Bodi ya Sukari: Sukari ipo ya kutosha na nyingine inashushwa bandarini Dar na nyingine ipo mpakani Kasumulu inaingizwa kutoka Malawi

Prof. Keneth Bengesi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa bodi ya sukari amesema taifa lina sukari ya kutosha na huu uhaba bandia umesababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kuficha bidhaa hiyo.

Prof Bengesi amesema kwa sasa kuna tani nyingi za sukari zinashushwa bandarini Dsm lakini pia kuna tani za kutosha ambazo tumeimport kutoka Malawi ziko mpakani Kasumulu zinafanyiwa clearance ni zitaingia madukani muda wowote ule kuanzia leo.

Bengesi amesema yatafanyika marekebisho ya bei elekezi ya sukari kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Dsm, Tanga, Arusha nk

Chanzo: Channel ten!

BEI ITAPANDA AU ?
WAFANYE 4000/=
 
La msingi Serikali ilete sukari yakutosha na iiuze kwa TSH 1000, kama kweli kuna mtu ameficha sukari lazima aitoe tu ili angalau apate hiyo Tsh1000.. Serikali ifanye hivi kwa mwaka mmoja tu halafu uone kama kuna mtu ataleta mchezo..
 
Prof. Keneth Bengesi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa bodi ya sukari amesema taifa lina sukari ya kutosha na huu uhaba bandia umesababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kuficha bidhaa hiyo.

Prof Bengesi amesema kwa sasa kuna tani nyingi za sukari zinashushwa bandarini Dsm lakini pia kuna tani za kutosha ambazo tumeimport kutoka Malawi ziko mpakani Kasumulu zinafanyiwa clearance ni zitaingia madukani muda wowote ule kuanzia leo.

Bengesi amesema yatafanyika marekebisho ya bei elekezi ya sukari kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Dsm, Tanga, Arusha nk

Chanzo: Channel ten!
Huyu wa kutumbuliwa tu watu wanahangaika yeye katulia hadi Waziri anaingilia kati yeye katulia leo anatuletea ngonjera alikuwa wapi hadi hali imefika hapa tulipo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sukari ipo ya kutosha.

Ila tumeimport nyingine kutoka Malawi.

Mmmmhhhh so unayo ila umenunua nyingine kutoka Malawi? Ya nini sasa wakati unayo?

Hapa mtaani kwangu sukari ipo duka moja tu, Kilo 4000.
Waripoti kwa mamlaka hao, ni walanguzi
 
Mkuu Yohanmbatizaji asitudanganye kama watoto wadogo sukari hakuna, wanategemea hiyo waliyo-import ndiyo waingize sokoni. Kama ipo wameagiza ya nini?
Hivi inaingia akilini kusema kuna wafanyabiashara wameficha sukari na waachwe tu huku raia wanateseka kutafuta sukari ilipo?

Unakumbuka kauli ya Gavana wa DSM? Alisema hivyo hivyo na kwamba atapitisha msako mkali na atataifisha akikamata sukari iliyofichwa. Wiki nzima imepita hawajaambulia kitu.

Ukweli ni kwamba kulikuwa na uzembe mkubwa sana ktk kuagiza sukari nje ili kuziba pengo ambalo viwanda vyetu huwa vinaacha. Kuepuka huo uzembe mzigo unasukumiwa kwa wafanyabiashara kwamba eti wameficha sukari.
Atakuwa ni mfanyabiashara mwenye funza kichwani ambaye ataficha sukari kipindi hiki cha uhaba, wakati ndiyo muda mzuri wa kupata super profit.


Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa watu wanajua wanaongoza mazoba tupu au?maana yanadanganya waziwazi.sisi tunayaona Mapumbavu tu Fulani. Jitu linalegeza domo sukari ipo nyingi.iko wapi?.wafanyabiashara wameifungia kwanini msiwakamate.maana hata madukani haiuzwi kwa bei elekezi na bado haipatikani
 
Ngoja kichwa kibovo kiongozi wa nchi wiki ijayo aongee. Utasikia Zambia afunge mipaka milele na wala asitutishe; kama sukari amna si waweke chumvi au muunguze pipi? mbona zamani tulifanya hivyo.
Wewe Ndugai spika wa Bunge wabane hivyohivyo..big up.
 
Anadai tatizo ni wafanyabiashara wasio na uaminifu, halafu anakiri kwamba wanaenda kubadili bei elekezi, yani serikali inapandisha bei!

Bei elekezi ilikuwa unrealistic. Serikali haijali au haijui gharama ya kufikisha sukari dukani.
Haya ni matatizo yanasababishwa na serikali, bei elekezi wanakaa ofisini wanafikiri fikiri wanaamua iwe hivi, hata boss akisikia bei hii atafurahi. Hawaendi field kujua kiwandani bei gani, muuzaji mkubwa anauzaje na muuzaji wa mwisho anaipata kwa bei gani.
Siwapendi sana ma DC na RC, wanajua hali halisi, lakini bado watachukuwa kamera na kuendesha kamata kamata, waonekane hii inatokea hata kwenye mbolea na hata sembe!
 
Mbona maswali ni mengi kuliko majibu.
-Kama sukari ipo ya kutosha nchini kwanini serikali iagize mzigo mwingine nje?
-Kama sukari ipo ya kutosha nchini, kwanini serikali itangaze bei ipande?
-Kama sukari ipo ya kutosha, kwanini haipatikani madukani?
 
Ujinga wa Wa Hali ya Juu ni Ule kuamini kwamba kila Kitu kilichokosewa ni Hujuma...Kila Kitu Beberu ooh beberu..Nchi Hii haiwezi kwenda kwa kutafta wa kusukumia lawama..Nchi lazima iongozwe kwa makubaliano ya Wote...Na kufuata Sheria hivi kweli Mtu awe na sukari afiche ili iweje??

Niliona siku moja hawa wenye viwanda hapa Tz wanasingizia kwamba wana sukari nyingi sana na Haiuzwi kwasababu kuna Sukari Nyingi toka nje...Sasa iko wapi??? wanaonunua sukari wanasema wazi sukari kutoka Brasil mpaka hapa ina bei nafuu zaidi kuliko sukari kutoka Moshi au Mtibwa hapo.

Serikali Inakosea sana Kufanya mambo namna hii sasa Sukari ni elf 4 mambo ya kijima yale yamerudi tena hakuna Sukari Kabisa ni aibu sana..Kila mahala haipo iliyopo bei ghali sana ...tukubali kuna jambo limeenda tofauti sana kwa serikali hii na wengine wote wanakariri wa kutupia lawama.
 
Back
Top Bottom