Bollen Ngetti apatikana huko Segerea

Duuh mpka huruma
 
Wamemteka Bollen na kubwa walilomhoji ni mahusiano yake na Bernard Membe anayetishwa kila siku na CCM kwa hisia zao kuwa atajitosa kupambana kuitaka tiketi ya kuteuliwa na chama kugombea Urais.

Hivi hapo kosa lipo wapi? Mbona mnamuogopa hivyo hadi kutumia vyombo vya dola kusumbua watu wengine?

Hii inaonyesha hamuungwi mkono ndani ya CCM kama mnavyotaka kuaminisha huku nje ndio maana mnahaha na kutaabika kunyamazisha kwa vitisho na ubabe kwani mnajua kuwa kukiwa na uchaguzi ni chali tu.

Acheni kutesa watu kwa hisia zenu.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe naye ndo wale waliolea Mfumo dhalimu , wakati tukiendelea kutubu

Nina maswali
1.Where is Ben
2.Kwanini laini yake ya Simu aliuziwa Mwingine
3.Kwanini hasa kwa nini
 
Membe naye ndo wale waliolea Mfumo dhalimu , wakati tukiendelea kutubu

Nina maswali
1.Where is Ben
2.Kwanini laini yake ya Simu aliuziwa Mwingine
3.Kwanini hasa kwa nini
Membe ni wale wale lakini bado najiuliza inakuwaje wanasema hawamuogopi lakini wanateka vijana wengine ili kuwauliza ya Membe wakati wamemuita kamati ya maadili.
Hivi huyo anayetaka kunyang'anywa na Membe nafasi ya kugombea hawezi jitetea mwenyewe kwa kuonyesha anafaa hadi vibaraka watumie ofisi zao na nguvu kubwa kumsimamisha Membe?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Membe akikubali kwenda kuhojiwa tu Basi watamkolimba, bora atulie tu
 
Kisu kimeanza kukata mfupa (membe) atafikiwa tu ,jipe muda

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
Atafikiwa ili iweje? Kwamba Hana haki ya kugombea nafasi yoyote ya kiuongozi ccm? Na Kama ndio, ni kwanini njia ya kidemokrasia isitumike kuwapata viongozi huko ccm kwa maana ya kupigiwa kura kwa wahitaji? Ngoja nisubiri kuuona udikteta unavyotamalaki ccm huku wakiwanyooshea vidole wengine!
 
Membe naye ndo wale waliolea Mfumo dhalimu , wakati tukiendelea kutubu

Nina maswali
1.Where is Ben
2.Kwanini laini yake ya Simu aliuziwa Mwingine
3.Kwanini hasa kwa nini
Kamuulize Membe mwenyewe!
 
Wakati mwingine hoja zenu zinakuwa kama za makafiri fulani hivi!!! Yaani mtu akiwa na hoja tofauti juu ya mwingine basi jawabu ni utekaji na si kwenda mahakamani kushtaki!!!? Yaani tupo kwenye "Law of the jungle" katika serikali ya awamu ya tano. Kwamba ukiwa na mawazo yaliyo tofauti na mtawala basi wewe umeingia vitani dhidi ya serikali!!? Kweli tuko Misri, lini tutaiona Kaanani, Mungu anajua!!!
 
Membe, endelea kuwavuruga hao wakuja mpaka wapoteane! Unatambua fika kuna mtu "mzito" yuko nyuma yako hivyo hawana cha kukufanya, zaidi tu wataishia kukutishia nyau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…