Boeing walituahidi ndege ya nyongeza, imeshafika?

kwanini msiende kuuuliza wizara husika milango iko wazi tatizo mkipewa fursa ya kuuliza mnakaaa kimya tu mnabaki kulalamika mitandaoni tu BAADHI ya watanzania ni wanafiki
 
Mkuu inaelekea unataarifa Kuwa ipo kiwandani inapakwa rangi; ngoja wamalize itakuja tu.
 
kwanini msiende kuuuliza wizara husika milango iko wazi tatizo mkipewa fursa ya kuuliza mnakaaa kimya tu mnabaki kulalamika mitandaoni tu BAADHI ya watanzania ni wanafiki
Nini faida ya mitandao kama kila kitu lazima uende wizarani.
 
Hahahaha, NDEGE YA NYONGEZA! Kule kijijini kwetu Isanje ukinunua dagaa kwa kipimo cha bakuli sawa na TZS 500 unalalamika kwa muuzaji yaani nimekuchangia/nimekuungisha halafu hata huongezi kama ni hivyo kesho sinunui kwako. Hatimaye anakuongeza dagaa kiasi kidogo ujazo wa kiganja cha mtoto mchanga aliyezaliwa jana ili asipoteze wateja maana anajua utaenda kumtangaza kwa watu wengine kuwa upimaji wake unapunja.
 
Tukipewa ndege ya nyongeza ikiletwa ujue tumepigwa kipigo cha mbwa mwizi,kwa mzungu hakuna cha bure,akikupa cha bure kama siyo wewe umepigwa atakuwa amepigwa mwenzako au alipigwa babu yako ndioukapewa kitu cha bure, hata ndege hiyo ya nyongeza ikija haitakuwa imetolewa bure japokuwa itatajwa kama ndege ya nyongeza huku watoaji wa nyongeza wakitung'ong'a na kusema wajinga ndiowaliwao.
 
Nakumbuka baada ya kununua Boeing 787 Dreamliner kwa cash rais alisema wazungu (Boeing) wamefurahi sana, akasema wameahidi kutupa ndege nyingine ya nyongeza bure.

Tayari Dreamliner imeshafika, nauliza tu ile ndege ya nyongeza tumeshapewa au bado iko kiwandani inamaliziwa kupakwa rangi.

Wajinga ndio waliwao.

CC: Msemaji wa serikali.
Watanunuwa kwa hela zetu,halafu watasema wamepewa nyongeza bure.WAJINGA NDIYO WALIWAO.
 
Nakumbuka baada ya kununua Boeing 787 Dreamliner kwa cash rais alisema wazungu (Boeing) wamefurahi sana, akasema wameahidi kutupa ndege nyingine ya nyongeza bure.

Tayari Dreamliner imeshafika, nauliza tu ile ndege ya nyongeza tumeshapewa au bado iko kiwandani inamaliziwa kupakwa rangi.

Wajinga ndio waliwao.

CC: Msemaji wa serikali.
Kwanza wamalize kurekebisha Wi-Fi
 
Back
Top Bottom