Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) yakanusha Taarifa kuwa Haina Fedha za kulipa wanafunzi

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,375
HESLB YAKANUSHA KUWA HAINA FEDHA

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

TAARIFA KWA UMMA
KUKANUSHA TAARIFA KWAMBA BODI HAINA FEDHA

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inapenda kukanusha taarifa za upotoshaji zinazoenezwa kwa sasa kwamba haina fedha.

Si kweli kwamba Bodihaina fedha, ila ni kweli kwamba kumekuwa na ucheleweshaji wa kufikisha fedha za wanafunzi vyuoni kutokana na zoezi la kuhakiki wanafunzi wanaonufaika na mikopo linaloendelea vyuoni hivi sasa.

Hata hivyo, maandalizi ya malipo hayo yameshafanyika na ‘pay sheets’ zimeshapelekwa vyuoni tayari kwa wanafunzi wanaonufaika na mikopo kusaini.

Bodi inatarajia wakati wowote wiki ijayo baada ya zoezi la uhakiki kukamilika; itapeleka fedha hizo vyuoni.

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
TAREHE 2 JULAI 2016

Mytake: Hakika UKAWA wanazidi kuumbuka. Kila wakitoa uzushi, majibu yanatolewa mapema na hivyo kujikuta wakizama shimoni. Na bado

Source: Michuzi Blog
 
Ukweli ni kwamba fedha hakuna. Hizo ni danganya toto. Kwanza hizo taarifa kwenye website ya bodi hakuna. Usituletee habari za kutunga hapa.
Kwani kila taarifa ni ya kutunga? Ama mmezoea kutunga uongo? Subirini wiki ijayo si mbali. Mtaendelea kuumbuka mchana kweupe
 
Mkuu ukawa hawana hoja ya maana kabisa .

Walichobakiza ni kutunga uongo tu .

Walitunga uongo kupotosha wananchi kwamba ikifika tarehe 1/7 watu watakatwa pesa sana lkn Leo ni tarehe 2/7 hamna mwananchi aliyekatwa !!!

Ufipa sasa wanatoa macho tu baada ya uongo wao kuumbuka.

Ngoja tusubili kufika kesho watakuja na uongo na uzushi gani tena
 
Hii serikali kila siku ni kukanusha tu halafu mambo yanaendelea kuwa yaleyale.sijui huwa wanaangalia upepo unaendaje.
Mkuu, ni jambo gani Serikali iliwahi kukanusha then jambo likabaki kama lilivyo?
 
Mkuu ukawa hawana hoja ya maana kabisa .

Walichobakiza ni kutunga uongo tu .

Walitunga uongo kupotosha wananchi kwamba ikifika tarehe 1/7 watu watakatwa pesa sana lkn Leo ni tarehe 2/7 hamna mwananchi alikatwa !!!

Ufipa sasabwanatoa macho tu baada ya uongo wao kuumbuka
Ufipa wote akili zao zimeshikwa na DJ Ziro
 
Kwani kila taarifa ni ya kutunga? Ama mmezoea kutunga uongo? Subirini wiki ijayo si mbali. Mtaendelea kuumbuka mchana kweupe
Fedha hakuna,wanafunzi wamebakisha wiki 3 wafunge bado hawajapewa pesa mnaleta ngonjera hapa za kuhakiki!Mnatetea ujinga,period
 
Fedha hakuna,wanafunzi wamebakisha wiki 3 wafunge bado hawajapewa pesa mnaleta ngonjera hapa za kuhakiki!Mnatetea ujinga,period
Kwani ulikuwa hujui kuwa Serikali ilikuwa inahakiki wafanafunzi ili kujua kuna wanafunzi hewa wangapi? Wanafunzi wenyewe wanajua nini kinaendelea. Ila ninyi ambao hata form four hamjamaliza ndio maana mnaendelea kutumga uongo
 
Kwahiyo serikali inaenda kuhakiki chuo kimoja ikimaliza inaenda kingine mpaka cha mwisho?Acha ujinga,suala la uhakiki lingeweza kufanyika vyuo vyote kwa wakati mmoja!Hizi delays ni kwasababu fedha ni tatizo!Rudisha ufahamu ndio utaelewa,period!
 
Wengine tuna anza mitihani jumatatu afu una tusainisha leo izo pesa ambazo tulipaswa kupewa wiki3 nyuma huo ni uhakiki uchwara.. Period
 
Kwanini hizi taarifa hazitolewi mapema ili watu wajue mustakabali wao. wanasubiri watu wapige kelele ndo watoe matamko ambayo mwisho wa siku yanatugharimu
 
UKAWA wataendelea kudhalilishwa na mambo kama haya ya kutunga uzushi!
 
Kwahiyo serikali inaenda kuhakiki chuo kimoja ikimaliza inaenda kingine mpaka cha mwisho?Acha ujinga,suala la uhakiki lingeweza kufanyika vyuo vyote kwa wakati mmoja!Hizi delays ni kwasababu fedha ni tatizo!Rudisha ufahamu ndio utaelewa,period!
Pole sana. Endelea kuamini hivyo.
 
Wengine tuna anza mitihani jumatatu afu una tusainisha leo izo pesa ambazo tulipaswa kupewa wiki3 nyuma huo ni uhakiki uchwara.. Period
Hatuwezi kuacha uhakiki kwa sababu yako...
 
Kwanini hizi taarifa hazitolewi mapema ili watu wajue mustakabali wao. wanasubiri watu wapige kelele ndo watoe matamko ambayo mwisho wa siku yanatugharimu
Taarifa zinatolewa kwenye vyuo husika. Ila Ufipa ndio kawaida yao kutunga uongo.
 
Back
Top Bottom