Bomoa bomoa barabara ya Morogoro inaendelea

Bomoa bomoa barabara ya Morogoro inaendelea

Hii bomoa bomoa haiko rasmi nilikuwepo sehemu ya tukio na nikafanikiwa kuongea na baadhi ya wahusiki na kwa majibu yao leo walikua wanatoa salam tu kwa nyumba zote zenye x na ni kama tangazo kua kuanzia leo siku yoyote watakuja kubomoa, na kwa nyumba amvazo tayari watu walishabomoa nyumba zao na kuacha baadhi ya kuta ndio wakikua wanamalizia kuibomoa, wakasema siku wakija hawataruhusu mtu kutoa kitu hata kimoja ndani hivyo watu wahame wenyewe..

Kuhusu kesi ni kweli kuna kesi mbili za malalamiko ya bomoa bomoa, Moja ikiwa ipo katika hatua za awali na nyingine ni keshi ya msingi ambayo inangoja kupangiwa siku ya kutajwa.

All in All tumuombe Mwenyezi Mungu maana ni watu wengi sana watakao athirika kwani ni mita 122 kila upande.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna maeneo mengine Tanroad wanatia aibu! Kwani ili ujenge barabara ni muhimu kuwa na eneo la kutosha ili kupunguza ajali na foleni! Ila hizi barabara wanazojenga kama kwa Mzee wa upako ni Mfano WA ukosefu WA weledi na matumizi mabaya ya pesa za walipakodi! Na hizi barabara kila uchao ni ajali! Ndyamkama Badilika acha sihasa
 
Habarini za mchana, wale wa mororgoro road kuanzia stop over na waliondani ya mt 90 za barabara rejeeni nyumbani huku wameanza kubomoa

Na huko ndiko ' Kiuchambuzi ' imeonekana katika zile ' Kura ' Milioni 6 za Mzee wa Matumaini ' Hewa ' alipata almost ' Kura ' kama Milioni 4 hivi huku hizo zilizobaki nyingi zikiwa ni za Kilimanjaro na Arusha. Miaka hii mitano na ile mitano ijayo na ile 20 tunayopanga kumuongezea ' tutaheshimiana ' tu hapa Tanzania.

Akhsante sana Serikali ya Awamu ya ' Gwala / Tano ' fanyeni Kazi yenu kwani tunatambua fika kwamba nchi hii inaendeshwa kwa misingi ya Sheria hivyo popote pale ambapo itatokea mkaona Sisi ' Raia ' tumeanza ' Kukengeuka / Kukosea ' tafadhali msinyamaze au msituogope bali ' tunyoosheni ' ili akili zetu zitukae sawa na tuache kuishi kwa mazoea.
 
Kwanini wabomoe usiku.

Tuwekee picha kiongozi
 
wengine tumetii sheria bila shuruti.
tulibomoa wenyewe na kuhama mapema!!!
 
wengine tumetii sheria bila shuruti.
tulibomoa wenyewe na kuhama mapema!!!
Mbona unazungumza kirahisi namna hiyo mkuu? Hivi umewahi kumiliki hata kibanda kweli!!

Nauliza tuu
 
Back
Top Bottom