Bodi ya Sukari: Sukari ipo ya kutosha na nyingine inashushwa bandarini Dar na nyingine ipo mpakani Kasumulu inaingizwa kutoka Malawi

Prof. Keneth Bengesi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa bodi ya sukari amesema taifa lina sukari ya kutosha na huu uhaba bandia umesababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kuficha bidhaa hiyo.

Prof Bengesi amesema kwa sasa kuna tani nyingi za sukari zinashushwa bandarini Dsm lakini pia kuna tani za kutosha ambazo tumeimport kutoka Malawi ziko mpakani Kasumulu zinafanyiwa clearance ni zitaingia madukani muda wowote ule kuanzia leo.

Bengesi amesema yatafanyika marekebisho ya bei elekezi ya sukari kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Dsm, Tanga, Arusha nk

Chanzo: Channel ten!
Ipo kweli na mimi tayari nimejipanga mstari hapa Kasumulu Kyela nasubiri bodi waanze kutuuzia, mimi uwezo wangu ni kilo moja tu.
Bodi ya Sukari ilizembea haikuagiza sukari kwa wakati, sisi hatuhitaji sukari bandarini wala boda tunahitaji sukari madukani, serikali iuchukulie hatua uongozi wa bodi ya Sukari.
 
Baada ya kunywa uji bila sukari leo unaamka na akili angalau kidogo. Eti serikali... :D :D :D. Kumbe unajua kuwa kuna serikali eeh? Basi sasa ipo siku utatamani tuwe na bunge pia
Wewe, mimi siyo kama nyie.
Mimi huwa nareason. Sijashikiwa akili na mwenyekiti wa chama kama bavicha mlivyo shikiwa na mwenye kiti wenu.

Mimi penye kukosoa na kosoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nazani hii bodi ya sukari kuna tatizo! Na kwakuwa hali hii ya tatizo la suksri sasa imejirudia kwa mara ya pili , ni wakati sasa wa serikali na bodi yake kujitazama upya namna inavyoshughulikia suala zima la uzalishaji na uingizaji wa sukari pamoja na usambazaji wake! Ni jambo la ajabu katika kipindi hiki ambacho tayari tuna mifumo ya kielektroniki ya kila aina eti bodi ya sukari haina mfumo wa kutrace au kuweka taarifa ya sukari inanunuliwa na nanin na inakwenda wapi, inauzwa kwa nani na nani? Ninaamini kama bodi ingekuwa na mfumo wa kuweka vizuri hizi taarifa zote tusingeweza kuanza kupiga ramli ya kutafta sukari imefichwa na nani? Inashangaza na kusikitisha sana eti bodi inajuwa kuwa sukari ipo , lakini haijui ipo wapi?....Pia jambo hili ni vema likaifumbua serikali macho itambuwe kuwa si kila kitu unweza kukitatua kwa amri sababu tu una polisi wa kukamata na mahakama za kuhukumu, bali mambo mengine yanahitaji muafaka wa pamoja kufikia suluhu ya kudumu! Hivyo kuendelea kuamrisha wafanyabiashara kufuata bei elekezi bila kufanya bussiness analysis kunaweza kuliongeza tatizo hili badala ya kulitatua!...
 
Mchezo hapa ni mdogo viwanga vinajulikana na wanunuzi wa kuu wanajulikana why wasi ulize kiwana nani alinunua kwa kiasi gani alafu ndo wakaMulize alipo ipeleka au wananufaika wao kwa virushwa vidogo vidogo
 
Ngonjera zisizo isha, hawa wenye viwanda huwa wanalalamika soko sukari zao zimejaa hakuna wanunuzi sasa inakuwaje tena shida? Kipindi hiki si ndiyo wangezalisha kwa wingi? Nchi tunamatatizo flani vichwani naona Mungu hutusukumizia duniani bila kumalizia vitu kwenye ufahamu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachoelewa mimi bidhaa ikiadimika maana yake uzalishaji wake umepungua sana au kiwanda kimefungwa ndipo wafanyabiashara wanabagain bei kutokana na uhitaji wa bidhaa yenyewe.

huuu UMBUMBUMBU wa kuiaminisha jamii kwamba wafanyabiashara wameficha bidhaa sijui awamu hii ya Meko wameutoa waaapi!!!!!?

Suala linaeleweka viwanda vyetu vya ndani havina uwezo wa kukidhi mahitaji ya sukari kwa nchi nzima alafu bidhaa inakuja inaadimika wanawasingizia wafanyabiashara





Foooooooolish one alafu nimewamind๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ

๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ๐Ÿ˜ˆ
 
Prof. Keneth Bengesi ambaye ni mkurugenzi mkuu wa bodi ya sukari amesema taifa lina sukari ya kutosha na huu uhaba bandia umesababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu kuficha bidhaa hiyo.

Prof Bengesi amesema kwa sasa kuna tani nyingi za sukari zinashushwa bandarini Dsm lakini pia kuna tani za kutosha ambazo tumeimport kutoka Malawi ziko mpakani Kasumulu zinafanyiwa clearance ni zitaingia madukani muda wowote ule kuanzia leo.

Bengesi amesema yatafanyika marekebisho ya bei elekezi ya sukari kwa baadhi ya mikoa ikiwemo Dsm, Tanga, Arusha nk

Chanzo: Channel ten!
Katika mikoa ilioathirika na bei elekezi ni mikoa ya Mbeya, Songwe na Rukwa. Kabla ya bei elekezi sukari ilikuwa inauzwa kati ya sh. 2,500/= na 2,800/=, sasa kwa mfano Rukwa inauzwa 3,200/=.

Tunalaani vikali serikali kuingilia biashara ya sukari.
 
Tatizo bei elekezi inatolewa kwa uzaji wa rejareja. Kwanini wasiitoe kwa wauzaji wa jumlajumla. Ukipunguza jumlajumla bei inashuka yenyewe, lakini hii serikali inapungunza kwa rejareja. Hakuna mfanyabiashara anayependa kupata hasara. Hii serikali haina huruma kabisa kwa wamanchi wake.
Ndio muitoe sasa bei elekezi itashuka soon!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Put it this way

Juma anazalisha na kuuza peremende kinondoni wateja wake wakubwa wanafunzi wa shule ya msingi na chekechea.

Uwezo wa Juma kuzalisha peremende ni 1000 kwa wiki mahitaji ya watoto kwenye pipi ni elfu mbili kwa wiki.

Wafanyabiashara wengine wanajitokeza kuziba hilo pengo kwa kuagiza na kuuza kwa bei nafuu na wanauewezo wa kuleta zaidi iwapo wataruhusiwa.

Wazee mtaani wanasema hapana hawa jamaa watamuondoa Juma kwenye biashara na familia yake inamtegemea.

Haya tunamuweka Mzee Rajabu kazi yake kusimamia wanaoagiza kuakikisha awaleti madhara atakuwa anawapa kibali cha kuagiza kufikia mahitaji kuziba pengo la Juma.

Ulaji wa pipi wenyewe nao unatofauti, kipindi cha likizo watu badala ya kula pipi 2000 kwa wiki kwa sababu watu wapo nyumbani siku nzima ulaji wa pipi una panda mpaka 5000 kwa wiki.

Watu wanaoagiza pipi kutoka huko zinakotoka hadi kufika inachukua mwezi kuanzia wanapotoa order; yeye mzee Rajabu alijua kuna likizo mwezi wa sita inakuja badala ya kutoa kibali tangia mwezi tano cha pipi 4000 zitakazofika mwezi wa sita yeye anatoa kile kile cha kuagiza pipi 1000.

Inafika mwezi wa sita sokoni kuna pipi 2000 tu za Juma 1000 na za kuagiza 1000. Mzee Rajabu kwakuwa awezi kazi na watoto majumbani wanasumbua wazazi wanataka peremende. Mzee Rajabu anaanza kusingizia waagizaji kwa wazazi wameficha peremende ili walangue sijui hiki na kile; wakati nyuma ya pazia anaagiza pipi kwa kuficha uzembe wake.

Sasa kwa wafanyabiashara private sector hiyo scenario wao washazoea kujipanga. Isipokuwa serikarini tumejaza maprofessor uchwara hata simple operation logistic zinawashinda.

2025 nchi inahitaji raisi atakaekuja kubadili civil services imejaza viazi wengi mno.
 
Back
Top Bottom