Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,191
- 144,025
Kauli uliyoitoa mapema leo huko Mwanza ya kwamba watu wa huko 'wasibomoleshwe' nyumba zao kwa sababu wao ndo walokupa urais si nzuri hata kidogo.
Ni kauli ya kibaguzi kabisa na ambayo inapaswa kupingwa na mtu yeyote yule mwenye akili timamu.
Wewe unatoa kauli kama hiyo huko Mwanza huku kukiwa na mamia kama siyo maelfu ya watu wa sehemu zingine ambao tayari wameshavunjiwa nyumba zao na majengo yao, unadhani utaelewekaji? Unadhani hakuna kati ya hao ambao wameshavunjiwa nyumba zao waliokupigia kura?
Tayari baadhi ya watu wanadhani wewe ni mkabila na mkanda na leo ndo umezidi kuthibitisha kuwa wako sahihi.
Sasa mimi sijui kilichopo moyoni mwako maana sina uwezo wa kuingia na kushuhudia mwenyewe kwa macho yangu kilichomo humo.
Lakini kwa maneno uliyoyazungumza huko Mwanza, na kwa kuangalia mambo ambayo tayari yameshafanyika [ya watu kuvunjiwa nyumba zao sehemu zinginezo nchini], mtu akikuita wewe ni mkabila na mkanda na mwenye upendeleo wa waziwazi atokuwa hajakosea wala kukusingizia.
Sasa basi, wahenga walisema ulimi hauna mfupa. Labda ulikosea tu kwa ulimi kuteleza lakini hukuwa unamaanisha kama ilivyopokelewa na watu. Hivyo, kama ulikosea tu na hukumaanisha ulichokisema basi jishushe na omba radhi.
Tena omba radhi kwa maneno yako mwenyewe na siyo ya mtu mwingine. Ongea kutoka kwenye kilindi cha moyo wako. Nje ya hapo huenda kusiwepo na mtu atakayeamini udhati wa hiyo radhi yako na utaenda kwenye vitabu vya historia kama rais mbovu kupita wote katika historia ya Tanzania.