Bomoabomoa Mwanza: Rais Magufuli omba radhi kama....

Bomoabomoa Mwanza: Rais Magufuli omba radhi kama....

Kauli uliyoitoa mapema leo huko Mwanza ya kwamba watu wa huko 'wasibomoleshwe' nyumba zao kwa sababu wao ndo walokupa urais si nzuri hata kidogo.

Ni kauli ya kibaguzi kabisa na ambayo inapaswa kupingwa na mtu yeyote yule mwenye akili timamu.

Wewe unatoa kauli kama hiyo huko Mwanza huku kukiwa na mamia kama siyo maelfu ya watu wa sehemu zingine ambao tayari wameshavunjiwa nyumba zao na majengo yao, unadhani utaelewekaji? Unadhani hakuna kati ya hao ambao wameshavunjiwa nyumba zao waliokupigia kura?

Tayari baadhi ya watu wanadhani wewe ni mkabila na mkanda na leo ndo umezidi kuthibitisha kuwa wako sahihi.

Sasa mimi sijui kilichopo moyoni mwako maana sina uwezo wa kuingia na kushuhudia mwenyewe kwa macho yangu kilichomo humo.

Lakini kwa maneno uliyoyazungumza huko Mwanza, na kwa kuangalia mambo ambayo tayari yameshafanyika [ya watu kuvunjiwa nyumba zao sehemu zinginezo nchini], mtu akikuita wewe ni mkabila na mkanda na mwenye upendeleo wa waziwazi atokuwa hajakosea wala kukusingizia.

Sasa basi, wahenga walisema ulimi hauna mfupa. Labda ulikosea tu kwa ulimi kuteleza lakini hukuwa unamaanisha kama ilivyopokelewa na watu. Hivyo, kama ulikosea tu na hukumaanisha ulichokisema basi jishushe na omba radhi.

Tena omba radhi kwa maneno yako mwenyewe na siyo ya mtu mwingine. Ongea kutoka kwenye kilindi cha moyo wako. Nje ya hapo huenda kusiwepo na mtu atakayeamini udhati wa hiyo radhi yako na utaenda kwenye vitabu vya historia kama rais mbovu kupita wote katika historia ya Tanzania.
Kimtokacho mtu ndicho kimwuingiacho
 
Alishindwa kuwa mkweli kusema yeye ni mbaguzi hivyo akaja na sababu uchwara kwamba wao ndiyo waliomchagua. Kwa maneno mengine mikoa yote iliyobaki hawakumchagua hivyo kubomolewa wa kwenye mikoa hiyo ni RUKHSA.

Leo bwana Yule amewaagiza mawaziri wake kabla ya kuwabomolesha wakazi wa Mwanza kwanza wapitie upya ramani Na wawe Na human face. Je, hii sio double standards? Kwanini human face haikuwa kwa wanaKimara ambao Pia nao wamekuwa pale kwa muda mrefu? Je, kapataje taarifa za boboaboboa ya Mwanza asiijue ya Kimara kilometa 4 kutoka Ikulu? Au dawa ya Mh Nyarandu imemkolea?

It hurts
 
Mbona mimi nilikuwepo kwenye eneo lenyewe la hotuba na sijaona kama kauli aliyoitoa Rais kama ina ukabila au ukanda kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu JF.

Ninavyoona mimi watu wana Ile hisia ya kwamba rais ni mbaguzi hivyo walishatengeneza attention flani.So akiongea kitu hata ambacho inawezekana hakumaanisha wanapitia humohumo.

Rais anaweza kuwa mbaguzi lakini tumuhukumu kwa hoja zingine ila sio hii ya Leo.
 
Mbaya zaidi ametoa kabisa maagizo kwa wateule na watendaji wa serikali kuhakikisha Mwanza nyumba hazibomolewi.

Ushauri mzuri sana, lakini alishaweka wazi hapangiwi wala hashauriwi
kwa nini mnapindisha maneno? Si sawa hii. Mkuu kaongea vizuri kabisa na kasema kwamba wakae wafanya maamuzi kwa wale ambao wako ndani ya eneo hakuna jinsi watabomolewa kwa haitakuwa busara ndege kuruka ndani ya makazi.Concern ya mkuu ni kwamba kuna nyumba haziko ndani ya eneo husika so wafanya maamuzi waangalie upya kuona kama kama kama kuna uwezekano wa ku-exclude wale wapiga kura.
 
Hoja yenyewe na mahali alipoitolea ndiko kunakoleta utata. Na nadhani washauri wake wa mambo ya hotuba wamwambie kwamba maneno yana sumu kali kuliko matendo!

Nakubaliana nawe kabisa.

Angesema hivyo mapema kabisa wakati zoezi zima ndo linaanza na akasema hivyo sehemu kama Dar basi naamini mapokezi yake yangekuwa tofauti kabisa maana Dar ndo melting pot ya Tanzania.

Sasa kasemea huko Mwanza...Usukumani....

Jamaa ikija kwenye political skils ni bure kabisa yaani.....
 
nimekupa like kwa mara ya kwanza kwa mambo yahusuyo siasa
The same to me. Kuna wakati watu wanauona ukweli na wanausema. Hakika NN katwanga ukweli hapo. Ila hata akiomba radhi ni too late kwani watu wameshathibitisha kile kisemwacho kila siku kuhusu tabia yake ya ubaguzi. Na kwa vile hataki hotuba za kuandaliwa bali yeye anayatoa ya moyoni basi ndivyo alivyo.
Nilisoma sura za wale waliokuwapo jukwaani ambao sio wakazi wa Mwanza, zilionyesha kukerwa kabisa na kauli ile. Ni kwa vile mkuu hawezi kuzabwa kibao tuu!
 
Watu wamemnukuu vibaya. Kama angekuwa na lengo hilo asiwaambia mawaziri wakae wajadiliane ni wepi waondoke na ni wepi wabaki. Mfano, eneo la Kigoto, kuwaondoa wakara wa watu pale ni kuwaonea tu, wamekuwepo pale kabla ya hilo bwalo la polisi.
kwa hiyo humu Jamii forum watu wote hatujui kutafisiri alicho kiongea JPM au humu wote tuna chuki na JPM hadi tunukuu vibaya
 
Kauli uliyoitoa mapema leo huko Mwanza ya kwamba watu wa huko 'wasibomoleshwe' nyumba zao kwa sababu wao ndo walokupa urais si nzuri hata kidogo.

Ni kauli ya kibaguzi kabisa na ambayo inapaswa kupingwa na mtu yeyote yule mwenye akili timamu.

Wewe unatoa kauli kama hiyo huko Mwanza huku kukiwa na mamia kama siyo maelfu ya watu wa sehemu zingine ambao tayari wameshavunjiwa nyumba zao na majengo yao, unadhani utaelewekaji? Unadhani hakuna kati ya hao ambao wameshavunjiwa nyumba zao waliokupigia kura?

Tayari baadhi ya watu wanadhani wewe ni mkabila na mkanda na leo ndo umezidi kuthibitisha kuwa wako sahihi.

Sasa mimi sijui kilichopo moyoni mwako maana sina uwezo wa kuingia na kushuhudia mwenyewe kwa macho yangu kilichomo humo.

Lakini kwa maneno uliyoyazungumza huko Mwanza, na kwa kuangalia mambo ambayo tayari yameshafanyika [ya watu kuvunjiwa nyumba zao sehemu zinginezo nchini], mtu akikuita wewe ni mkabila na mkanda na mwenye upendeleo wa waziwazi atokuwa hajakosea wala kukusingizia.

Sasa basi, wahenga walisema ulimi hauna mfupa. Labda ulikosea tu kwa ulimi kuteleza lakini hukuwa unamaanisha kama ilivyopokelewa na watu. Hivyo, kama ulikosea tu na hukumaanisha ulichokisema basi jishushe na omba radhi.

Tena omba radhi kwa maneno yako mwenyewe na siyo ya mtu mwingine. Ongea kutoka kwenye kilindi cha moyo wako. Nje ya hapo huenda kusiwepo na mtu atakayeamini udhati wa hiyo radhi yako na utaenda kwenye vitabu vya historia kama rais mbovu kupita wote katika historia ya Tanzania.
Heri nawe umejitambua, japo kwa masaa tu, siyo mbaya!
 
Je shida ni lugha tu ama ni moyo na dhamira yake.
Ingekuwa lugha tu asingeenda mbali na kuwaagiza viongozi mbalimbali wakae chini na kujadili mbinu tofauti. Wakati sehemu zingine hata kauli ya mahakama haikusikilizwa. Watu wa tabora hawakuwa karibu na airport walikuwa tu karibu na shule tu na bado wakaachwa.
Nasikia Kimara nyumba zote zimevunjwa isipokuwa ya Mkapa. Je ni kweli?
 
Daa sindio muweke clip jaman[emoji35][emoji35][emoji35]ikiwezekana iwe ndo ringtone ya simu zetu ili 2020 watu ambao hawakubolewa ndio wamrudishe.... daah inauma sana lkn hakuna namna. Ajitolee mmoja basi afanye mambo ya kiafghanistan
 
Mtaelewa tuu kuwa tangu tulivyoanza kupiga kelele kuhusu huyu mtu tulilkuwa tupo timamu zaidi yenu wafunga Gidamu.
Mtasubiri sana kuna rais aliwahi sema hahitaji kura za wafanyakazi na bado walimpigia na kumuita shemeji unatuachaje! !!! Hakuna mbadala wa ccm. Wakuu wanalijua hilo na wapiga kura wanajua. Hata Nyarandu analijua hilo. Mtasubiri sana. Bila ccm makini nchi itayumba.
 
Jamaa ikija kwenye political skils ni bure kabisa yaani.....
Kinachokera badala ya wapinzani wake kujenga hoja zitakazomgutusha wataishia kumsakama. Ni vizuri akaambiwa kwamba Urais ni cheo kikubwa sana, kila alisemalo linaweza kuleta athari kwa nchi nzima!
 
Back
Top Bottom