Bomoa bomoa yaendelea Kariakoo na Mnazi Mmoja

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Habari wakuu,

Muda huu kuna bomoa bomoa inaendelea Kariakoo katika jitihada za upanuzi/maboresho ya reli. Sio siri ni simanzi kubwa kwa waathirika.

[HASHTAG]#MsinipangieChaKubomoa[/HASHTAG]
 
Yaani watu wamekula pesa last week, wiki hii wanaenda kubomoa.

Wamechoka kazi zao hao, warudishe hizo pesa haraka.

Kama hao walijenga pasipotakiwa, basi ndio ilivyopangwa.
 
Ni matendo ya kuwatumbukiza watu katika lindi la umaskini uliotopea, ndio ni nia njema ya kuboresha ama maendeleo lakini hawa binadamu wanaoondolewa katika maeneo hayo wana watoto wao wadogo wanaoyaona matukio na kuathirika je tunatarajia watakuwa wazalendo kweli kwa miradi itakayofanyika hapo? Nadhani wanapaswa hawa watendaji wetu kuwa na uono mpana zaidi sio kuhimiza na kuimba uzalendo huku wanawavunja mioyo wananchi na kulemaza vipato vyao.
 
Kama mtu alijenga eneo la reli kubomolewa ni haki yake ya kikatiba. Watu wengi wanaweza kuwaonea huruma hao waliojenga kwenye hifadhi ya reli lakini ukweli lazima tuuseme, asilimia kubwa utakuta hao watu walitoa sana rushwa ili wapate vibali vya ujenzi kwenye eneo la reli, na hii huwa inatokea kwa watu wenye kupenda kung'ang'aniza mambo kisa tu anahela, sasa acha sheria ifuate mkondo wake.
 
Wafanya biashara ndogondogo walioondolewa mtaa wa Msimbazi palipojengwa BRT Terminal walipelekwa pale na Jiji wakawa wanachukua kodi!! Leo wanaambiwa wako pale kinyume cha sheria. Najiuliza: Wakati Halmashauri inawapeleka pale walikuwa hawajui kama ni eneo la reli? Kama walijua si eneo halali kwanini waliwapeleka pale na kisha kuwatoza tozo? Je wale mama ntilie na wauza bidhaa mbalimbali wametengewa wapi mbadala licha ya kuvunjiwa bidhaa zao? Je pindi wakitupiga roba mitaani tulie na nani?
 
Habari wakuu,

Muda huu kuna bomoa bomoa inaendelea Kariakoo katika jitihada za upanuzi/maboresho ya reli. Sio siri ni simanzi kubwa kwa waathirika.

[HASHTAG]#MsinipangieChaKubomoa[/HASHTAG]

Mwambieni RC wa Dar apite hapo mida hii kuangalia maendeleo ya zoezi
 
dah hilo jengo si lilijengwa barabaran kabisa hapo kamata!

halafu kuna reli, nadhan hata ile sheli pia itaondoka hapo kamata
 
Ni matendo ya kuwatumbukiza watu katika lindi la umaskini uliotopea, ndio ni nia njema ya kuboresha ama maendeleo lakini hawa binadamu wanaoondolewa katika maeneo hayo wana watoto wao wadogo wanaoyaona matukio na kuathirika je tunatarajia watakuwa wazalendo kweli kwa miradi itakayofanyika hapo? Nadhani wanapaswa hawa watendaji wetu kuwa na uono mpana zaidi sio kuhimiza na kuimba uzalendo huku wanawavunja mioyo wananchi na kulemaza vipato vyao.
Nanni aliwauzia kiwanja?.nani aliwapa kibali cha ujenzi??
 
Back
Top Bottom