Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) yakanusha Taarifa kuwa Haina Fedha za kulipa wanafunzi

Wengine tuna anza mitihani jumatatu afu una tusainisha leo izo pesa ambazo tulipaswa kupewa wiki3 nyuma huo ni uhakiki uchwara.. Period
Hahahahahaaaaa! Hiyo mitihani mnafanyia hapo Ufipa?
 
Hakuna taarifa iliyo kua imetolewa kabla vyuoni muwe mnafatilia kwanza sio kusifia kila jambo
Haya ni mambo ya kiutawala. Ulitaka watoe u tangazo hata kwa wasiohusika?
 
HESLB YAKANUSHA KUWA HAINA FEDHA

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.

Si kweli kwamba Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.

Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE 2 JULAI 2016

Mytake: Hakika UKAWA wanazidi kuumbuka. Kila wakitoa uzushi, majibu yanatolewa mapema na hivyo kujikuta wakizama shimoni. Na bado

Source: Michuzi Blog
Hebu tafuteni uongo mwingine bas.... Mm ni Mwanachuo na hakuna Pay sheet yoyote iliyofika vyuoni.... Hadi Jana Majibu ya bodi ni kwamba hawajapewa hela na Hazina.......
 
Nina clip ambazo kaimu mkurugenzi wa bodi ya mikopo amepigiwa simu akakiri kuwa hamna pesa, viongozi wa vyuo wameenda kufuatilia mikopo pale bodi wakaambiwa hamna pesa, wakaenda hazina wakaambiwa warudi bodi, hakuna uhakiki wowote wa wanafunzi uliofanyika,.
Muache kutesa watoto wa wanyonge na msitetee ujinga hapa.
 
Mkuu, ni jambo gani Serikali iliwahi kukanusha then jambo likabaki kama lilivyo?
Angalia matamko ya TAMISEMI kauli zilizotofautiana Kati ya waziri na naibu waziri kuhusu ajira za walimu tangu mwanzoni mwa mwaka, halafu walishatoa makanusho Kama mawili hivi kuhusu ajira za walimu hadi Leo hizo ajira zipo si kila siku wanabadili sababu, haya cheki sasa na hili bumu la wanafunzi unafahamu ni mda gani watu hawajapata hiyo pesa ya kujikimu halafu hawa wanakuja na sababu za "uhakiki" halafu tena unaongezewa na wiki zingine za kusubiri hawajui kuwa wengine wanategemea hilo bumu kulipa baadhi ya michango ya chuo na UE kwa baadhi ya vyuo ndo inaanza wiki ijayo, aaagh inachosha Sana ndo maana huwa siwapendi wanasiasa mpaka basi. Mkuu niwe muwazi tu sina imani kabisa na matamko ya hii serikali mpaka nione matokeo yake.
 
Fedha hakuna,wanafunzi wamebakisha wiki 3 wafunge bado hawajapewa pesa mnaleta ngonjera hapa za kuhakiki!Mnatetea ujinga,period
..halafu wakati huo huo ndio wanategemea mwanafunzi afaulu vizuri mitihani yake ya Chuo ya Mwisho wa semester wakati hata pesa ya kununua maji shida.

Hii serikali ya ccm imejaa wababaishaji wengi.
 
Hebu tafuteni uongo mwingine bas.... Mm ni Mwanachuo na hakuna Pay sheet yoyote iliyofika vyuoni.... Hadi Jana Majibu ya bodi ni kwamba hawajapewa hela na Hazina.......
Kwani pay sheet wanakabidhiwa wanavyuo? Hahahahahaaaaa! Kweli machadema yamechanganyikiwa.
 
Hebu tafuteni uongo mwingine bas.... Mm ni Mwanachuo na hakuna Pay sheet yoyote iliyofika vyuoni.... Hadi Jana Majibu ya bodi ni kwamba hawajapewa hela na Hazina.......
..Halafu kuna watu wa ajabu kama huyu lizardbone kazi yao ni kushabikia na kukifanya mjuaji wa kila jambo, wakati hajui kinachoendelea vyuoni.
Sometimes it's better kama hujui jambo ni bora ukaa kimya kuliko kujifanya mjuaji cz kuna wanafunzi humu wa vyuo vikuu tunamshangaa tu jinsi mleta mada anavyo bwabwaja.
 
Yaan dah........ Inaumiza.....Watu wengine wanashindia mikate na maji kila cku..... Wengine tunaishi off campuses... Nauli kila cku bado hujadaiwa hela ya LUKU.. Mara maji............. It's so painful to live like a beggar in your own country......
 
HESLB YAKANUSHA KUWA HAINA FEDHA

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.

Si kweli kwamba Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.

Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE 2 JULAI 2016

Mytake: Hakika UKAWA wanazidi kuumbuka. Kila wakitoa uzushi, majibu yanatolewa mapema na hivyo kujikuta wakizama shimoni. Na bado

Source: Michuzi Blog
Na walio hakikiwa na wakapewa boom but hela ya field hawajapata wala kusign hadi leo unazungumziaje??? Au na hao pia wana hakikiwa?? mara ya pili
 
Kwani pay sheet wanakabidhiwa wanavyuo? Hahahahahaaaaa! Kweli machadema yamechanganyikiwa.
And by the way I'm not a politician... I think hujawah kuona comment yang yoyote huku except today ... I just commented bcoz I know the real situation and you people trying to cover the truth....... Unaleta siasa wakati watu tunaumia..... Jumatano wanatusambazia magazeti ya Jambo Leo et tuone kwamba hata wabunge wanadai posho.... Are we the same with them???
 
Sio bodi ya mikopo tu serikali nzima haina pesa ndio maana hata watumishi waluoajiriwa mei wamerudishwa...ndio maana wamekazana huku kwenye 18% wakusanye ndo haueni.
 
Back
Top Bottom