisemi ukweli wa jinsi matukio yalivyokuwa Arusha. Kwa ushahidi wa picha za video uliopo marehemu mmoja aliuawa eneo la Mianzini ambalo liko zaidi ya kilometa tatu kutoka Kituo cha Polisi cha Arusha.

  " Aidha, marehemu wa pili alipigwa risasi katika eneo la Kaloleni ambalo nalo liko zaidi ya kilometa moja kutoka kituo hicho. Ushahidi wa video unaungwa mkono na ushahidi wa watu walioshuhudia mauaji hayo wenyewe". Kwa mujibu wa vyanzo kasha vya habari Lema atakosoa pia utaratibu wa jinsi Meya wa Arusha alivyopatikana, utaratibu ambao kwa mujibu wa Waziri Mkuu Pinda ni halali.


  Anasema Lema katika utetezi wake kuhusu utaratibu huo: " Chini ya kanuni ya 8(3) ya Kanuni za Halmashauri, akidi katika mkutano wa kawaida wa mwaka na mkutano wa kwanza wa Halmashauri itakuwa theluthi mbili ya wajumbe wote wa Halmashauri.

  " Kwa kusoma kanuni ya 8(3) pamoja na kanuni ya 9, ni wazi kwamba Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri wanatakiwa kuchaguliwa na mkutano wa kwanza wa Halmashauri.


  " Ili kukidhi matakwa ya kanuni hizi, mkutano wa uchaguzi wa Meya na Naibu Meya wa Arusha ulipaswa kuwa si chini ya wajumbe 21 ambao ni theluthi mbili ya wajumbe wote wa Halmashauri hiyo. Kwa maana hiyo, mkutano wa tarehe 18 Desemba haukuwa mkutano halali na viongozi wa Halmashauri waliochaguliwa na mkutano huo hawawezi kuwa halali".

  Kipengele kingine cha utetezi wa Lema kinahusu kauli ifuatayo ya Waziri Mkuu aliposema; "Mheshimiwa Spika, yaani hata kwa hesabu tu za kawaida za mtoto wa darasa la kwanza hakuna namna ambavyo kwa hali ilivyokuwa kwamba mna CHADEMA wajumbe 14, mna CCM 16, utashindaje?"

  Anajibu kauli hiyo Lema akisema: "Hapa Waziri Mkuu alitaka kuaminisha Bunge kwamba hata kama wajumbe wa CHADEMA wangehudhuria kwenye mkutano huo bado wasingeshinda kwa sababu wajumbe wa CCM walikuwa wengi zaidi ya wajumbe wa CHADEMA".

  Anaendelea: "Lakini kwenye hotuba hiyo hiyo Waziri Mkuu alitoa kauli kuhusu matokeo ya uchaguzi wa Naibu Meya wa Halmashauri hiyo ya Arusha: ' wakaingia awamu ya pili ya kumtafuta Naibu Meya, wakapiga kura, mjumbe wa kutoka TLP akashinda, CCM alishindwa hakupata kura hata moja, CHADEMA hawakupata kura hata moja'. "Kama iliwezekana kwa mgombea wa TLP ambaye yuko peke yake katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kupata kura za wajumbe wote wa CCM na kumshinda mgombea wa CCM ambaye – kwa kauli ya Waziri Mkuu – hakupata kura hata moja, je, ingeshindikanaje kwa mgombea wa CHADEMA yenye wajumbe 14 kushinda? "Swali hili ni muhimu hasa kwa vile chini ya kanuni ya 9(1) ya Kanuni za Kudumu za Halmashauri ya Jiji la Arusha inasema kwamba kura ya kumchagua Mwenyekiti na Makamu wake itakuwa ni ya siri! Na kama inavyofahamika, katika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, ni mgombea wa CHADEMA ndiye aliyeshinda pamoja na kwamba CCM ina wajumbe wengi zaidi katika Halmashauri hiyo."

  Baadhi ya wabunge wa CCM waliozungumza na Raia Mwema mjini Dodoma, wamesema hakukuwa na sababu kwa Spika kumlazimisha Lema kuwasilisha ushahidi na badala yake angetumia busara zaidi kuimaliza hoja hiyo bila kuathiri pande zote.

  "Spika ameteleza ama anakusudia kumdhalilisha Waziri Mkuu kwani hakuwa na haja ya kumlazimisha Lema awasilishe ushahidi maana hakuwa amesema Waziri Mkuu ni muongo bali aliomba mwongozo. Sasa ndiyo maana tena amebadili na kumtaka awasilishe ushahidi kwa maandishi," anasema Mbunge mmoja wa CCM, ambaye ameomba asitajwe.
   
 3. n

  niweze JF-Expert Member

  #3
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sasa Tutaona Demokrasia ya Tanzania, Huko nje ya nchi wanataka "Kuonekana ni Viongozi wa Demokrasia Wakati ni Wanyima Haki na Waongo Kupindukia"
  Makinda Mwache Mnyika Atoa Ushahidi Mbele ya Wananchi Kwani Pinda si Alidanganya Taifa Mbele ya Wananchi...
   
 4. Kimilidzo

  Kimilidzo JF-Expert Member

  #4
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 1,346
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Namuonea huruma sana huyu mama yangu Makinda... Hadi 2015 kivuli cha Mzee Six kitamuandama sana.
   
 5. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #5
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Pinda na hesabu za drs la I...Kaazi kwelikweli
   
 6. Avocado

  Avocado Member

  #6
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ndiyo shida ya kusema mambo bila kuyafanyia utafiti wa kina,tatizo ni kutokubali kuwajibika hata pale makosa ya waaazi yanapofanyika,kisa CHAMA TAWALA !
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Huyu mama inabidi awe makini, akifikiri kuwa anasaidia ccm kumbe ndo anabomoa...
   
 8. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #8
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  mkuu ni Lema si mnyika,naomba urekebishe hapo.
   
 9. ChescoMatunda

  ChescoMatunda JF-Expert Member

  #9
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,189
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  yangu macho kumbe hesabu ndogo ndo saizi yetu kubwa tunaibiwa ibiwa sana vipi kuhusu hesabu za kulipa downs??
   
 10. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #10
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kama ilikuwa kumsikiliza pinda cku ile daah utazani alikuwa anatoa ukweli. hata alipoambiwa iundwe tume huru bado alikuwa anakomaa..hakuna kuunda timu! na pia bac w/k aombe radhi.
   
 11. L

  Lorah JF-Expert Member

  #11
  Feb 17, 2011
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 1,193
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mijizi yote... imeanza Misri na kwetu itawezekana bwana kwanza wapiga mabomu wameshachakachuliwa mishahara yao hawatatoa yale makali....watu hamuamini ila ndo tunakoelekea tumechoka hata muuza chipsi ameshachoka .... wazazi wa wale wanafunzi 300,000 wa shule za kata nao wameshachoka, wawekezaji nao wameshachoka na umeme, sasa tunasubiri nini ..........
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  pinda naye ameshakuwa mwiba sasa................yaani pinda na akili yake anawakumbusha watz kuhusu elimu ya darasa la kwanza?.......hajui kuwa hisabati ni somo linalwashindwa wanafunzi kwa zaidi ya 100%?......pinda pinda pinda.....pinda hajui kuwa watoto wetu wanamaliza darasa la saba na kufaulu kuendelea na kidato cha kwanza wangali hawajui kusoma na kuandika?.....pinda pinda pindA KWELI AMEPINDA.........bora angesema hata watoto wa form six wanaweza hiyo hesabu ndogo.................sijui wapi tutapata viongozi wa kutusaidia
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hapo sasa! Hata vyombo vya mlipa kodi vinachakachua mambo, anayandika riport ya uongo na kumpa kiongozi wake sio muhujumu? Kumbe hizi ndio zinaitwa taarifa za kiinteligensia. Naanza kupata wasiwasi kama kweli kuna inteligensia malini. Naona kama demokrasi makini inakuja juu sana.

  Masikini wee, watu watalia tena bungeni.:msela:
   
 14. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #14
  Feb 17, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Akomeshwe kabisa huyo Pinda kama hana Adabu afundishwe adabu sio kazi kuja kusema uongo bungeni akifikiri watanzania ni wajinga kama wamezoea kuiba mali za Taifa sasa utafikia kikomo chao wapumbavu pamoja na Makimba wao:coffee:
   
 15. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Mkinda anataka kumlinda Pinda lakini amekosea wazi wazi, kwanza kama kiongopzi hakupaswa kutoa majibu mepesi kwenye maswali magumu. Bado kidogo ataangua machozi tena akitaka Lema aadhibiwe ili aendelee kupeta na uwaziri mkuu wake.
   
 16. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #16
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Waliopinga makinda kuwa spika hawakusema hivyo eti kwa sababu tu ya kumpenda sitta, bali kwa kuwa wanajua pia kuwa ana makinda bado na ataendelea kuwa kinda asiye na hekima wala busara, mtu anayetawaliwa na jazba na kutotumia busara.
   
 17. matungusha

  matungusha JF-Expert Member

  #17
  Feb 17, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Spika wetu hutenda kabla yakufikiri sasa kaumbuka anataka akaufiche ushahid oficine kwake!!! hii ni fedheha kwa bunge la kumi kupata spika asiye mstaarabu!!!!
   
 18. S

  SUWI JF-Expert Member

  #18
  Feb 17, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Waonyeshe uungwana.. Waziri Pinda aombe msamaha kwa kutoa habari kutokana na chanzo cha upande mmoja, zisizo na uchunguzi. Nae Spika aombe radhi kwa kutomtendea haki Lema alipotaka mwongozo badala yake akampa muda wa kujieleza.!!!!!!!!! THEY SHOULD KNOW KWAMBA WTZ HATA KAMA NI WAJINGA SI KWA KIWANGO WANACHODHANI!!! SHAME ON THEM.....
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  Feb 17, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  asante kwa kuichambua hii kitu kwa makini namna hii! hapa kuna maana mbili...1)Waziri Mkuu amepewa ripoti ya uongo na kuisoma bila kuhakikisha; au 2) Waziri Mkuu alikuwa na adha ya kudanganya bunge!
  Nadhani conclusion ya yote mawili ni resignation! Hatuwezi kukubali hata kidogo! Pinda mmoja wa walewale na anaendeleza siasa za walewale. Hakuna cha mtoto wa mkulima wali nini!

  P.S.: It's a shame kwa chombo cha mlipa kodi kumdanganya huyo huyo mlipa kodi...
   
 20. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #20
  Feb 17, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  no longer SON OF PEASANT!!!!!! ccm ni MACHINE MOJA MBAYA SANA. NDIYO MAANA HATA MIMI NIMEIHAMA! UKIINGIA KULE LAZIMA NA WEWE UVISHWE MAWANI MAPYA ILI UUONE UHALISIA KATIKA MWANGA TOFAUTI!
   
Loading...