Bodi ya mikopo: Vijana CCM ni wazushi

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
645
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), imeurarua Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kutokana na kile ilichokiita ni kutoa taarifa, "za kizushi na za kukurupuka," na kutaka isigeuzwe jimbo la uchaguzi la wanasiasa.Tamko hilo la HESLB chini ya kichwa cha habari, "Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu haihusiki na Migomo ya hivi karibuni katika Vyuo vya Elimu ya Juu," linajibu mapigo ya tamko la UVCCM, lililotaka mapinduzi ndani ya bodi hiyo ikiituhumu kushindwa kukidhi mahitaji ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

Hata hivyo, ikitoa ufafanuzi wa tuhuma moja hadi nyingine kati ya zilizoelekezwa kwake, bodi ilipiga kombora ikisema, "mmoja wa viongozi UVCCM, amekitolea mfano Chuo Kikuu kishiriki Mkwawa (MUCE) kama mfano, wakati akitoa tamko la kukurupuka dhidi ya bodi bila hata kufanya uchunguzi wa sababu za ndani za migomo ya wanafunzi wa vyuo."

Vijana hao wa CCM katika tamko lao, walisema, “UVCCM umebaini kuna urasimu unaofanywa na watendaji na haiingii akilini, Mkwawa University wagome kwa kutolipwa posho zao na baada ya siku moja walipwe posho zao baada ya kugoma. Jambo hili si utamaduni wa vijana wa Kitanzania, wale wote wanaohusika CCM ichukue hatua,”

kweli ni wanafiki watupu. Wakumbuke mwaka 2004 chini ya Deodurius Kamala walitoa tamko la kussuport bodi hiyo. Wakati huo chuo kikuu walifukuzwa kwa kugomea muswada huo na kama mnakumbuka Bwana David Tweve aliongoza mgomo huo, sasa leo iweje bodi iwe mbaya mbele ya macho yao ? Takataka tu.
 
UVCCM's poor calculations, hawakumbuki hata mambo ya jana tu. Na hao ndiyo eti viongozi watarajiwa!!
 
Na katika mkutano wao na Jukwaa la Wahariri walisema 'No research No right to speak'.....sasa sjui walifanya research gani? Tusubiri watareact vp!

Na kwa upande mwingine ndicho nilichotarajia kutoka Bodi (HESLB) wasingekaa kimya wakati kitumbua chao kinamwagiwa mchanga...
 
Nasikia kichefuchefu nikisikia kitu kinachoitwa UVCCM..........!
 
hawa jamaa ningewaona wamaana kama wangeanza kufuatilia agizo la mwenyekiti wao wa taifa ccm, kuhusu swala la bodi la kua na account yao ambayo hela toka hazina zingeiingia moja kwa moja na kuachana na mtindo wa hela hizo za mikopo kwa wanafunzi kupitia wizara ya elimu na baadae zipilekwe bodi... je limetekelezwa... ?!!!
 
CCM ichukue hatua?? these i.diots are on drugs! lol
Hiyo inaonesha jinsi hawa vijana wa ccm walivyo na mawazo mgando... vijana wanamawazo sawasawa na wazee wao, hawana fikra mpya... lakini ukiangalia kwa umakini kabisa hawa vijana walitumia karata ya bodi ili kujaribu kurudisha fikra za vijana kwenye chama chao, kitu ambacho hakitofanikiwa kamwe kwani vijana washachoka na mienendo yao....:sick:
 
Hongera sana bodi mikopo mnajitahidi sana najuaa kuna urasimu sana wizara fedha hadi wizara yenu pia mnapewa pesa mafungu mafungu sana.......ila mnajtahidi hao uvccm nafikiria muda wao umefika watafute shughuli ingine pale isiwe kijiwe cha kuficha njaa zao....watafute kazii zingine wafanye waache unafiki!
 
BODI ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), imeurarua Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kutokana na kile ilichokiita ni kutoa taarifa, "za kizushi na za kukurupuka," na kutaka isigeuzwe jimbo la uchaguzi la wanasiasa.Tamko hilo la HESLB chini ya kichwa cha habari, "Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu haihusiki na Migomo ya hivi karibuni katika Vyuo vya Elimu ya Juu," linajibu mapigo ya tamko la UVCCM, lililotaka mapinduzi ndani ya bodi hiyo ikiituhumu kushindwa kukidhi mahitaji ya wanafunzi wa elimu ya juu nchini.

Hata hivyo, ikitoa ufafanuzi wa tuhuma moja hadi nyingine kati ya zilizoelekezwa kwake, bodi ilipiga kombora ikisema, "mmoja wa viongozi UVCCM, amekitolea mfano Chuo Kikuu kishiriki Mkwawa (MUCE) kama mfano, wakati akitoa tamko la kukurupuka dhidi ya bodi bila hata kufanya uchunguzi wa sababu za ndani za migomo ya wanafunzi wa vyuo."

Vijana hao wa CCM katika tamko lao, walisema, "UVCCM umebaini kuna urasimu unaofanywa na watendaji na haiingii akilini, Mkwawa University wagome kwa kutolipwa posho zao na baada ya siku moja walipwe posho zao baada ya kugoma. Jambo hili si utamaduni wa vijana wa Kitanzania, wale wote wanaohusika CCM ichukue hatua,"

Salhadoxine mbona hujatupa nyama kwenye mada yako jinsi bodi ya mikopo ilivyojibu hoja za uvccm? Nilivyoona kichwa cha habari nilitegemea utatupa fulldata
 
wazushi si kidogo! wameona njia ya kupata wafuasi wengi sasa ni maandamano ya kupinga, wanampinga nani? kwa nini wasimwambie Mwenyekiti wa Chama chao asiishughulikie Bodi ya Mikopo! Maajabu ndo sihasa!
 
Hawa UVCCM wameshaona chama chao kinakufa sasa wanatafuta pakutokea.......Tumewasomaaaaaa......tumewafahamuuuuuu.......Tumewagunduaaaaaaa...........HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Chuo Kikuu wamepinga mawazo ya UVCCM. Sasa wanajiharibia kudandia hoja zisizowahusu za kutaka kuwawajibisha watu ambao hawakuwaweka kwenye BODI. Labda wana agenda ya siri ila wameingia vibaya. Wajipange waanze upya.
 
Back
Top Bottom