Bomoa bomoa yaanza Kurasini shimo la udongo kupisha muwekezaji

Miaka 20 ijayo ukisikia magadi walipua Bomu jamii mnabaki kulaumu! Hivi umnategemea nini katika mazingira kama haya!
Leo hii mtoto mdogo wa umri wa miaka btwn 5-10 anashuhudia nyumba yao inabomolewa na wao kubakia nje bila kibanda chakujihifadhi chini ya usimamizi wa Serikali?.

Serikali makini kwa mtazano wangu ingewafungulia mashitaka wale wote waliokataa kuhama ili hali wamechukua pesa za kuwa fidia na si kunyume chake!
Sidhani kama ni kweli mimi nilikuwa naishi kurasini mwenye nyumbani wangu alipewa mil 200 hivi zilikuwa nyumba mbili afu Akasema hazitoshi wakapeleka malalamiko waongezewe yaani walikuwa wanatest tu kama hataongezewa ila hakuna mkazi wa Kurasini ambaye hakulipwa ila haturidhiki na tunachopewa.
 
cjui nani atamstopisha huyu ndugu..... kichaaa kapewa rungu kwa kweli!!!! kesi bado iko mahakaman watu wanavunjiwa
 
Tatizo lao ni tamaa wenzao washachukua chao na kujenga nyumba zenye viwango sehemu zingine kuliko walizokuwa nazo awali wao wanadai bei za soko bila ya uhalisia ya wanunuzi wa bei zao eneo zima.

Binafsi ningeelewa kama umoja wao ni kutaka muwekezaji aende sehemu zingine awaachie makazi yao hata hivyo inataka support ya wengi kuliko wachache; muda wa kuleta maendeleo sasa sio wa kubembelezana na tamaa vunja vunja; halafu mtu aliekuwa anawatetea Abas Mtevu wamemtema maana ili zoezi lilikuwa lianze muda mrefu sana.
 
cjui nani atamstopisha huyu ndugu..... kichaaa kapewa rungu kwa kweli!!!! kesi bado iko mahakaman watu wanavunjiwa

utawala hadaa!sura kamili sasa.tutaonesha huruma hadaa ikikaribia 2020.
 
Back
Top Bottom