Maelekezo waliyopewa ni kuhakikisha wale wote waliojenga mabondeni , kwenye viwanja vya wazi , juu ya bomba kubwa la majitaka wabomoe nyumba zao kabla ya tarehe Januari 5 .
Hii notisi imebandikwa jana na imesainiwa na mkurugenzi wa manispaa ya Temeke ( nimeiona ).
Wahanga ni pamoja na waliojenga nyuma ya gereza la Keko , Keko Mwanga , Keko Machungwa hasa wale waliojenga kandokando ya mfereji wa maji unaoanzia kota za polisi maarufu kama Mchomba line , wakazi wa Keko juu nao hawajasahaulika hasa walio chini ya Kisiwani bar , tuendelee kutega sikio .
KWA KWELI HUU NI UONEVU WA HALI YA JUU KWA NCHI ZA WENZETU HII HALI HAIKUBALIKI .WATU HAWA WOTE WALIACHIWA KUJENGA KWA MIAKA KADHAA LEO WANARUDI KUWAHUJUMU MAISHA YAO . NYUMBA ELFU 3 NA KUENDELEA NI NYINGI SANA TUJAALIE KILA NYUMBA WANAISHI 3 HAPA TUNAPATA WATU ELFU 9 MBALI WATOTO NADHANI HAPA MH MAGUFULI ANAHUJUMIWA NA WANATAKA KUMHARIBIA UONGOZI WAKE .
NATOWA WITO KWA WANYONGE WOTE WANAOKABILIWA NA JANGA HILI WAUNGANE PAMOJA KAMA NI MAANDAMANO AU NJIA NYENGINE YOYOTE WASIMAMIE HAKI YAO .
HII SI MOVE YA KUSAPORT KWA KWELI .